2 days ago

Michuzi

Waziri Mwakyembe akutana na wasanii wa sanaa ya uchongaji kutatua changamoto ya umiliki wa eneo la Mwenge

Na Genofeva Matemu – WHUSMWaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa tasnia ya sanaa ya uchongaji haiwezi kuendelea kama mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge utaendelea kuchukua nafasi kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku hivyo kushindwa kujiinua kiuchumi na hata kushindwa kuchangia katika pato la taifa.Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na wasanii wachongaji pamoja na wafanyabiasha wa kazi za...

 

1 month ago

Michuzi

TAMASHA LA BUSARA KUENZI SANAA NA UTAMADUNI WA MWAFRIKA

. Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao. 
Hayo yamesema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe, Unguja - Zanzibar kwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbali mbali vya sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya.
 “Katika Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali hukutana,...

 

2 months ago

Michuzi

Msanii Pretty Kind afungiwa kujihusisha na kazi za Sanaa kwa muda wa Miezi Sita, Giggy Money aitwa kujieleza

Na Anitha Jonas – WHUSM ,Dar es Salaam

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amemfungia Msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kujihusisha na shughuli za Sanaa kwa muda wa miezi sita.
Naibu Waziri Shonza amechukua hatua hiyo leo jijini Dar es Salaam kutokana na msanii huyo Kutoa wimbo usiyo na maadili wenye jina la ‘’Viduduwasha’’, Kufanya kazi ya Sanaa bila kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, pamoja na kuweka mtandaoni picha ya nusu utupu...

 

2 months ago

Michuzi

SERIKALI YA KUTANA NA WADAU WA SANAA KUJADILI KUHUSU SUALA LA MAVAZI KWA WASANII

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wadau wa Sanaa (hawapo pichani) kuhusu nini kifanyike kwa mavazi ya wasanii sababu ya kuwepo kwa wasanii wengi wanaovaa mavazi yanayokiuka na maadili ya kitanzania katika kikao chake na wadau mbalimbali wa Sekta ya Saana nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey...

 

2 months ago

BBCSwahili

Kwa Picha: Warsha ya kuonyesha sanaa na vipawa iliyoandaliwa Nairobi

Warsha ya kuonyesha sanaa na vipawa mbalia mbalia imeandaliwa mjini Nairobi Kenya kwa lengo la kusherehekea ubunifu katika kanda nzima ya Afrika mashariki.

 

3 months ago

Zanzibar 24

Diamondplatnumz atumia sanaa kutuma salam kwa wapenzi wake wa zamani

Supastaa Diamondplatnumz ametuma salamu nzito kwa waliokuwa wapenzi wake kupitia nyimbo mbili maridhawa zinazowazungumzia wapenzi wake hao.

Supastaa huyu asieisha visa katika maisha yake ya mapenzi aliachia wimbo wa sikomi uliojikita kuelezea maisha yake ya kimapenzi tangu anaanza safari ya muziki ukianza na maneno kama “Ile pru mpaka Makka nikadandia kwa Bongo movie, kumbe mapenzi hayataki haraka, ni kama tango unatia tu chumvi… mwenzenu nikaoza haswa, na kujitia kitandani mjuzi, eti nataka...

 

3 months ago

Michuzi

Mtandao wa Muziki Tanzania waipongeza Msama Auction Mart KWA KAZI NZURI YA KUPAMBANA NA UHARAMIA WA KAZI ZA SANAA

kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiendelea nayo muda mrefu ya kukamata wezi wa kazi za muziki na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kupunguza uharamia na kuhamasisha uchangiaji wa pato la Taifa kupitia kazi za sanaa. 
Katika pongezi hizo Mwenye kiti wa Tanzania Musicians Network , John Kitime amesema, 'Kwa niaba ya wanachama wa chama chetu Tanzania Musicians Network, naomba nitoe shukrani kwa mchango wako mkubwa ambao kampuni yako inaufanya katika jitihada za kupunguza uharamia wa kazi za sanaa...

 

3 months ago

Michuzi

MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA KAMPUNI YA MSAMA AUCTION MART KUSAIDIA KUTOKOMEZA UHARAMIA WA KAZI SANAA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Shilingi Milioni 10 za Kitanzania kwa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart inayosimamia zoezi la kutokomeza kazi feki za sanaa nchini.
Kiasi hicho cha Pesa kimetolewa katika Kampuni hiyo ya Msama ili kuendesha vizuri mapambano dhidi ya wanaodurufu kazi hizo sehemu zote za jiji la Dar.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa Kampuni hiyo inamshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa...

 

3 months ago

Michuzi

WANAODURUFU KAZI ZA SANAA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.


 Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart imethibitisha kuwa Watuhumiwa wote waliokwamatwa kushiriki kufanya biashara ya kazi feki za sanaa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa Watuhumiwa hao watapelekwa Mahakamani kutokana na kuwa na kesi ya kujibu.

Ameendelea kusema ni kosa kuuza Kazi za Wasanii hao ambazo hazina Stika ya TRA, kwani zinawakosesha Mapato Wasanii...

 

4 months ago

Michuzi

KAMPUNI YA UDALALI YA MSAMA AUCTION MART YAENDELEA NA ZOEZI LA KAMATA KAMATA MAHARAMIA WA KAZI ZA SANAA NA WAKWEPA KODI.

Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeendelea na zoezi la ukamataji wa Wadurufu wa kazi za sanaa na wakwepa kodi kupitia kazi hizo.

Zoezi hilo limeendelea katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ambapo pia imesisitizwa kuendelea nchi nzima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza kwa shughuli hiyo, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart amewaasa...

 

4 months ago

Michuzi

TRA IKISHIRIKIANA NA MSAMA AUCTION MART YAENDELEZA MSAKO YA KUWABAINI WAKWEPAJI KODI KATIKA KAZI ZA SANAA


Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameendelea na zoezi la kupita Duka kwa Duka, Mlango kwa Mlango Lusaka wezi wa kazi za Sanaa na wakwepaji wa Kodi hapa nchini.

Zoezi hilo linaloendelea kwa nchi nzima, hapo jana liliendeshwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kamishna wa Kodi za Ndani - TRA, Elijah Mwandumbya amesema wameamua kufanya zoezi hilo ili kujiridhisha katika maduka ambayo yanafanya biashara...

 

4 months ago

Michuzi

DKT. MWAKYEMBE: KAZI ZA SANAA NA FILAMU ZIKIDHI SOKO KIMATAIFA

Na Genofeva Matemu, WHUSM, Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka Bodi ya Filamu pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa kuendelea kusimamia kazi za sanaa na filamu ili ziweze kukidhi soko la ndani na la kimataifa.

Waziri Mwakyembe amesema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu.

“Bodi...

 

4 months ago

Michuzi

EASTAFAB Kibwebwe kinachopigia chapuo Sanaa EAC

KADRI siku zinavyokwenda mbele, wadau wanaoguswa na sanaa hapa nchini wanasaka namna ya kusaidia tasnia hiyo ambayo ni eneo adhimu kwa jamii duniani. Mara nyingi wasanii wamekuwa wakilalamika kwamba wanafanywa kama yatima ambao wanakosa msaada wa kuwasogeza katika njia ya maendeleo baada ya kufanya kazi zao kwa ufanisi. Wasanii hulalamika katika matukio mbalimbali ya kazi zao, hali ambayo husababisha kuonekana kwamba tasnia hiyo sio eneo la kukimbilia kwa sababu ya malalamiko kutoka kwa...

 

4 months ago

CCM Blog

WAZIRI MWAKYEMBE NA NAIBU WAKE JULIANA SHONZA WASHIRIKI JUKWAA LA SANAA


===========
Na Mathias Canal, SingidaMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu amezindua msimu wa kilimo 2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi kuanza kujiandaa kwani tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia.
Katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji na kata ya Ihanja wilayani Ikungi Mhe Mtaturu pamoja na  mambo mengine lakini amewasihi kutumia vizuri mvua za mwanzo kupandia.
Katika mkutano huo wa uzinduzi  Mhe Mtaturu pia ameanzisha...

 

4 months ago

Michuzi

Prof. Elisante awaaga watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, DodomaKatibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel amewaaga watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo mjini Dodoma.Prof. Elisante awali ndiye alikuwa anaiongoza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya mabadiliko ya safu ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Alhamisi Oktoba 26, 2017.Prof. Elisante...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani