(Yesterday)

CCM Blog

MWENYEKITI WA MTAA WA BUNGONI, ILALA ATOA MABATI 150 KUSAIDIA UJENZI WA ZAHANATI ILALA

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bungoni Ilala, Barua Mwakilanga akikabidhi bati 150 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, leo jijini Dar es Salaam. Ametoa bati hizo kuitikia mwito ulitoalewa hizi karibuni na Waziri Mkuu majaliwa Kassim Majaliwa kumwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchangisha fedha kwa wadau ili kupatikana fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati Ilala.
"Asante sana" Sophia Mjema akimshukuru Barua wakati akipokea...

 

(Yesterday)

Michuzi

DED MNASI AKAGUA MIRADI YA UJENZI WA MADARASA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA ILEJE

Na Fredy Mgunda,Ileje 
HALMASHAURI ya wilaya ya Ileje mkoani songwe imetumia zaidi ya shilingi milioni mia moja themanini katika ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za EPFR ambazo hutolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukagua miradi hiyo,mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi alisema kuwa jukumu la uongozi ni kuhakikisha kuwa pesa inayotolewa na serikali inatumika kama ilivyokusudiwa na serikali kuu kwa faida ya...

 

1 day ago

Michuzi

UJENZI WA BARABARA YA NYAHUA-CHAYA KM 85.4 KWA KIWANGO CHA LAMI WAANZA RASMI

Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi wa kampuni ya CHICO kutoka China, ili kuweza kuufungua mkoa wa Tabora na mikoa jirani ya katavi na kigoma.
Amesema hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati aliposimamishwa na wakazi wa kijiji cha Tura, wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, alipokuwa akikagua kambi ya mkandarasi na kuangalia hatua za awali za matayarisho ya ujenzi wa barabara...

 

2 days ago

Michuzi

DCC LUSHOTO YASITISHA MPANGO WA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Lushoto (DCC) imeamua kusitisha mpango wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli lilokuwa lijengwe kwenye eneo jipya la Kwehangala hadi hapo suluhu ya mgogoro baina ya viongozi wa halmashauri hiyo itakapopatikana. 
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto January Lugangika (Pichani Juu) alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kuwepo sintofahamu kati ya Madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wengine juu ya suala hilo. .
Hivi...

 

2 days ago

CCM Blog

MBUNGE MGIMWA AMETOA BATI 590 NA MIFUKO YA SARUJI 220 KWA AJILI YA UJENZI NA UKARABATI WA MADARASA KATA YA IHALIMBA

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi  na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano...

 

2 days ago

Michuzi

PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka makandarasi wazawa wa kampuni ya Samota, Anam na Jossam JV wanaojenga barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliowekwa.
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo katika kijiji cha Motomoto, Wilaya ya Urambo mkoani Tabora alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mtandao wa barabara mkoani humo na kutoridhishwa na kasi ya...

 

3 days ago

Michuzi

MGIMWA ATOA BATI 590,MIFUKO YA SARUJI 220 UJENZI MADARASA KATA YA IHALIMBA

Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi. 
Akizungumza na walimu wa kata hiyo mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza...

 

5 days ago

Michuzi

KAIMU MKURUGENZI WA VIWANJA VYA NDEGE AIOMBA SERIKALI KUTOA KIPAUMBELE UJENZI WA UWANJA WA NDEGE SIMIYU

Na Stella Kalinga, SimiyuKaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA),  Richard Mayongela ameiomba serikali kutoa kiupaumbele cha ujenzi wa Viwanja vya Ndege kwa mikoa ya Simiyu na Lindi katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ili kuongeza fursa za uwekezaji na utalii. Mayongela ametoa ombi hilo katika kijiji cha IGEGU kata ya Sapiwi wilayani  BARIADI katika eneo linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na...

 

6 days ago

Michuzi

PROF. MBARAWA AAHIDI KUKAMILIKA KWA UJENZI WA DARAJA LA MTO MARA

Serikali imesema ujenzi wa daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 lililopo katika barabara ya Tarime-Mugumu-Nata litakamilika mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka huu.
Amezungumza hayo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua ujenzi wa daraja hilo ambalo linaunganisha wilaya ya Tarime na Serengeti na kuwatoa hofu wananchi wa wilaya hizo kuwa endapo daraja hilo likikamilika litaondosha adha waliyokuwa wanaipata ya kuvuka hasa vipindi vya...

 

7 days ago

Michuzi

MAHAKAMA YAANZA UJENZI WA MAHAKAMA TATU MKOANI GEITA

Na Lydia Churi-Geita.
Katika kutekeleza dhamira yake ya kuboresha huduma za Mahakama na kusogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi, Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imeanza rasmi ujenzi wa majengo matatu ya Mahakama katika mkoa wa Geita pamoja na wilaya zake za Bukombe na Chato.
Ujenzi wa Mahakama hizi ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015/16 hadi 2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao ulianza...

 

7 days ago

Michuzi

SERIKALI KULIPA FIDIA WANANCHI UJENZI WA BANDARI ZA ZIWA NYASA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi milioni 358 kwa ajili ya kulipa fidia nyumba na ardhi za wananchi waishio mwambao wa Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari za Ziwa hilo
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake aliyoifanya ya kukagua bandari za Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Manda iliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi...

 

1 week ago

Michuzi

WAZIRI KALEMANI ASHIRIKI MAKABIDHIANO YA SOKO LA SAMAKI, UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA, CHATO

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 14 Februari, 2018 ameshiriki makabidhiano ya Soko la Kimataifa la Samaki la Kasenda lililojengwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya Dola za Marekani 148,146. Aidha, Waziri Kalemani ameshiriki utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Japan na Tanzania kwa ajili ya ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita moja ya Muganza kwa gharama ya Dola za Marekani 90,645.Balozi wa Japan Nchini,...

 

1 week ago

Michuzi

KWANDIKWA AKAGUA MIRADI YA UJENZI MKOANI TANGA

Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa akizungumza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Mombo ikiwemo stendi ya Mombo jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen NgonyanNaibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (katikati) akiongozwa na Mbunge wa Korogwe Vijijini,...

 

1 week ago

Michuzi

KWANDKWA: SERIKALI KUIMARISHA SEKTA YA UJENZI NA UCHUKUZI MKOA WA TANGA

Na Ismail Ngayonga -MAELEZO 
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema Serikali imekusudia kuimarisha sekta ya ujenzi na uchukuzi katika Mkoa wa Tanga ikiwemo Ujenzi wa Daraja kubwa lenye urefu wa Mita 550 katika Wilaya ya Pangani, hatua inayolenga kufungua fursa na kuinua pato la kiuchumi kwa wanachi wa Mkoa huo. 
Akizungumza katika mkutano wake na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Sheghela jana Jumanne Februari 12, 2018, Naibu Waziri Kwandikwa aliyopo katika ziara ya...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani