(Today) 20 minutes ago

Mwanaspoti

USAJILI MPYA SIMBA NOMA

SIMBA sasa imetega macho yake katika tiketi mbili za mashindano ya kimataifa ambazo zipo mbele yao na ikitokea tu wakajihakikishia ushiriki wa mashindano hayo, watafanya usajili kabambe.

 

(Today) 21 minutes ago

Dewji Blog

Simba SC yaanza mchakato wa kuondoa nyasi bandarini

Baada ya kuwepo kwa taarifa ambayo inaelezea kuwa kampuni ya Majembe Auction Mart itapiga mnada nyasi bandia za Simba SC ambazo zipo bandarini, uongozi wa klabu ya Simba umejitokeza na kuzungumza kuhusu hatua ambayo wamefikia za kuondoa nyasi hizo.

Akizungumza na kituo cha redio cha E Fm, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu amekeri nyasi hizo kukaa bandarini kwa muda mrefu na baada ya serikali kukataa ombi lao la kupata msamaha wa kodi tayari wameshaanza taratibu za kulipa kodi...

 

(Today) 9 hours ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS WA KLABU YA SIMBA, GEOFREY NYANGE KABURU AZINDUA TAWI LA SIMBA LA KICHWABUTA LEO BUKOBA


Picha na habari na Faustine RuttaMakamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu(wa pili) kutoka kushoto akiwa na  Viongozi wa Tawi la Kichwabuta lililozinduliwa jana kwa shangwe na nderemo mjini Bukoba. Tawi hilo limepewa Jina la Kichwabuta kutokana na kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama mpenzi na Mwanachama wa Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba. Tawi hilo mpaka sasa lina Wanachama 160...

 

2 days ago

Mwanaspoti

Maniche awajaza upepo Simba

KIUNGO wa zamani wa Simba, Awadhi Juma ‘Maniche’ ambaye kwa sasa anaitumikia Mwadui FC, amewapa mbinu Simba kwamba wakiifunga Kagera Sugar, watakuwa wana ujasiri wa safari ya ubingwa msimu huu.

 

2 days ago

Mwanaspoti

Simba wamalizana na wachezaji

MABOSI wa Simba wametazama idadi kubwa ya nyota wanaomaliza mikataba katika kikosi cha watani zao Yanga na kubaini kuwa wana nafasi ya kuipiga bao timu hiyo mapema na kujitengeneza ufalme.

 

3 days ago

Channelten

Asaa Simba akubali adhabu CCM, Aahidi kutoihama CCM, haki imetendeka

Screen Shot 2017-03-27 at 11.39.33 AM

Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Ilala Asaa Simba Haroun amesema ameipokea bila kinyongo adhabu aliyopewa na chama chake huku akiamini kuwa haki imetendeka kwani lengo kuu lilikuwa ni kukijenga na kukiimarisha chama hicho.

Adhabu aliyopewa ni kuondolewa katika nafasi ya uongozi na kuwekwa chini ya uangalizi katika kipindi cha miezi 30.

Ameyasema hayo jijini dar es salaam na kuwapongeza wajumbe wa kikao kilichofanya maamuzi chini ya mwenyekiti wake Rais John Magufuli...

 

3 days ago

Mwanaspoti

Okwi atamka mambo mazuri Simba

UNALIKUMBUKA lile pambano la watani la Oktoba Mosi, mwaka jana lilivyoleta kizaazaa kwa mashabiki wa Simba kung’oa viti na kuiponza timu yao kulazimika kukarabati viti zaidi ya 1700? Kisa si bao la mkono la Amissi Tambwe wa Yanga.

 

3 days ago

Mwanaspoti

Simba yaitia aibu Yanga Dar

KITENDO cha Yanga kusajili wachezaji wa gharama kubwa kutoka nje ya nchi kimewaponza kwani katika kikosi cha Taifa Stars sasa kuna mchezaji mmoja tu anayeanza kati ya wachezaji wanne walioitwa.

 

5 days ago

Bongo5

Mo Dewji kuificha Simba mikononi mwa Juventus ya Italia

Mohammed Dewji amepanga kuiunganisha Simba kwa Juventus ya Italia.

Tajiri huyo namba moja kwa sasa hapa nchini alitua Italia katika klabu hiyo mapema wiki hii na kufanya nao mazungumzo juu ya kuinua soka la Tanzania. Akiongea na mtandao wa Salehjembe, Dewji amesema, “Wiki hii nilifanya kikao na Juventus FC. Wanayo nia ya kuendeleza soka kwa vijana wa Tanzania. Ninatazamia kuitambulisha timu hiyo ya Italia kwa uongozi wa Simba SC ili waanze majadiliano ya jambo hilo.”

Juventus imekuwa...

 

6 days ago

Bongo5

Mwamuzi Jacob Adongo aliye chezesha mechi ya Simba na Mbeya City amepewa onyo kali na TFF

Mwamuzi Jacob Adongo amepewa onyo kali kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria katika mechi namba 186 kati ya Simba na Mbeya City iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Onyo hilo limetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Kadhalika katika mchezo huo namba 186 (Simba 2 vs Mbeya City 2). Klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa timu yake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(14)...

 

6 days ago

Mwanaspoti

Simba Mkude, Yanga Nadir

MTIKISIKO mkubwa umewakumba manahodha wa vigogo wa soka nchini Simba na Yanga baada ya nafasi zao katika vikosi vya kwanza kujaa utata.

 

6 days ago

Mwanaspoti

Simba yamuomba Mghana Azam

APRILI Mosi ni siku ya Wajinga Duniani. Yanga na Azam zitacheza siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa. Straika wa Azam, John Bocco ‘Adebayor’ hatakuwepo kwenye mchezo huo kwavile ni majeruhi lakini Simba, wamemuomba Mghana Yahya Mohammed awaokoe kwa kuituliza Yanga.

 

7 days ago

Mwananchi

Mapato ya Madini, Simba yang'oa kigogo Arusha

Meneja wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Jackson Jolwa amesimamishwa kazi na wammiliki wa uwanja huo kwa madai alikuwa hafanyi ipasavyo majukumu yake.

 

1 week ago

Mwananchi

Simba yaendeleza vipigo Kaskazini

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wameendeleza ubabe dhidi ya timu za Kanda ya Kaskazini baada ya kushinda  mechi ya kirafiki katika mji mdogo wa Mererani iliyolenga kuhamasisha soka katika wilaya hiyo ya Simanjiro.

 

1 week ago

Habarileo

Simba yavunja rekodi

MCHEZO wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali ulizozikutanisha timu ya Madini na Simba katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, umevunja rekodi baada ya kukusanya Sh 81,427,000.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani