(Today) 19 minutes ago

Channelten

Rais wa Marekani Donald Trump Aanza kufanyia mabadiliko sheria za Obama

1200

Rais mpya wa Marekania Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais, baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yaliyoafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama.

Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bwana Trump, alitia saini amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama Obama Care, ambayo Trump aliahidi kufanyia marekebisho.

Rais Trump pia ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri...

 

(Today) 3 hours ago

BBCSwahili

Sheria za uwekezaji Tanzania zinamfaa kijana?

Ripoti ya kila mwaka ya uwekezaji duniani ya mwaka 2015 inaonyesha Tanzania ilifanikiwa kuvutia ongezeko la 14.5% ya uwekezaji wa mitaji kutoka nje.

 

(Today) 6 hours ago

BBCSwahili

Trump aanza kufanyia mabadiliko sheria za Obama

Rais wa Marekania Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais, baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama.

 

(Today) 10 hours ago

MillardAyo

Sheria inasemaje pale Mshindi wa Urais anapoapishwa nje ya nchi kama Gambia?

Rais mteule wa Gambia ambaye alikimbilia Senegal kutokana na hali ya hatari Gambia baada ya Rais aliyeshindwa kwenye uchaguzi kugoma kuondoka madarakani, aliapishwa kwenye ubalozi wa Gambia kwenye nchi jirani ya Senegal. Sasa inawezekana na wewe umejiuliza kama mimi, kisheria imekaaje pale ambapo Mgombea anaeaminika kushinda kwa kura anakimbilia nchi jirani na kwenda kula kiapo […]

The post Sheria inasemaje pale Mshindi wa Urais anapoapishwa nje ya nchi kama Gambia? appeared first on...

 

(Yesterday)

Dewji Blog

Serikali kupitia upya sheria na kanuni za utangazaji

Serikali imejipanga kupitia upya kanuni za utangazaji za Sheria ya Utangazaji ya mwaka 2003 ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye wakati wa ziara yake kwa vyombo vya habari vya Channel, na Tumain Media iliyolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya Serikali na vyombo vya habari nchini.

Waziri Nape amesema kuwa lengo la mapitio ya kanuni hizo ni uboreshwaji wa kanuni hizo ili kuisaidia kukuza sekta ya...

 

(Yesterday)

Channelten

Serikali ipo katika hatua za awali za kufanya mapitio ya kanuni ya sheria ya utangazaji za mwaka 2003

Screen Shot 2017-01-20 at 4.49.12 PM

Serikali ipo katika hatua za awali za kufanya mapitio ya kanuni ya sheria ya utangazaji za mwaka 2003 ambazo zinatumika hadi sasa ili ziweze kuendana na mabadiliko ya technolojia na uhalisia wa taaluma ya utangazaji kwa sasa.

Channel Ten

“HAMID ABDULRAHMAN – Mkurugenzi wa Uendeshaji – AMGL (kushoto) akiwa na Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye wakizungumza jambo”.

Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ameyasema hayo alipotembelea Kampuni ya Africa Media Group...

 

2 days ago

Mwananchi

MAONI YA MHARIRI: Sheria izingatiwe mgogoro wenyeviti wa mitaa

Juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alitangaza kusitisha agizo la kuwataka wenyeviti wa Serikali za Mitaa nchini kukabidhi mihuri kwa maofisa watendaji mpaka pale utaratibu mzuri utakapotolewa.

 

2 days ago

Mwananchi

Sheria ya kuwabana wote wanaojiita ‘madaktari’ yaja

Serikali imekuja na Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi ambao utazuia watu kujiita madaktari bila kuwa na elimu ya kiwango cha shahada na kuendelea.

 

2 days ago

Michuzi

RAIS WA FIFA INFANTINO ATAKA SHERIA ZA SOKA KUBADILISHWA

Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka kabisa kwa kutaka kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta vyake hasa baada ya kupelekea mapendekezo ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48 na sasa amekuja na mpya ya kutaka kubadili namba ya kupiga penati.
Kwa kumtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten wamependekeza baadhi ya sheria mpya katika soka.Kuondoa offside.
Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten...

 

2 days ago

Dewji Blog

Serikali yaombwa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 itumike kuwalinda wanahabari

Wadau wa habari nchini wameendelea kuisisitiza serikali kuhakikisha Sheria za Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na ya Takwimu 2016 zinawawezesha na kuwalinda waandishi wa habari pamoja na watoa taarifa kufichua maovu sambamba na takwimu za mambo yanayoiathiri jamii.

Akizungumza katika mdahalo uliohusisha wakuu wa vyombo vya habari na baadhi ya wasimamizi wa sheria hizo, Januari 18, 2017 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Internews Tanzania, Wenceslaus Mushi amesema baadhi ya vifungu vya...

 

2 days ago

Mwananchi

Wanahabari wapinga sheria kortini

Mwanza. Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), kwa kushirikiana na Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, jana walifungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 wakidai vinakiuka Katiba na kuminya uhuru wa maoni.

 

3 days ago

Mwananchi

Wanaokiuka sheria Zanzibar waadhibiwe

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein hivi karibuni amekuwa akiwatahadharisha watu wa Zanzibar hasa vijana juu ya hatari na athari za kutoheshimu sheria. Wakati akiwa Pemba alikutana na wananchi kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi na kuwaonya wanaovunja sheria kwamba mwisho wa siku watajikuta wamejiingiza katika matatizo.

 

3 days ago

Channelten

Waandishi wa Habari watahadharishwa Ni kuhusu kuzielewa sheria mpya zilizopitishwa

Uhuru habari

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuzifahamu sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 ili kujiepusha na mgogoro wa sheria pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kuuhabarisha umma.

Sheria ambazo ambazo zimeshasainiwa na Rais Baada ya kupitishwa na Bunge, kwa baadhi ya watu zimeonekana kama zitaminya uhuru wa vyombo vya habari, lakini baadhi ya wanasheria wamezielezea kuwa zimebainisha mambo ya msingi ambayo mwandishi wa habari anatakiwa kuyatekeleza...

 

3 days ago

Mtanzania

KESI NYINGINE YA KUPINGA SHERIA MPYA YA HABARI YAFUNGULIWA MWANZA

Karsan

Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan

Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na Kampuni ya Hali Halisi Publishers leo wamefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza wakidai ufafanuzi wa Mahakama juu ya sheria mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kukiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18.

Mlalamikaji mkuu katika kesi hiyo ni UTPC akishirikiana na Hali Halisi Publishers ambapo tayari kesi hiyo imekwishafunguliwa na...

 

3 days ago

Zanzibar 24

Serikali ipo tayari kubadilisha sheria zinazobana tasnia ya Habari

Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na wadau katika sekta ya habari kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ambazo zinaonekana kubana na kukandamiza tasnia hiyo kwa kwendana na mabadiliko ya wakati na teknolojia.

 

Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa kauli yake wakati wa ziara yake aliyoifanya katika vyombo vya habari vya IPP yenye lengo la kuangalia changamoto ambayo sekta hii ambayo inakabiliana nazo. Waziri huyo amesema wakati umefika...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani