4 weeks ago

Zanzibar 24

Hukumu ya Scorpion mtoboa macho yakamilika

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Salum Henjewele maarufu ‘Scorpion’ aliyekuwa akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho, Saidi Mrisho, kwenda jela miaka saba na kulipa fidia ya shilingi milioni 30 kwa kosa la kujeruhi na wizi.

Baada ya mahakama kumkuta na hatia Salum Henjewele na kufungwa miaka saba ikiwa pamoja na kulipa fidia ya milioni 30, Saidi Mrisho ambaye alifanyiwa tukio hilo la kinyama amefunguka na kusema kuwa hajaridhika na maamuzi ya mahakama hiyo.

Said Mrisho amesema...

 

8 months ago

Mwananchi

Kesi ya Scorpion yashindwa kusikilizwa tena

Kwa mara ya sita mfululizo, kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njetwe, maarufu kama ‘Scorpion’ imeshindwa kusikilizwa baada mshitakiwa huyo kushindwa kufikishwa mahakamani.

 

8 months ago

Mwananchi

Kesi ya Scorpion yakwama kusikilizwa kwa mara ya tano

Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njetwe maarufu ‘Scorpion’ imekwama kuendelea kusikilizwa kwa mara ya tano mfululizo baada ya Hakimu alinayesikiliza shauri hilo kuwa mgonjwa.

 

9 months ago

Mwananchi

Kesi ya Scorpion yaahirishwa kwa mara nne mfululizo

Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njetwe maarufu ‘Scorpion’ imeshindwa kuendelea kusikilizwa kwa mara ya nne mfululizo baada ya wakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani.

 

10 months ago

Mwananchi

Shahidi akwamisha kesi ya Scorpion

 Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njetwe maarufu ‘’Scorpion’’  imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka  kudai shahidi ambaye walimtegemea kuendelea kuulizwa maswali na wakili anayemtetea Scorpion, kuwa  bado ni mgonjwa.

 

11 months ago

Global Publishers

Shahidi Kesi ya Scorpion Chupuchupu Kutupwa Lupango

Salum Njwete ‘Scorpion’ aliyeshika daftari.

DAR ES SALAAM: Mkazi wa Buguruni jijini hapa, Deus Johakim Magosa (45) ambaye ni shahidi wa nane upande wa Jamhuri katika kesi namba 303 ya mwaka 2016 ya kumjeruhi, kumtoboa macho na kumfanyia unyang’anyi wa kutumia silaha, Saidi Mrisho inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini, leo alinusurika kutupwa lupango baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga kumtuhumu kutoa ushahidi wa uongo.

Wakili Katuga...

 

11 months ago

Mwananchi

Shahidi adai Scorpion alikuwa mlinzi wa amani

Meneja wa Baa ya Kimboka iliyopo Buguruni Mnyamani,  Hussein Fundi (41) , ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala kuwa anamfahamu mshtakiwa Salum Njwete (34) kama mlinzi wa amani wa wafanyabiashara ndogondogo katika Barabara ya Mandela eneo la Buguruni Sheli.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani