8 months ago

Zanzibar 24

Mtoto auawa kwa kuchapwa fimbo na Baba yake kisa kugoma kwenda shule

Jeshi la Polisi katika Wilaya ya Pader, nchini Uganda, linamshikilia Bwana Omony Odokonyero (30) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanae mwenye umri wa miaka saba kilichotokana na kuchapwa  fimbo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor limeripoti Juni 7 2018, katika kijiji cha Omakigira, ambapo mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Richard Odokonyero, mwanafunzi wa shule ya msingi Pader Ogom alipigwa na fimbo baada ya kukataa kwenda shule akitaka kupelekwa kwa bibi yake.

Mwenyekiti wa Kijiji...

 

8 months ago

Malunde

BABA AUA MTOTO KISA KAGOMA KWENDA SHULE

Polisi katika wilaya ya Pader nchini Uganda wamemkamata mwanaume mwenye miaka 30 baada ya kumpiga mtoto wake wa miaka 7 kwa fimbo mpaka kufa kisa tu mtoto huyo amekataa kwenda shule.
Richard odokonyero mwenye miaka 7 alikuwa akisoma katika shule ya msingi Pader kabla ya uhai wake kukatishwa na baba yake Denis Omony Juni 6,2018.
Mwenyekiti wa eneo hilo Charles Otto Lalobo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa baba huyo aligeuka hayawani na kumshambulia mwanae kwa fimbo kichwani...

 

8 months ago

VOASwahili

Wazazi wawaondoa watoto shule ya Moi

Wazazi mjini Nairobi walivamia shule ya bweni Jumatatu na kuwachukuwa watoto wao, wakiutuhumu uongozi wa shule ya wasichana ya Moi Nairobi kwa kushindwa kuwalinda watoto wao.

 

8 months ago

Michuzi

UONGOZI SHULE YA ST FLORENCE WAMZUNGUMZIA MWALIMU ANAYETUHUMIWA KWA KUDHALILISHA WANAFUNZI WA KIKE

Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii
UONGOZI wa Shule ya St Florence Academy ya jijini Dar es Salaam umesema umesikitishwa na habari za mmoja wa walimu wake kutuhumiwa kuwadhalilisha wanafunzi wa kike kijinsia huku ikifafanua kuwa umejipanga kuongeza CCTV Camera katika sehemu mbalimbali za shule ili kuimarisha usalama
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Shule hiyo, Flora Damas Assey amesema kuwa wao kama uongozi, wazazi na walezi wamesikitishwa mno na...

 

8 months ago

Malunde

MWALIMU ABAKA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BWENINI..ARUKA UKUTA

Jeshi la Polisi katika eneo la Laikipia nchini Kenya, linamtafuta mwalimu wa kiume ambaye anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi Slopes View Academy.
Kwa mujibu wa Citizen Kenya imeripoti leo Juni 4, 2018 kwamba tukio hilo limetokea asubuhi ya Juni 2 ambapo mwalimu wa zamu alikutana na msichna huyo alipokuwa anaenda darasani kujisomea na ndipo alimuamuru kurudi bwenini huku akimfuata na kisha kumbaka
Mtuhumiwa wa ubakaji ambaye ni mwalimu aliruka ukuta wa shule...

 

8 months ago

BBCSwahili

Shule ya Moi Girls yafungwa Kenya baada ya tuhuma za kubakwa wasichana shuleni.

Masuali mengi yanaulizwa kuhusu ni vipi wasichana wa Moi Girls Kenya wamebakwa ndani ya shule na mtu asiyejulikana Jumamosi usiku.

 

8 months ago

Malunde

SHULE YAFUNGWA BAADA YA WANAFUNZI KUBAKWA

Shule ya sekondari ya Wasichana ya Moi nchini Kenya imefungwa kwa dharula kwa muda wa wiki moja, baada ya kuwepo kwa tuhuma za vitendo vya ubakaji.
Katibu wa Tume ya Elimu Amina Mohamedi ametoa agizo la kufungwa kwa shule hiyo Juni 3,2018 baada ya kufanya kikao na uongozi wa shule hiyo, ambayo imekutwa na tukio la ubakaji.
Katibu huyo amesema kwamba serikali inajipanga kuweka ulinzi shuleni hapo, huku ikijiandaa kufanya hivyo kwa shule zingine ili kuzuia vitendo kama hivyo visijitokeze...

 

8 months ago

Malunde

MOTO WATEKETEZA MITIHANI NA VYETI VYA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI KAZIMA TABORA


Picha haihusiani na tukio halisi
Jengo la utawala la shule ya sekondari Kazima katika Manispaa ya Tabora limeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyaraka mbalimbali ikiwemo mitihani ya kujipima, ya kidato cha nne na cha tano.

Akizungumza na wanahabari Mkuu wa shule hiyo Mrisho Kivuruga, amesema jengo hilo limeanza kuungua na moto majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo.
Kivuruga amesema moto huo umeteketeza nyaraka zote muhimu za shule hiyo ikiwemo vyeti vya wanafunzi, mitihani...

 

8 months ago

Michuzi

DC SHINYANGA AKABIDHI MSAADA WA BIMA ZA AFYA, SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 200 TAMASHA LA TVMC

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro leo Ijumaa Juni 1,2018 amekabidhi msaada wa nguo za shule na kadi za bima ya afya kwa wanafunzi 200 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata za Chamaguha,Ibadakuli,Kizumbi, Mwawaza na Mwamalili zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.Msaada huo umetolewa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi...

 

8 months ago

Malunde

Picha : DC SHINYANGA AKABIDHI MSAADA WA BIMA ZA AFYA, SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 200 TAMASHA LA TVMC

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro leo Ijumaa Juni 1,2018 amekabidhi msaada wa nguo za shule na kadi za bima ya afya kwa wanafunzi 200 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata za Chamaguha,Ibadakuli,Kizumbi, Mwawaza na Mwamalili zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.
Msaada huo umetolewa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi...

 

8 months ago

Michuzi

TAARIFA KWA UMMA: uteuzi wa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bara mwaka 2018 kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limefanya uteuzi wa wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bara kwa mwaka 2018, kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.Sanjari na uteuzi huo, JKT limewapangia Makambi ya JKT watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01-10 June 2018. Wahitimu hao, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT...

 

8 months ago

Malunde

DC JENERALI GAGUTI AWAPONGEZA WANANCHI KUJITOLEA KUJENGA SHULE KUNUSURU WANAFUNZI 600

Zaidi ya wanafunzi 600 wa darasa la tatu katika shule ya Msingi Kumkambati kata ya Nyamidaho wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wanalazimika kusoma katika chumba kimoja kutokana na uhaba wa madarasa na wingi wa wanafunzi hali iliyowalazimu wazazi kuanzisha ujenzi wa shule nyingine katika vijiji jirani vya Kumtundu na Mkuyuni.
Hayo yalibainika jana wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akitembelea miradi ya wilaya hiyo iliyoanzishwa na wananchi na...

 

8 months ago

Michuzi

RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameuagiza uongozi wa wilaya ya Gairo na mkoa wetu kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wa shule msingi mpaka sekondani wanapatiwa chakula mashuleni. Kauli hiyo ameitoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika Ufunguzi wa madarasa ya shule ya sekondari Chagongwe katika ziara yake kwa siku ya tatu Wilayani Gairo kukagua miradi ya maendeleo.
 Ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Gairo kujiwekea mpango...

 

8 months ago

Malunde

RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua majengo ya shule ya Chagongwe wakati wa ziaya yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kushoto) wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kumaliza ufunguzi wa majengo ya shule ya sekondari Chagongwe.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani