2 days ago

Zanzibar 24

ZAECA yakamata watu watatu na madawa ya kulevya unguja

Mamlaka  ya kupambana na kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar Zaeca kitengo cha madawa ya kulevya kimewakamata watu watatu kwa tuhuma  ya  kukutwa na madawa ya kulevya katika maeneo tofauti.

Akizungumza na Zanzibar24  Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Mwanaidi Suleiman amesema  zaeca  kupitia kitengo hicho ilifanya msako maalumu na kufanikiwa  kuwakamata  watu hao  katika eneo la kianga, kwarara na kilimani Mjini unguja ambapo kesi hiyo  tayari imesha kamilika  uchunguzi wake na hatua...

 

4 days ago

Zanzibar 24

Kizee wa miaka 60 amlawiti mtoto wa miaka 8 Bwereu Unguja

Mzee mwenye umri wa miaka 60 amlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 8 huko Bwereu Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Baba mzazi wa mtoto huyo ameeleza kuwa “nikweli kuwa mwananangu jambo hili limemtokezea kwani tumesha mpeleka hospitali na madaktari wameshathibitisha kuwa amesha lawitiwa na anamichubuko ndani yake”

Kwahiyo mzazi huyo ameiomba Serikali pamoja na vyombo vya Sheria viweze kuchukua hatua kubwa ya kuvitokomeza vitendo hivyo.

Nae Sheha wa Shehia ya Bwereu Juma Nyange Omar amesema kuwa...

 

5 days ago

Zanzibar 24

Watatu watiwa mbaroni kwakukutwa na Dawa za kulevya Unguja

Jeshi là polisi Mkoa wa Kusini Unguja jana 12 February 2018 limewashikilia vijana watatu, wawili waakazi wa paje Mkoa wa Kusini Unguja na mmoja  mkaazi wa Kwarara Wilaya ya Mgharib B Unguja wakiwa na kete za Dawa za kulevya kwa nyakati tofauti. Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Kusini unguja Kamishna msaidizi Makarani Khamis Ahmed amesema kuwa mkaazi wa kwarara amekutwa akiwa na kete za dawa za kulevya 432 pamoja na vijana wawili waakazi paje wakiwa na kete...

 

5 days ago

Zanzibar 24

Habari Picha:Waandishi wakizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Unguja

Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Karym akiuliza maswali katika Mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheir kuhusiana na kuanzishwa Mabaraza ya Wadi na Kamati za Mashauriano za Shehia katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheir akifafanua jambo wakati akijibu maswali katika mkutano na...

 

6 days ago

Zanzibar 24

Watoto wafariki wakiwa wanaogelea katika Pwani ya Maruhubi Unguja

Watoto wawili wakaazi wa Muembe Makumbi wameripotiwa kufa maji wakati wakiogelea katika pwani ya Maruhubi wilaya ya mjini magharibi Unguja.

Akitoa taarifa hiyo kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi Unguja Hasan Nasir Ali amesema tukio hilo limetokea Februari 10 majira ya saa 7 mchana ambapo mtoto Juma miaka 14 na Ismail Abdalla miaka 11 wakaazi wa Muembe Makumbi wamefariki dunia wakiwa wanaogelea katika Pwani ya Maruhubi.

Jeshi la polisi na kikosi cha KMKM walifanikiwa kuipata miili ya...

 

6 days ago

Zanzibar 24

Vijana waendelea kusherehekea miaka 41 ya kuzaliwa chama cha CCM Unguja

Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Nyerere “A” Jimbo la Magomeni wameendelea na sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa Chama chao kwa kufanya Bonanza la Michezo mbalimbali Jimboni humo.

Bonanza hilo lilifanyika kwa lengo la kuimarisha afya na mashirikiano miongoni mwa Wanachama wa CCM na jamii kwa ujumla.

Akizungumza katika Bonanza hilo Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amesema ili kuweza kukienzi na kuendeleza matunda yaliyoachwa na waasisi wa chama hicho ni vyema...

 

6 days ago

Zanzibar 24

Atiwa mbaroni kwa kumpiga mapanga mtoto wa miezi mitano Kizimkazi Unguja

Mtoto mwenye umri wa miezi mitano acharazwa mapanga na babu yake wakambo anaefahamika kwajina la Ali Mwinyi Kondo anaekadiriwa kuwa anaumri wa miaka 45 mkaazi wa Kizimkazi Mkunguni na hatimae kukimbizwa Hospitali ya Makunduchi kwa matibabu.

Tukio hilo limetokea huko kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja.

Ambae ni Bibi wa Mtoto huyo amesema majira ya saa 5 usiku amegongewa mlango na kuletewa mtoto huyo akiwa na majeraha.”

“Alikuja Sheha Mstaafu kuniamsha na mumewangu usiku akanambia...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Upepo wasababisha hasara kubwa Koani Wilaya ya kati Unguja

Tukio hilo lakusikitisha limetokea huko kibonde maji Shehia ya Koani Wilaya ya kati kama anavyoeleza bi Asha Mahinda mwenye umri wa miaka 65 manusura wa ajali hiyo.

“Hali kwakweli sionzuri mda wa saa 7 kijana mmoja akaniita bibi toka humo ndani mti unaanguka ndipo nikatoka”

Miongoni mwa waliopata hasara katika upepo huo Juma Jaffar ameeleza hasara aliyoipata kuwa nyumba yake imeangukiwa na mdoriani na kumsababishia hasara kubwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Saidi Sukwa amefika eneo la...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Mjamzito akitumbukiza kichanga chooni akidhani ni haja Unguja

Mama mjamzito aliekuwa akisumbuliwa na uchungu bila yakujitambua nakukimbilia chooni bila ya kujitambua hatimae kujifungua na mtoto kuingia katika shimo la choo.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa asubuhi Gongostore ambapo mama huyo anasadikiwa kuwa mgonjwa wa akili.

Diwani wa Wadi ya Amani Makame Khamis Ame aliekuepo katika tukio hilo amesema “yeye kaona tumbo limemuuma nakuharakia chooni matokezeo yake mtoto ameingia chooni si kwa makusudi pia inasemekana lkidogo hayupo vizuri kiakili...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Msikiti wote wateketea kwa moto Bambi Wilaya ya Kati Unguja

Moto unaothadikiwa umesababishwa na shoti ya umeme katika msikiti wa Ijumaa Bambi umewaacha waumini wa dini ya kiislamu njia panda baada ya Msikiti huo kuteketea wote.

Taarifa zilizopatikana kwa Sheha wa Shehia ya Bambi Amour Hajji Mkombe amesema tukio hilo lakusikitisha limetokea majira ya saa 7 na nusu Usiku huko Bambi Wilaya ya Kati Unguja.

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ameeleza kuwa “msikiti umeungua wote nahakuna kilichobakia nasio kama ufanyiwe matengenezo nilazima ubomolewe...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Afariki Dunia papo hapo baada ya kusagwa na Gari Unguja

Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari wakati akiwa amepanda baskeli.

Tukio hilo lakusikitisha limetokea jana majira ya saa 3 asubuhi huko Mpapa Wilaya ya kati Unguja.

Taarifa kutoka kwa jeshi la Polosi mkoa wa kusini Unguja zinasema kuwa, ajali hiyo imetokea baada ya gari yenye namba za usajili Z 973 JA iliyokuwa ikiendeshwa na Khamis Masoud Ali mwenye umri wa miaka 32 mkaazi wa Magogoni.

Akitokea Dunga njia nne kuelekea  Bambi lipofika Mpapa kwa...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Kijana akutwa amefariki katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Unguja

Kijana mmoja ameokotwa katika Soko kuu la Mwanakwerekwe akiwa ameshafariki dunia huku mwili wake ukiwa na majeraha.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 1 za asubuhi ambapo marehemu huyo hajafahamika jina lake wala anapoishi hadi sasa na anakadiriwa kuwa na miaka 25 hadi 30

Sheha wa Shehia ya Jitimai Rashid Mwadini Omar alieleza kwamba mtuhuyo anasadikika kuwa ameuliwa sehemu ya mbali hatimae kutupwa katika eneo hilo.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Hassan Nassir Ali amesema...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Gari lapinduka na kusababisha ajali mbaya Mlima wa Kiashange Kaskazini Unguja

Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine 16 wamelazwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja na Kivunge kwakupata matibabu baada ya gari waliokuwa wakisafiria kupinduka eneo la Mlima wa Kiashange Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya kusikitisha iliyotokea jana asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Hasina Ramadhan Tawfik amesema ajali hiyo imesababishwa na gari yenye namba Z 216 FB ambayo iliyokuwa ikiendeshwa na Makame Seif Hajji.

Amefahamisha...

 

2 weeks ago

Michuzi

Dkt. Shein Afungua Jengo Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe Unguja,kushoto Waziri Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman na kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Makungu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
BAADHI ya Wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Wavunjifu wa sheria za barabarani watozwa zaidi ya milioni 8 Unguja

Zaidi ya shilingi Milioni nane zimekusanywa kutokana na makosa mbalimbali ya usalama Barabarani yaliyojitokeza   katika Mkoa wa Mjini Magharibi kwa wiki iliyoishia tarehe 4, Februari, 2018.

Akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na Matukio ya wiki ya Mkoa wa Mjini Magharib Kamanda wa Polisi Mkoa huo Hassan Nassir Ali, amesema fedha hizo zinatokana na makosa 191 ya usalama barabarani ambayo yalifikishwa mahakamani na kutozwa fedha hizo taslim kama adhabu.

Amesema katika kukabilia na...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani