2 days ago

MillardAyo

Haji Manara amewasikia wanaoibeza Simba kutoka sare ya 2-2 vs Mwadui FC

Baada ya wekundu wa msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu jana dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na kutoka sare ya kufungama magoli 2-2 maneno yamekuwa mengi na watu wameanza kukosoa kuwa Simba imepunguza kasi ya Ubingwa. Kupitia ukurasa wake wa instagrama afisa habari wa Simba Haji Manara ameamua […]

 

3 days ago

MillardAyo

Simba imewapa matumaini Yanga, Azam FC na Singida kwamba Ubingwa upo wazi

Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo kwa wekundu wa Msimbazi Simba kuwa wageni wa Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Simba waliingia Kambarage kucheza mchezo wao wa 18 wa Ligi Kuu. Simba imekuwa ikipata tabu kupata matokeo ya ushindi kwa baadhi ya game katika uwanja wa CCM Kambarage dhidi ya Mwadui FC […]

 

6 days ago

Malunde

JANGILI AUAWA KWA KULIWA NA SIMBA AKIWINDA WANYAMA

Moja ya habari kubwa wiki hii ni kuhusu mtu mmoja anayedhaniwa kuwa jangili katika hifadhi ya simba karibu na Mbuga ya Wanyama ya Kruger amevamiwa na kuliwa na kikundi cha simba akiwa katika shughuli zake hizo za uwindaji nchini Afrika Kusini.
Polisi katika eneo hilo wameeleza kuwa mtu huyo ameraruriwa vibaya na vipande vichache tu vya mwili wake ndiyo vimepatikana ikiwa ni pamoja na mabaki ya kichwa.
Wameeleza kuwa mpaka sasa haijajulikana mtu huyo ni nani lakini uchunguzi unaendelea. 
Hata...

 

1 week ago

Michuzi

MSHAMBULIAJI wa Simba John Bocco ndiye mchezaji bora wa LIGI KUU mwezi Januari

MSHAMBULIAJI wa Simba ya Dar es Salaam John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba na Awesu Awesu wa Mwadui kutokana na uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana wiki hii kupitia ripoti za makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo...

 

1 week ago

Michuzi

Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe.

Na Agness Francis Globu ya jamii 
VINARA  wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sc  wanaendelea kujifua vikali kukabiliana na mchezo wao  kimataifa dhidi ya Gendarmerie Nationale FC  ya nchini Djibouti katika kuwania Kombe la Shirikisho  la CAF.
Mtanange huo utakaorindima Februari 11 katika Dimba la Uwanja wa Taifa Jijini  Dar es  salaam Majira ya Saa 10:00 jioni . Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam katika Makao Makuu ya Timu ya    SimbaSc' Mnyama'  Msemaji  Mkuu wa Timu ya ...

 

2 weeks ago

Michuzi

AZAM FC, SIMBA SC VITANI KESHO UWANJA WA TAIFA

Na Agness Francis,  Globu ya jamii MABINGWA Afrika Mashariki na kati Azam FC watakuwa wageni dhidi ya vinara aa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sc katika mchezo wao wa 2 mzunguko wa 2.
Mchezo huo  utakaorindima kesho  katika  dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Mzizima jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema wapo vizuri katika kumkabili mnyama Simba na kuhakikisha wanaondoka ...

 

2 weeks ago

Michuzi

AZAM FC YAAHIDI KUTOWAANGUSHA MASHABIKI,WAPO KAMILI KUIVAA SIMBA

NAHODHA Msaidizi wa Azam FC,  Agrey Moris ameweka wazi kuwa hawatawaangusha mashabiki kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba.
Moris ametoa kauli hiyo ikiwa zimebaki  siku mbili kabla ya timu yao ua Azam FC kupambana na Simba.Mchezo huo utakafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ,keshokutwa saa 10 jioni.Ni mchezo unaotarajiwa kuwa mkali ya wa aina yake kutokana na Azam FC iliyojikusanyia pointi 33 kuwa kwenye vita kali ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo dhidi...

 

3 weeks ago

Michuzi

BALOZI SIMBA AKUTANA NA UGENI KUTOKA NCHINI MAREKANI

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia) akimkaribisha katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, Afisa wa Masuala ya Siasa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, Daniel Daley, kabla ya kuanza mazungumzo kwa ajili ya ugeni kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo. Katikati ni Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Rendi Mccoy aliyetembelea Wizara hiyo kwa ajili ya kuona Serikali ya Tanzania inavyotekeleza vita dhidi ya Biashara Haramu ya...

 

4 weeks ago

Michuzi

RAIS WA SIMBA FC ALAZWA MUHIMBILI

* Mahakama yaelezwa anasumbuliwa na Figo
MWENDESHA Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ,(Takukuru) , Leonard Swai ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa Hospital ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na Figo.
Aveva ambaye ni mshtakiwa wa kwanza shtakiwa mwingine katika kesi ya uhujumu uchumi anashtakiwa pamoja na Makamu rais wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' ambaye alikuwepo mahakamani hapo
Wakili Swai amedai...

 

4 weeks ago

Michuzi

SIMBA SC WAJINOA UWANJA WA BANDARI

 Kocha  mkuu wa Simba SC, Pierre  Lechantre  katikati na kushoto ni kocha Msaidizi  Masoud Djuma wakipeana maelekezo katika mazoezi  hayo kulia ni Meneja wa Simba SC, Robert Richard Uwanja wa Bandari Temeke Jijini Dar es Salaam. Wachezaji SimbaSc wakiwa kwenye mazoezi ya kujifua kukabiliana na mchezo wao wa raundi ya 16 dhidi ya Wanalizombe MajimajiFc utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili hii majira ya Saa 10 jioni.Mchezaji wa Simba SC, Shomari Kapombe...

 

4 weeks ago

Michuzi

SIMBA SC WAREJEA DAR KWA RAHA ZAO

Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC kimewasili leo jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Kagera kilikokuwa na mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar.
Mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Kaitaba ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Akizungumza na Michuzi Blog baada ya kuwasili leo,jijini Dar es Salaam katika uwanja kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kocha Msaidizi wa Simba Massoud Djuma amesema kuwa anawashukuru wachezaji wake kwa...

 

4 weeks ago

Malunde

NYOSSO AKAMATWA NA POLISI KWA KUMCHAPA MAKONDE SHABIKI WA SIMBA


Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limethibitisha kumshikilia mlinzi wa Kagera Sugar Juma Said Nyosso kwa kosa la kumpiga shabiki anayeaminika kuwa ni wa Simba baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa mjini Bukoba.
Tukio hilo limetokea baada ya mechi kumalizika na wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo na mashabiki wakawa wanashangilia kwa kutoa maneno makali kitendo ambacho kilimfanya Nyosso akose uvumilivu na kumpiga shabiki huyo.
Baada ya...

 

4 weeks ago

Michuzi

Serikali yatoa Msimamo wake kwa Klabu ya Simba kuhusu suala la uwekezaji

Na Anitha Jonas – WHUSM
Serikali imetoa msisitizo kwa Klabu ya Mchezo ya Simba kuzingatia sheria na kanuni zinayosimamia suala la uwekezaji kwa Klabu zilizoanzishwa na wanachama ambapo wanachama wanachukua 51% na mwekezaji anachukua 49%.
Msisitizo huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokutana na uongozi wa Klabu ya Simba na kuzungumza nao kufuatia kutoa asilimia 50% kwa mwekezaji wa klabu hiyo Bw.Mohamed Dewji...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani