5 days ago

Michuzi

Twanga Pepeta waipania Tanga hatari

WAKALI wa muziki wa dansi nchini Tanzania, The African Stars Band, Twanga Pepeta 'Wazee wa Kisigino', wameipania vilivyo ziara yao ya Mkoa wa Tanga, wakisema wanakwenda kuonyesha makali yao halisi kwa mashabiki wao wa muziki, kwa kuanzia na onyesho la Ijumaa Machi 23, katika Ukumbi wa Tanga Hotel, jijini Tanga kwa kiingilio kidogo tu cha Sh 7,000.
Twanga wanapanda jukwaani ikiwa ni miezi kadhaa tangu walivyoenda katika Mkoa wa Tanga, maarufu kwa Wagosi wa Kaya, jambo linaloongeza mguso kwenye...

 

7 days ago

Michuzi

Balozi wa Kuwait azuru Shule ya Sekondari ya Old Tanga

Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem amezindua kituo cha kompyuta katika Shule ya Sekondari ya Old Tanga ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi huo unaofahamika kwa jila la “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”. kituo hiki ni cha pili kuzinduliwa nchini na Ubalozi huo kufuatia kile cha awali kilichozinduliwa mwaka jana katika Taasisi ya Taaluma Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Kituo cha Kompyuta katika Shule ya Old Tanga kimeunganishwa na huduma ya mtandao ili...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Tangazo la wito wa usaili ofisi ya msajili wa hakimiliki

Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia vijana ambao wameomba nafasi za kazi kwa Ofisi ya Msajili wa Hakimiliki kufika katika usaili siku ya Jumapili tarehe 11 Machi, 2017 katika Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) Tunguu saa 2:00 asubuhi.

Wasailiwa wote wanatakiwa kuchukua vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi.

 

Tangazo la wito wa usaili ofisi ya makamo wa pili wa rais

WASAILIWA WENYEWE NI:

WAHUDUMU
NO JINA KAMILI
1 AMINA AHMED...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Tangazo la wito wa usaili ofisi ya makamo wa pili wa rais

Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia vijana ambao wameomba nafasi za kazi kwa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi kufika katika usaili siku ya Jumapili tarehe 11 Machi, 2017 katika Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) Tunguu saa 2:00 asubuhi.

Wasailiwa wote wanatakiwa kuchukua vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi.

WASAILIWA WENYEWE NI:

KATIBU MUHTASI
NO JINA KAMILI
1 ABDALLAH SEIF ABDULLA
2 AMINA ABDULLA RASHID
3 GHANIMA KHATIB...

 

2 weeks ago

Michuzi

SERIKALI YATENGA BILIONI TATU UJENZI WA BARABARA YA MUHEZA-AMANNI MKOAN TANGA

Na Mwandishi Wetu, Tanga
SERIKALI imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 39 kutoka mjini Muheza hadi Amani wilayani humo, kwa kiwango cha lami. 
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoani Tanga, Mhandisi Alfred Ndumbalo alisema fedha hizo zimetengwa kama utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa mwaka jana kwamba barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami. 
Ndumbalo alisema nia ya serikali...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Habari Picha: Moto ulivyo teketeza bweni la korogwe Girls Tanga

MOTO umeteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe iliyoko mkoani Tanga na kuwaacha wanafunzi hao katika hali mbaya kufuatia mshtuko wa kupoteza vifaa vyao vyote.

Moto huo ulitokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo wakati wanafunzi takribani 40 wanaoishi katika bweni hilo wakiwa darasani wakijisomea.

Hata hivyo licha ya moto huo kutekeza bweni, hakuna madhara ya kimwili kwa upande wa wanafunzi hao isipokuwa kwa wale waliopata mshituko na kuzimia ambao wamelazwa...

 

3 weeks ago

Michuzi

SERIKALI YABAINI UJENZI WA NYUMBA KATIKATI YA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA HOROHORO TANGA

Na Munir Shemweta, Mkinga Tanga
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini uwepo ya nyumba za watanzania zilizojengwa katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya huku eneo moja la nyumba hizo likiwa upande wa Kenya.
Katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro mkoa wa Tanga mhe Mabula alijionea jinsi nyumba zilivyojengwa bila utaratibu wa kuacha umbali wa mita mia kama eneo huru.
Eneo lililoathirika zaidi na ujenzi huo, ni katika...

 

3 weeks ago

Malunde

MAGARI 13 KUSHIRIKI MBIO ZA MAGARI "MKWABI TANGA RALLY 2018" MKOANI TANGA


Mratibu wa Mashindano ya Magari  Tanzania,Faheem Ao akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na  Mashindano hayo wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mbio za Magari Mkoani Tanga Akida MachaiMwenyekiti wa Chama cha Mbio za Magari Mkoani Tanga Akida Machai kulia akizungumza kuhusiana na mashindano hayo  Meneja wa Mkwabi Super Market ambao ndiyo wadhamini wa Mashindano hayo,Lawi Sozigwa 
***ZAIDI ya magari 12 yanatarajiwa  kushiriki kwenye michuano ya Mbio za Magari ya Mkwabi Tanga Rally...

 

3 weeks ago

Malunde

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 35 KIWANDA CHA NYUZI CHA PPTL TANGA KWA UKIUKWAJI WA SHERIA

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amekitoza faini ya shilingi milioni 35 (milioni thelathini na tano), kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko eneo la Kange MkoaniKilimanjaro.
Mhe.Mavunde alichukua uamuzi huo, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo Machi 2, 2018 ili kubaini waajiri ambao hawatekeelzi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa...

 

3 weeks ago

Michuzi

MAVUNDE AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 35 KIWANDA CHA NYUZI CHA PPTL KILICHOKO MKOANI TANGA KWA UKIUKWAJI WA SHERIA

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amekitoza faini ya shilinhgi milioni 35 (milioni thelathini na tano), kiwanda cha kusokota nyuzi cha PPTL kilichoko eneo la Kange Mkoani Kilimanjaro.

Mhe. Mavunde alichukua uamuzi huo, wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo Machi 2, 2018 ili kubaini waajiri ambao hawatekeelzi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia...

 

3 weeks ago

Michuzi

Mkazi wa Lindi akabidhiwa Kirikuu yake aliyojishindia katika kampeni ya Malengo ya Benki ya NBC mjini Tanga leo

 Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi funguo ya gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ kwa mkazi wa Lindi,  Saidi Chiwina baada ya kuibuka mmoja wa washindi sita wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo katika hafla iliyofanyika mjini Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja tawini hapo, Mwanahawa Jangwa. Meneja wa Tawi la benki ya NBC Tanga,Asia Chambega (katikati) akimkabidhi kadi ya gari ya gari aina ya Suzuki Carry...

 

4 weeks ago

Michuzi

DK. KIGWANGALLA AAGIZA MBINU MPYA ITUMIKE KUDHIBITI WANAOCHIMBA MADINI KWENYE CHANZO CHA MAJI YA MTO ZIGI JIJINI TANGA


Na Hamza Temba, WMU, Muheza Tanga..........................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.


Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kutembelea eneo...

 

4 weeks ago

Michuzi

DALALI ATAKA TAWI LA SIMBA CREAM TANGA KUANZISHA TIMU YA VIJANA U-17

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Simba, Hassani Dalali amelitaka tawi la Simba Cream la Jijini Tanga kuanzisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ili iweze kuwa hazina kubwa ya wachezaji kwa siku za mbeleni.
Licha ya hivyo lakini pia inasaidia kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga ambao wanaweza kuonekana thamani yao siku zinazokuja kwani mkoa wa Tanga una vipaji vya soka vingi.
Dalali aliyesema hayo juzi akizungumza na wanachama wa Simba ikiwemo kuhimiza umoja na mshikamano ili kuiwezesha...

 

4 weeks ago

Zanzibar 24

Hatua iliyo fika SMZ tatizo la usafiri Pemba kwenda Tanga

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inaendelea na jitihada za kulipatia Ufumbuzi tatizo la ukosefu wa Usafiri wa Uhakiki wa kutoka pemba kwenda Tanga ili wananchi waweze kunufaika na huduma ya usafiri.

Naibu waziri wa Wizara ya ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Muhammed Ahmada amesema serikali inatambua tatizo la ukosefu wa Usafiri na tayari inazungumza na kampuni ya Azam Marine kuharikisha matengenezo ya Meli ya Sea link2 ili iweze kutumika kwa usafiri wa Pemba kwenda Tanga.

Amesema...

 

4 weeks ago

Michuzi

IGP SIRRO AZUNGUMZA NA ASKARI WA MKOA WA TANGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro (kulia) akizungumza na kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana walipokutana katika eneo la Msata Bagamoyo wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Jeshi la Polisi. Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro akipokea salamu ya Kijeshi kutoka kwa Mkaguzi wa Polisi, Ali Masumbuko wakati alipowasili katika Kituo cha Polisi wilaya ya Handeni mkoani Tanga leo, akiwa...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani