1 week ago

VOASwahili

Tatizo la kujaa maji mjini Dar es Salaam

 

1 week ago

VOASwahili

2 weeks ago

Zanzibar 24

Zawa yataja mambo mawili yanayo pelekea tatizo la maji kwa wananchi

Zanzibar bado inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa huduma ya maji safi na salama katika Wilaya mbali mbali jambo ambalo linawapa usumbufu mkubwa wananchi wakati wanapohitaji huduma katika harakati zao.

Wakizungumza na Zanzibar24 kwa Nyakati tofauti Baadhi ya wananchi katika maeneo ya Amani ,Michenzani na Jambiani wamesema kwa kipindi kirefu kumekuwa na usumbufu wakati wanapohitaji huduma ya maji safi na salama bila kujua tatizo.

Wamesema wanachukua jitihada mbalimbali katika kutoa taarifa...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Dkt. Shein- Tatizo la uhaba wa dawa mwisho Julai, 2019

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuanzia mwezi Julai mwaka 2019, Zanzibar haitakuwa tena na tatizo la uhaba wa dawa kwa magonjwa yote yanayowakabilia wananchi wake.

Alisema hilo linawezekana, kutokana na uchumi wa Zanzibar kuimarika hatua kwa hatua, hivyo wananchi wa Zanzibar wataondokana na shida waliyonayo hivi sasa, kwa uhaba wa dawa uliopo kwenye vituo vya afya pamoja na hospitali kadhaa.

Dk. Shein alieleza hayo leo, huko katika uwanja...

 

2 weeks ago

Michuzi

TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema suala la maji Mkuranga ni tatizo la muda lakini sasa matumaini yameanza kuonekana baada ya  benki ya Dunia kuleta  mradi wa maji wa visima 29 utakaokuwa na thamani ya zaidi ya bilioni mbili.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanambaya, amesema kuwa mradi wa maji utakuwa historia kutokana na hatua zinazochukuliwa na serikali. Amesema katika ziara zake amekuwa akikutana na changamoto za maji lakini...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

ZURA yathibitisha tatizo la upungufu wa mafuta nchini

Mamlaka ya Udhibiti wa  huduma za Maji, nishati na Mafuta Zanzibar  ZURA  imesema upungufu wa mafuta ya Petroli uliojitokeza nchini katika vituo mbalimbali Zanzibar  unatokana na kuongezeka kwa mahitaji ya huduma hiyo  kwa wananchi.

Akizungumza na Zanzibar24 huko Ofisini kwake Maisara mjini unguja,  Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Mbaraka Hassan Haji amesema  kiwango cha mafuta  kilichotengwa kutumika kimekuwa kidogo  ukilinganisha na mahitaji ya wananchi hasa  katika kipindi hichi cha skukuu...

 

3 weeks ago

Michuzi

Hatuna tatizo la dawa nchi nzima-Dkt. Ndugulile

Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii

Serikali imesema kuwa hakuna tatizo la dawa katika sehemu kutoa huduma za afya katika Hospitali, Vituo vya Afya , Dispensari pamoja na Zahanati.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkanoge Kata ya Nyamato Wilayani Mkuranga.

Dk.Ndugulile amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya Wizara ya afya kumefanya Wizara kujipanga katika...

 

3 weeks ago

Michuzi

WANANCHI WAITAKA SERIKALI KUFANYIA KAZI TATIZO LA KUKATIKA UMEME KWENYE VITUO VYA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA- MTWARA


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeendelea na Usajili wananchi Vitambulisho vya Taifa mkoani Mtwara ambapo katika Wilaya ya Mtwara Idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza kushiriki zoezi hilo huku baadhi wakilalamikia kukaa muda mrefu kwenye vituo vya Usajili na baadhi ya mashine kutokufanya kazi.Bwana Athumani Salum mkazi wa Kata ya Magomeni amesema “zoezi kama zoezi ni zuri ila changamoto kubwa ni kukatika kwa umeme na hivyo kusababisha wananchi tusubiri muda mrefu kiasi cha...

 

1 month ago

Michuzi

SERIKALI GEITA YAJIPANGA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWA WANANCHI

Na Joel Maduka, GeitaSerikali mkoani Geita imejipanga kutatua kero ya maji kwa wananchi inayowakabili wananchi kwa muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ametoa kauli hiyo alipotembelea miradi ya uzalishaji wa maji inayosimamiwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jinni Geita, GEUWASA.
Alisema serikali imedhamiria kuona mji wa Geita unakuwa na maji ya kutosha ambapo kwa sasa kuna tanki lenye Mita za ujazo elfu moja na mia mbili na kwamba zipo jitihada za...

 

1 month ago

VOASwahili

Tatizo la maradhi ya mgongo wazi na ulemavu wa watoto

Wataalamu wa afya duniani wanakadiria kuwa kwa kila watoto elfu wanaozaliwa mmoja huzaliwa na tatizo la kichwa maji ama mgongo wazi.

 

1 month ago

Zanzibar 24

Ukosefu wa vifaaa kwa wakulima wa miche ya karafuu ni tatizo

Umoja wa Wakulima wa Miche ya Mikarafuu Donge Vijibweni Uwamido wameiyomba  Serikali  kuwasaidia  vifaa vitakavyowasaidia  katika kuikuza miche wanayoipanda.

Akizungumza na Zanzibar24 Katibu wa Uwamido Ameir Abasi Ameir amesema wamejikusanya pamoja katika kupanda  mikarafuu lakini wanakabiliwa na ukosefu wa vifaa  vinavyotumika katika uatikaji wa miche hiyo ikiwemo mabero,glove,ndoo na keni za kumwagilia maji.

Amesema kukosekana kwa vifaa hivyo  kunarejesha nyuma  jitihada zao ikizingatia ...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Tatizo la kukatika ovyo umeme Tanzania mwisho Desemba 15

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema hakuna mgawo wa umeme nchini na tatizo la kukatika kwa umeme linalojitokeza maeneo mengi hivi sasa kutokana na marekebisho ya mitambo chakavu  litamalizika Desemba 15, mwaka huu. Akizungumza katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na TBC1, Dk Kalemani alisema lengo la marekebisho yanayofanywa ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na mitambo itakayowezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika wakati wote. Alisema umeme una umuhimu katika...

 

2 months ago

BBCSwahili

Panya na mende ni tatizo Ikulu ya Whitehouse Marekani

Panya, Mende wadudu na viti vya vyoo vilivyovunjika ni miongoni mwa vitu vingi vilivyoripotiwa kwa wafanyikazi wa kurekebisha na wafanyikazi wa rais Donald Trump katika ikulu ya Whitehouse

 

2 months ago

Malunde

Imefichuka : WANAUME WENGI WANA TATIZO LA UZAZI....VIUNGO VYA UZAZI NAVYO BALAA


WAKATI kukiwa na dhana potofu kuwa baadhi ya wanaume wa Jiji la Dar es Salaam, ndio wanaopungukiwa zaidi na sifa za kuwa wanaume halisi kutokana na maisha wanayoishi, imebainika kuwa hivi sasa kuna kesi pia zinazothibitisha baadhi ya wanaume katika mikoa mbalimbali nchini, wanakabiliwa na matatizo ya uzazi.

Imebainika pia kuwa uhaba wa wataalamu wa tiba wa magonjwa ya uzazi kwa wanaume nchini, unaathiri kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa tiba sahihi ya magonjwa hayo ya uzazi yanayowakabili...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani