4 months ago

Michuzi

Taswa FC yang'ara Media Day ya DSTV

Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imewafundisha soka timu ya MultiChoice Tanzania (DSTV) baada ya kushinda katika mchezo maalum wa ‘Media Day’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam.Taswa FC ilianza mchezo huo kwa ‘dharau’ na kujikuta ikipachikwa bao katika dakika ya tatu ya mchezo. Bao hilo liliwashtua timu hiyo ya waandishi wa habari na kusawazisha katika dakika 11 kupitia kwa Hare Temba baada ya pasi safi ya Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto...

 

6 months ago

Michuzi

Taswa SC kukipiga na Saleni FC ya Lugoba

Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC)  kesho  itacheza mechi maalum ya kirafiki dhidi ya timu ya Saleni FC  kwenye uwanja wa  Saleni, Lugoba.
Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10.00 jioni na imeandaliwa kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya timu hizo mbili.
Mwenyekiti wa Taswa SC Majuto Omary alisema kuwa  maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na timu ya waandishi itaondoka jijini saa 3.00 kuelekea Lugoba, Chalinze.
Majuto alisema kuwa wachezaji wote wa Taswa SC...

 

7 months ago

Michuzi

TASWA FC YAIADHIBU POLISI FC MABAO 5-0 UWANJA WA UHURU

  MSHAMBULIAJI wa Taswa Fc, Said Seif (kushoto) akiruka kumkwepa beki wa Polisi Fc, Andew Thomas, wakati wa mchezo wa kirafiki katika Maadhimisho ya 10 ya Mtandao wa Polisi yaliyoanza jana Nov 4 katika Uwanja wa Uhuru Dar esSalaam, yakitarajia kumalizika Nov 9 mwaka huu. Katika mchezo huo Taswa Fc ilishinda mabao 5-0. Picha na Muhidin Sufiani.

 DCP Mary Nzuki wa Jeshi la Polisi, akimkabidhi Ngao ya ushindi Nahodha wa Taswa Fc, Willbert Moland, baada ya Taswa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0...

 

8 months ago

Michuzi

Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa FC, Wilbert Molandi mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya 12 mfululizo. anayeshuhudia ni mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary. Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa Queens, Zuhura Abdinoor mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya...

 

9 months ago

Michuzi

TASWA kufanya uchaguzi Novemba 5, mwaka huu

KAMATI ya Utendaji ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), iliyokutana Dar es Salaam jana Septemba 7, 2017, imepanga Uchaguzi Mkuu wa chama hicho ufanyike Novemba 5, mwaka huu.

Uchaguzi huo utafanyika Dar es Salaam katika ukumbi ambao utatangazwa na tayari kamati imeaigiza sekreterieti ya TASWA, ifanye maandalizi kuhusu uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya usimamizi wa karibu.

Kikao kimekubaliana watakaoshiriki...

 

11 months ago

Michuzi

Taswa FC yachapwa mabao 3-2 na TPB bank FC

Timu ya soka ya TPB Bank FC imefanikiwa kulipiza kisasi kwa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC baada ya kuifunga kwa mabao 3-2 katika mchezo huo maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sheria (Law School)  uliopo maeneo ya kituo cha mabasi cha Mawasiliano jijini Dar es salaam.Katika mchezo wa kwanza, Taswa FC iliifunga TPB Bank FC kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja  huo huo.TPB Bank FC ilitumia  idadi pungufu ya wachezaji wa Taswa FC kufunga mabao...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani