(Today) 40 minutes ago

Michuzi

UVCCM YAVUNA WANACHAMA 350 CHUO KIKUU DAR ES SALAAM


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokea jumla ya Wanachma wapya 350 katika Kongamano Maalum lililoandaliwa na Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Kheri amewataka Vijana wanaopata nafasi za uongozi kuitumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuwakomboa wengine na kuacha kutumika na makundi ya watu.
“Vijana wengi ambao wameaminiwa wameacha kushughulika na matatizo ya Vijana na yenye tija kwa taifa, wamekuwa wakiendeshwa na watu...

 

2 days ago

Michuzi

MWENYEKITI WA UVCCM KHERI JAMES AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALI MBALI WA UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cha Mapinduzi Ndugu Kheri Denis James (MCC) jana amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 17 Februari, 2018.
Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti amesisitiza kuwa  nguvu ya Vijana wa CCM itumike vizuri katika kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchanguzi huo.  ''Suala la ushindi wa CCM...

 

3 days ago

CCM Blog

MWENYEKITI WA UVCCM KHERI D JAMES AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALI MBALI WA UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni, kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis...

 

3 days ago

Michuzi

KATIBU UVCCM IRINGA MJINI ANUSURIKA KUFA BAADA KITU CHENYE MLIPUKA KURUSHWA KITANDANI KWAKE

Aelezea hatua kwa hatua namna nyumba yote ilivyoteketea kwa moto.
Na Said Mwishehe-Globu
KATIBU wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Alophance Myunga amenusurika kifo baada ya kitu chenye mlipuko kurushwa dirishani kwake na kufikia kitandani huku yeye akiwa amelela na kisha kusababisha moto ulioteketeza nyumba anayoishi yote.
Amesema kutokana na kurushwa kwa kitu hicho ambacho kilisababisha mlipuko mkubwa chumbani kwake na kisha moto kuanza kuwaka alichofanikiwa ni...

 

4 days ago

Michuzi

MWENYEKITI WA UVCCM AINGIA RASMI KAZINI

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kheri D James akisalimiana na Mtumishi wa Makao Makuu ya Umoja wa Vijana  wa CCM Bi.Sheila Alipowasili katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Umoja wa Vijana Wa CCM Upanga.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Taifa Ndg.Shaka Hamdu Shaka (kwanza kushoto)akimtambulisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James kwa Makatibu wasaidizi wakuu alipowasili ofisi ndogo za UVCCM Upanga.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja...

 

1 week ago

Michuzi

UVCCM KIBAHA MJINI YAWATAKA VIJANA KUSIMAMIA KWA VITENDO MAPINDUZI

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.
JUMUIYA ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mjini Kibaha mkoani Pwani imesema Taifa linawategemea vijana katika dhana nzima itakayothibitisha wanasimamia kwa vitendo Mapinduzi katika kuondoa maovu yanayolikabili Taifa hili.
Aidha imekemea tabia ya kujigawa na kuweka makundi baina yao kwani kwa kufanya hivyo ni kudidimiza harakati na juhudi za kuimarisha jumuiya na kupambana kimaendeleo .
Mwenyekiti wa UVCCM Mji wa Kibaha, Azilongwa Bohari aliyasema hayo, mara...

 

1 week ago

Zanzibar 24

BAVICHA wamjia juu kaimu katibu mkuu UVCCM kisa Tundu Lissu

Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Julius Mwita amesema kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka huenda ana matatizo ya akili.

Mwita amesema hayo leo Januari 11, 2018 katika Mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu tuhuma alizotoa kiongozi huyo wa UVCCM dhidi ya Tundu Lissu ambapo alisema kuwa Tundu Lissu ni muongo na hapaswi kuaminiwa kwani anatafuta tu umaarufu.

Kufuatia...

 

3 weeks ago

CCM Blog

UVCCM YAPONGEZA MIRADI YA AFYA TABORA.

Na Mwandishi wetu,Tabora 

Umoja wa Vijana wa CCM umesema umeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotokana na ahadi katika ilani ya uchaguzi katika halmshauri za wilaya mji  wa Nzega na Nzega vijijini mkoani Tabora. 

Pia Umoja huo umeeleza kikubwa kasi hiyo inatokana na kuwepo kwa mashirikiano makubwa kati ya viongozi wa chama,halmashauri za wilaya na serikali kuu. 
Matamshi hayo yametamkwa jana na Mwenyekiti  wa Taifa wa UVCCM Kheri Denise james mara baada ya kumaliza...

 

3 weeks ago

CCM Blog

MABODI AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO KWA UVCCM

MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheir James(kushoto) akitowa na  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk. Abdalla Juma Saasalla (Mabodi) wakati akitoa shukrani kwa mapokezi aliyopata zanzibar yeye na ujumbe wake.
------------
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  Dk. Abdalla Juma Saadalla (Mabodi)  amewahakikishia  Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) kuwa ataendelea kushirikiana nao katika masuala  mbali mbali ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Ahadi hiyo...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

UVCCM watakiwa kuachana na majungu ili kuimarisha chama

Vijana wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, wametakiwa kujiepusha na tabia ya majungu na makundi ambayo yanaweza kuhatarisha uhai wa chama

Akizungumza katika mapokezi ya uongozi mpya wa Umoja wa Vijana Taifa wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mwenyekiti wa wa Umoja Kheir Denis James katika makao makuu Gymkhana mjini Zanzibar, alisema panapo makundi ni vigumu kustawisha chama.

“Lazima sisi vijana tutambue wajibu wetu, chama kinatutegemea ili kukiimarisha na kuwa mfano wa uongozi bora unaofuata...

 

4 weeks ago

Malunde

UVCCM WAUNDA YAUNDA KAMATI KUFUATILIA VITEGA UCHUMI NA MALI ZAO
Umoja wa Vijana UVCCM, umeunda kamati ya kufuatilia vitega uchumi na mali za umoja huo nchi nzima. 
Kamati hiyo inaundwa na wajumbe nane na itaongozwa na Mariam Chaurembo.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema kamati hiyo inakwenda kuchunguza na kuangalia vitega uchumi na mali zote za umoja huo.

"Mwenyekiti ameanza na kazi hii ili aweze kujua mali na vitega uchumi na umoja viko katika hali gani na vinaendeshwaje,"

"Wajumbe hawa watafanya kazi hiyo kuanzia leo wakiangalia na...

 

4 weeks ago

Michuzi

UVCCM YATAJA MAJINA YA WATAKAOHAKIKI MALI ZA JUMUIYA YAO

Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) imetaja majina sita kati ya wanane ya wajumbe walioteuliwa  katika Kamati ya kuchunguza na kufuatilia mali za chama.
Hatua hiyo imekuja kutokana na maagizo ya Mwenyekiti wa Umoja huo Kheir James kutaka kuhakikiwa kwa mali zote za umoja huo.
Akizungumza leo katika Makao Makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa umoja huo Shaka Hamdu Shaka ametaja majina ya wajumbe wa kamati hiyo ambayo itaongozwa na...

 

1 month ago

Michuzi

MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA KHEIR JAMES AKUTANA NA WENYEVITI NA MAKATIBU WA MKOA MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Ndg Kheir James  (MCC) amekutana na kufanya mazungumzo na Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote nchini wa UVCCM.  
Kikao hiko kimefanyika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Dodoma kilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM  Ndg Tabia Mwita Maulid na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka. Baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa yote nchini wa UVCCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Ndg Kheir James  (MCC)...

 

1 month ago

MwanaHALISI

Aliyekuwa bosi wa UVCCM apata dhamana

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Dodoma imemwachia kwa dhamana aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis (Mbunge) anayekabiliwa na mashtaka ya kutoa rushwa wakati wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa UVCCM Taifa, anaandika Hamisi Mguta. Sadifa ameachiwa leo Desemba 19, 2017 baada ya mahakama kutupilia mbali pingamizi la upande wa mashtaka ...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Mahakama yamuachia kwa dhamana aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imemwachia kwa dhamana aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis (Mbunge) anayekabiliwa na mashtaka ya kutoa rushwa wakati wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa UVCCM Taifa.

Sadifa ameachiwa leo Desemba 19, 2017 baada ya mahakama kutupilia mbali pingamizi la upande wa mashtaka ambao waliliwasilisha mahakamani hapo kuweka zuio la kupewa dhamana.

Mtuhumiwa huyo ametakiwa kudhaminiwa na watu watatu pamoja na kusaini bondi ya Tsh....

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani