5 days ago

Malunde

Membe Amjibu Rostam Aziz Sakata La Kugombea Urais Mwakani

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe amemjibu mfanyabishara Rostam Aziz kuhusu suala la kugombea urais 2020 akimtaka hivi sasa ajikite kwenye masuala ya kitaifa yanayohusu uchumi.

Membe ametoa kauli hiyo akiwa nje ya jengo la Mahakama kuu ya Tanzania, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kusikilizwa kwa kesi anayodai fidia dhidi ya mmiliki wa gazeti la Tanzanite Cyprian Musiba, ambapo aliulizwa swali kuhusiana na kauli inayodaiwa...

 

1 week ago

RFI

Museveni: Nchi za Afrika zinapaswa kuondoa ukomo wa kuwania urais

Mwezi mmoja baada ya Mahakama ya Juu nchini Uganda kuunga mkono hatua ya bunge kuondoa ukomo wa kuwania urais nchini humo, rais Yoweri Museveni anataka mataifa ya Afrika yaondokane na sheria zinazowazuia viongozi wenye umri mkubwa kuwania urais katika nchi zao.

 

3 weeks ago

MwanaHALISI

Dk. Magufuli: Sikustahili urais

RAIS John Magufuli amesema kuwa, hakustahili kuwa Rais wa Tanzania bali Watanzania wenyewe ndio waliomchagua. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Amesema, wananchi wa Mbarali mkoani Mbeya na maeneo mengine ya nchi, ndio walimuona anafaa kushika wadhida huo kati ya wale waliokuwa wanagombea. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo tarehe 2 Aprili 2019, wakati akituhutubia mkutano wa ...

 

3 weeks ago

VOASwahili

Joe Biden aongoza katika kinyanganyiro cha kugombea urais ndani ya chama cha Demokratik

Wakati macho na masikio sasa yanaelekezwa katika siasa za uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao , Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden anaongoza katika kinyanganyiro cha kugombea tiketi ya urais ndani ya chama cha Demokratik kwa mujibu wa kura mpya za maoni zilizotolewa wiki hii.

 

4 weeks ago

BBCSwahili

Uchaguzi Ukraine : Mchekeshaji Zelensky ashinda nafasi ya urais

Petro Poroshenko amekubali matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Volodymyr Zelensky.

 

4 weeks ago

BBCSwahili

Mahakama ya Upeo ya Uganda 'yamsafishia njia' Museveni kugombea tena Urais

Awali umri wa mwisho kwa kugombea ulikuwa ni miaka 75.

 

4 weeks ago

CCM Blog

MCHEKESHAJI VOLODYMYR ZELENSKY ASHINDA URAIS UKRAINE

 Ukraine, Kiew: Wolodymyr Selenskyj (picture-alliance/dpa/Stringer)
Matokeo hayo yanaangaliwa kama maamuzi ya raia waliochoshwa na ufisadi uliotawala katika taifa hilo, pamoja na hali duni ya maisha.Zelensky ambaye uzowefu wake pekee wa kisiasi ni kuigiza kama rais katika kipindi cha televisheni, amemshinda rais aliyekuwa madarakani Petro Poroshenko kwa kunyakua asilimi 73 ya kura zote zilizopigwa, kulingana na matokeo rasmi ambayo hayakukamilika.Poroshenko amepata asilimia 24 ya kura, na kupoteza madaraka kwa Zelensky mwenye umri wa miaka 41, huku asilimia...

 

4 weeks ago

CCM Blog

MAHAKAMA YA JUU UGANDA: MUSEVENI ANAWEZA KUGOMBEA URAIS 2021

Mahakama ya Juu Uganda: Museveni anaweza kugombea urais 2021 Mahakama ya Juu nchini Uganda imeamua kuwa bunge la nchi hiyo lilifuata sheria wakati wa kuondoa kipengeie kilichozua mjadala mkubwa cha ukomo wa umri wa kugombea urais nchini humo, uamuzi ambao unampa nafasi Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 74, kuwania tena urais mwaka 2021.Wakiongozwa na Jaji Mkuu Bart Katureebe, Majaji wanne walitupilia mbali kesi hiyo ya upinzani huku Majaji watatu wakisema bunge halikufuata sheria wakati wa mabadiliko hayo. Uamuzi huo sasa unampa nafasi Rais...

 

5 months ago

VOASwahili

Elizabeth Warren atangaza azma ya urais Marekani 2020

Warren alisema "hata kama tuna tofauti zetu, wengi wetu tunataka kitu hicho hicho. Kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia watu tunaowapenda. Hicho ndicho ninachopigania na ndio maana leo ninazindua kamati ya uchunguzi kwa ajili ya kuwania urais”.

 

5 months ago

CCM Blog

WAPINZANI MADAGASCAR WATAKA KURA ZA UCHAGUZI WA URAIS ZIHESABIWE TENA

Wapinzani Madagascar wataka kura za uchaguzi wa rais zihesabiwe tenaWafuasi wa kambi ya upinzani nchini Madagascar wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo wakitaka kuhesabiwa tena kura za uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni nchini humo.Maandamano hayo yamefanyika siku mbili baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Madagascar kumtangaza Andry Rajoelina kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa rais. Waandamanaji hao wamesema kura za uchaguzi wa rais zinapaswa kuhesabiwa tena na kubaini nani mshindi halisi wa uchaguzi huo. Maelfu ya...

 

5 months ago

BBCSwahili

Marie-Josee Ifoku: Mama wa watoto nane anaegombea urais DRC

Bi Ifoku, mwenye miaka 53 si mgeni katika siasa za Congo.

 

5 months ago

BBCSwahili

Uchaguzi wa DR Congo: Huduma ya Intaneti yafungwa baada ya uchaguzi wa urais

Upinzani unasema kuwa serikali iliagiza hatua hiyo ili kuzuia kutangazwa kwa ushindi wa mgombea wao.

 

11 months ago

RFI

Pierre Nkurunziza : Sintowania muhula mwengine katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020

Wakati wa sherehe rasmi ya utiaji sahihi kwenye Katiba mpya ya Burundi, Rais Pierre Nkurunziza ametangaza kwamba hatowania muhula mwengine katika uchaguzi wa mwaka 2020.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani