(Today) 2 hours ago

VOASwahili

Upinzani Kenya wamchagua Odinga kuwania urais

Raila Odinga amechaguliwa kupeperusha bendera ya upinzani katika kinyang'anyiro cha uchaguzi nchini Kenya. Mgombea huyu amewahi kutumikia nafasi ya waziri mkuu katika serikali ya Kenya.

 

(Today) 3 hours ago

RFI

Kenya: Odinga ateuliwa na muungano wa NASA kugombea urais Agosti 8

Muungano wa upinzani nchini Kenya wa NASA umemtangaza aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga kuwa mgombea wake wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu.

 

(Today) 8 hours ago

VOASwahili

Upinzani Kenya kutangaza mgombea urais

Muungano wa upinzani nchini Kenya, The National Super Alliance, Alhamisi ulitarajiwa kutangaza kiongozi atakayewania urais kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu. Muungano huo Maarufu kama NASA, ulifanya mkutano wake katika bustani za Uhuru Park, mjini Nairobi, ambapo vinara watano wa muungano huo walitarajiwa kutangaza jina la yule atakayepeperusha bendera yao. Vinara hao ni kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, kiongozi wa Wiper National Movement, Kalonzo Musyoka, yule...

 

(Today) 8 hours ago

RFI

Upinzani nchini Kenya kumtaja mgombea wake wa urais

Maelfu ya wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wamefurika katika bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi kusubiri tangazo la mgombea urais kupitia muungano huo.

 

3 days ago

Channelten

Uchaguzi wa Urais Ufaransa, Emmanuel Marcon na Marine Le Pen washinda hatua ya awali

10087561-900-552

Emmanuel Macron atamenyana na Marine Le Pen katika duru ya pili ya Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa Mei saba mwaka huu baada ya wagombea hao wawili kushinda katika kinyang’anyiro cha raundi kwanza kilichokuwa na wagombea wa urais 11.

Macron kwa kupata asilimia 23.9 huku Bi. Le Pen akishika nafasi ya pili kwa asilimia 21.4. katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindani mkali.

Macron mwenye umri wa miaka thelathini na tisa na aliyewahi kuwekeza katika sekta ya benki, hajawahi kuingia...

 

4 days ago

VOASwahili

Uchaguzi mkuu wa urais waanza leo Ufaransa

- Uchaguzi mwaka huu hautabiriki

 

5 days ago

VOASwahili

Ufaransa yaonya magaidi wanaojaribu kuvuruga uchaguzi wa urais

Maafisa wa ngazi ya juu wa Ufaransa wamesema Alhamisi mashambulizi ya risasi jijini Paris na mpango wa mashambulizi uliodhibitiwa na polisi huko Marseilles mapema wiki hii ni sehemu ya jitihada za vikundi vya Kiislamu vyenye siasa kali kuvuruga matokeo ya uchaguzi.

 

6 days ago

BBCSwahili

Uchaguzi wa urais Ufaransa una maana gani kwa Afrika

Uchaguzi wa urais nchini Ufaransa utafanyika Jumapili. Je, uchaguzi huu una maana gani kwa bara la Afrika?

 

6 days ago

Mwanaspoti

Zitto Kabwe ajitosa urais TFF

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika mwezi Agosti, lakini Mwanaspoti limehakikishiwa kwamba mwanasiasa machachari na shabiki wa kulia machozi wa Simba, Zitto Kabwe atawania urais.

 

7 days ago

BBCSwahili

Mahmoud Ahmadinejad azuiwa kuwania urais Iran

Rais wa Iran Hassan Rouhani na mwanasiasa mwenye msimamo mkali Ebrahim Raisi wameidhinishwa kuwania uchaguzi wa urais mwezi ujao nchini humo, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

 

2 weeks ago

Channelten

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hakuzaliwa na urais na anaweza hata kujiuzulu akilazimika na chama chake

849x493q70Ranjeni-SONA2017-1

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hakuzaliwa na urais na anaweza hata kujiuzulu endapo italazimika kufanya hivyo na chama chake.

Zuma amewaambia wafuasi wake wakati akitimiza miaka 75 hapo jana na kuwa chama chake cha ANC kinaweza kuamua kumwondoa madarakani ikiwa kinataka kufanya hivyo.

Kauli hii ya Zuma imekuja baada ya maandamano makubwa katika miji kadhaa jijini Pretoria kumshinikiza Zuma kujiuzulu baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye alikuwa anakubalika sana...

 

2 weeks ago

BBCSwahili

Ahmadinejad kuwania urais licha ya kuonywa na Khamenei

Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, amejiandikisha kuwa mgombea kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuuujao nchini humo

 

2 weeks ago

RFI

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA haujaafikiana kuhusu mgombea urais

Mwafaka bado haujapatikana kati ya vigogo wanne wa kisiasa wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, kuhusu ni nani kati yao atapeperusha bendera ya muungano huo kupambana na rais Uhuru Kenyatta wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu.

 

2 weeks ago

RFI

Vigogo wa muungano wa upinzani nchini Kenya wakutana kumtafuta mgombea wa urais

Vigogo wanne wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wanakutana Pwani ya nchi hiyo kujadiliana na kuamua ni nani kati yao atakayepeperusha bendera ya muungano huo wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.

 

4 weeks ago

Mwananchi

Ogopa Waafrika wanaopewa urais wakiwa wadogo

Kuchukua madaraka ya nchi katika umri mdogo, kunatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazowafanya viongozi wengi wa Afrika kung’ang’ania madarakani.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani