1 week ago

Michuzi

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAOMBA KIKUNDI CHA ULINZI CHA KIJESHI KUIMARISHA ULINZI, KUWEZESHA UFUGAJI WA SAMAKI ZIWA VICTORIA

Na Stella Kalinga, Simiyu
Serikali mkoani Simiyu imeomba kuwepo kwa kikundi cha ulinzi cha kijeshi katika Wilaya ya Busega ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo uvuvi haramu na kuwezesha ufugaji wa samaki ndani ya Ziwa Victoria kufanyika kwa usalama.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati wa Hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo iliyoandaliwa na ndugu zake kijijini kwao Yitimwila ‘A’ katika Kata...

 

3 weeks ago

Michuzi

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAZIDI KUIVA UWANJA WA UHURU,PIA KUFANYIKA MIKOA YA MWANZA NA SIMIYUMkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kinondoni,jijini Dar es salaam kuhusiana na  maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 16 kwenye uwanja wa Uhuru na kutumbuizwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa mbalimbali na nchini Tanzania.

Msama amesema mwimbaji nguli kutoka nchini Afrika ya Kusini Solly Mahlangu atakuwa ni mmojawapo wa waimbaji kutoka nje ya nchi wakiwemo wengine kutoka...

 

4 weeks ago

Michuzi

RC Simiyu amaliza mgogoro wa wanakijiji na wawekezaji

 MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya mwekezaji katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao iliyopo wilayani Meatu, na baadhi ya vijiji vinavyounda jumuiya hiyo. 
Mwekezaji huyo Mwiba Holdings, amekuwa na mgogoro wa mipaka, mkataba wa kumiliki ardhi na uanzishaji wa ranchi na baadhi ya vijiji hivyo kiasi cha kusababisha kuwa na mahusiano mabaya na wananchi ambao wamekuwa wakisusia misaada mbalimbali inayotolewa na mwekezaji...

 

1 month ago

Malunde

Picha: MKUTANO WA WADAU WA MKONGE WILAYA YA KISHAPU - SHINYANGA NA MEATU - SIMIYU


Alhamis ,Machi 16,2017 kumefanyika Mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu na wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.Mgeni rasmi katika mkutano huo ulioandaliwa na shirika la OXFAM na asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na Maendeleo ya Jamii (Relief to Development Society- REDESO) alikuwa mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Mratibu Miradi (uchumi) kutoka shirika la OXFAM Haji Kihwele alisema...

 

2 months ago

Global Publishers

FFU Watumia Nguvu Kutuliza Ghasia Simiyu

Askari wa kutuliza Ghasia FFU akimfukuza mwanafunzi

WANAFUNZI takribani 600 wa Shule ya Sekondari ya Bariadi iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga Barabara Kuu ya Bariadi- Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Dues Toga.

Askari wanne wa kutuliza Ghasia wakimdhibiti mwanafunzi

Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri, lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia...

 

2 months ago

Channelten

Mradi wa upimaji na tiba, kupima wakazi laki tatu mkoani Simiyu

Mradi wa upimaji na tiba ya virusi vya ukimwi unatarajiwa kutoa ushauri nasaha na kupima ,jumla ya wakazi laki tatu Mkoani Simiyu sambamba na utoaji wa matibabu ya watoto wadogo elfu 20 ikiwa ni moja ya mkakati wa kupunguza kasi ya maaambukizi ya asilimia 3.1 kimkoa.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ,Paroko wa Parokia ya Bariadi Padre Kizito nyanga Victor wakati akitoa Taarifa ya Mradi unaotekelezwa na shirika lisilo la...

 

2 months ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA SIMIYU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka aliyemtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake leo.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es salaam.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu...

 

2 months ago

Michuzi

Friedkin Conservation Fund yachangia Saruji mifuko 3000 na Mabati 1000 Simiyu

Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia) shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 ikiwa ni msaada. Wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika tukio hilo Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF),...

 

2 months ago

Habarileo

Simiyu yapata msukumo mkubwa kuendesha Jukwaa la Biashara

MBUNGE wa Itilima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga amesifu kuwapo kwa jukwaa la biashara la mkoa huo ambalo watendaji muhimu wa taasisi mbalimbali za kifedha na mamlaka ya mapato walikuwapo kuangalia fursa mbalimbali.

 

2 months ago

Michuzi

JUKWAA LA BIASHARA MKOANI SIMIYU

Na Mroki Mroki, TSN Digital-Simiyu .Ni ile siku iliyosubiriwa ya kuumulika kibiashara mkoa wa Simiyu ulioanzishwa mwaka 2012, ambao umejipambanua kuwa ‘mkoa  darasa’, mintarafu suala zima la ujenzi wa viwanda nchini.


Mwezi uliopita, Rais John Magufuli alipotembelea mkoa huu, alipongeza juhudi zinazochukuliwa na mkoa huu chini ya mkuu wake, Anthony Mtaka, katika kujenga uchumi wa viwanda na hivyo kuelekea kuifanya ndoto yake ya Tanzania ya viwanda kutimia.


Kupitia Kampuni ya Magazeti ya...

 

2 months ago

Habarileo

Simiyu tayari kujenga kiwanda cha bidhaa za afya

MKOA wa Simiyu umedhamiria mwaka huu kuanza kujenga kiwanda cha aina yake Afrika Mashariki cha kutengeneza bidhaa za afya zinazotokana na pamba baada ya hatua za upembuzi yakinifu kuelekea kukamilika na michoro ya ramani ya kiwanda kuthibitishwa.

 

2 months ago

Michuzi

VIONGOZI WA TAASISI ZA UMMA SIMIYU WAHIMIZWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS

Na Stella Kalinga Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini ametoa wito kwa viongozi na Wakuu wa Taasisi za Umma mkoani humo,  kusimamia utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ya viungo Jumamosi ya pili ya kila mwezi. Sagini ametoa wito huo leo katika hotuba yake kwa watumishi wa umma,wanafunzi na wananchi walioshiriki mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali katika uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi ikiwa...

 

2 months ago

Michuzi

MHANDISI WA UJENZI MKOA WA SIMIYU ASIMAMISHWA KAZI


Na Stella Kalinga
Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka matatu.
Akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi huyo anashtakiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewa kwa kiwango cha kuridhisha.
Amesema akiwa mtumishi wa umma kinyume na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya jedwali la kwanza la kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali...

 

3 months ago

Channelten

Mkoa wa Simiyu umetajwa kushika nafasi ya 64 katika uzalishaji wa zao la Pamba duniani

Mkoa wa Simiyu umetajwa kushika nafasi ya 64 katika uzalishaji wa zao la Pamba duniani ,ambapo hapa nchini unaongoza kwa kuzalisha kwa asilimia 50 ili kuweza kuwa Miongoni Mwa Mataifa 10 Bora ,Kilimo Kinapaswa kifumuliwe kiwe cha Kisasa pia Wakulima wahamasishwe kutilia mkazo kwenye pamba ya organiki ili kuongeza Mnyoyoro wa thamani wa zao hilo hasa katika Soko la dunia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kuwasilisha Mwongozo wa uwekezaji Mkoani Simiyu katika kikao...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani