(Yesterday)

Michuzi

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Yakabidhi Hundi ya Milioni Hamsini Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda Kuchangia Ujenzi wa Vyumba Vya Walimu wa Shule za Jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo...

 

1 day ago

Zanzibar 24

Milioni 50 zatolewa kusaidia ujenzi wa ofisi za walimu 402

Benki ya watu wa  Zanzibar (PBZ) imetoa msaada wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 50 kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ili kusaidia ujenzi wa ofisi za walimu 402 katika mkoa huo.

Akikabidhi hundi ya fedha hiyo MJINI Zanzibar Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Juma Ameir Hafidhi amesema mbali na kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wamelazimika kufanya hivyo kwakuwa asilimia 53 ya faida ya benki hiyo inatoka kwenye matawi yaliyopo Jijini Dar es...

 

1 week ago

BBCSwahili

Zaidi ya walimu 20,000 waliofeli mtihani wa wanafunzi wao kufutwa Nigeria

Walimu hao kutoka jimbo la Kaduna walifeli mtihani unaostahili kufanywa na wanafunzi wao

 

1 week ago

Zanzibar 24

Wizara ya Elimu: Maslahi ya walimu lazima yaende sambamba na majukumu ya ufundishaji

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imesema madai ya walimu juu ya maslahi mazuri, lazima yaende sambamba na utekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji kama inavyopasa.

Naibu Waziri wa wizara hiyo Mmanga Mjengo Mjawiri, amesema ufundishaji usiokidhi viwango ni miongoni mwa sababu kadhaa zinazoshusha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Akizungumza leo Oktoba 8, 2017 katika kongamano lililofanyika kwenye ukumbi wa Sanaa Rahaleo kwa ajili ya kuadhimisha ‘Siku ya Walimu Duniani, Mjawiri alisema...

 

2 weeks ago

Michuzi

UNESCO, ILO, UNICEF, UNDP NA EDUCATION INTERNATIONAL YATOA SALAMU KWA WALIMU DUNIANI

Kufundisha Kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu Walimu ni msingi mkuu katika ustawi wa muda mrefu wa kila jamii kwa kuwa hujishughulisha kuwapatia watoto, vijana na watu wazima elimu na ujuzi wanaohitaji ili kufikia uwezo wao. 
Lakini duniani kote, walimu wengi sana hawana uhuru na msaada wanaohitaji kufanya kazi yao iliyo muhimu sana. Ndiyo maana maudhui ya Siku ya Walimu Duniani kwa mwaka huu – ‘'Kufundisha kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu'’ - inathibitisha thamani ya walimu waliowezeshwa na...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Walimu wapewa onyo Pemba

Mkuu wa Mkoa wa Mkaskazini Pemba, Omar Khamis Othman amesema, katika kutekeleza agizo la Rais wa Zanzibar Dk: Ali Mohame Shein kuhusiana na walimu watoro, ameanza kwa kupata orodha ya walimu wote wa mkoa wake, ili iwe rahisi wakati atakapofanya ziara za ghafla skulini, kuwatambua.

Akizungumza na Zanzibarleo Ofisini kwake Wete alisema, watahakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Rais wanayatekeleza ipasavyo likiwemo hilo la waalimu watoro.

Alisema kuwa, walimu hao atawafuatilia kwa kuwapitia...

 

3 weeks ago

Channelten

Mkazo masomo ya sayansi shule za sekondari, Walimu Ubungo,Dsm,wabadilishana mbinu shirikishi za Ufundishaji

IMG_8749

Walimu zaidi ya mia moja wa Masomo ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za Serikali Wilaya ya Ubungo,Mkoani Dar Es Salaam,wamesema dhana kuwa masomo ya sayansi ni magumu,inatokana na masomo hayo kutokuwa katika mfumo shirikishi na kwamba umefika wakati sasa,masomo hayo kufundishwa katika mfumo huo.

Baadhi ya walimu hao,wameimbia Channel Ten,katika mahojiano maalum,wakati wa mafunzo maalum yaliyolenga kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kufundisha masomo hayo,ambayo ndiyo msingi mkuu wa...

 

3 weeks ago

Channelten

Ujenzi wa Ofisi za Walimu DSM, Wadau waendelea kujitokeza kuunga mkono kampeni

MAKONDA PAUL

Wadau mbalimbali wa masuala ya elimu jijini dsm wameendelea kujitokeza kuunga Mkono Kampeni ya ujenzi wa Ofisi za walimu 402 pamoja na Vyoo kampeni inayolenga kuweka mazingira mazuri ya walimu wa shule za Msingi na Sekondari ili kuongeza ufanisi ya Utendaji wao.

Akizungumza katika kikosi cha jeshi cha JKT Mgulani ambapo ameshuhudia mifuko elfu kumi ya saruji ambayo inatokana na shilingi millioni mia moja zilizotolewa hivi karibuni na benki ya CRDB kutoka kampuni ya Saruji ya Kisarawe ambapo...

 

3 weeks ago

Michuzi

Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu Dar

Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni.
Mafunzo hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua...

 

3 weeks ago

Channelten

Ukaguzi wa Vyeti Feki, Walimu 51 waondolewa Babati

VYETI FEKI

Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, inakabiliwa na upungufu wa walimu 400 wa shule za msingi, baaada ya zoezi la ukaguzi wa vyeti feki kuwaondoa kazini walimu 51, na mwisho wa mwaka huu walimu wengine 27 wakitarajia kustaafu na hivyo kutishia maendeleo ya taaluma ya elimu kwenye wilaya hiyo.

Kaimu Afisa Elimu wa wilaya ya Babati Bw Julias Sikay, ameiomba wizara ya elimu, sayansi na Teknolojia kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo la upungufu wa walimu wa shule za msingi...

 

3 weeks ago

Channelten

Ujenzi wa Ofisi za Walimu DSM, CRDB yakabidhi hundi ya Shs Milioni 100 kwa kamati

MAKONDA CRDB

Katika kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda pamoja na kamati ya Ujenzi wa ofisi 402 za walimu na Vyoo Benki ya CRDB leo imekabidhi hundi ya shilingi Millioni mia moja kwa ajili ya Kuunga mkono ujenzi ofisi za walimu katika Mkoa wa Dsm.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt.Charles Kimei akizungumza kabla ya kukabidhi hundi amesema ameguswa na Kampeni hiyo ya ujenzi wa ofisi za walimu pamoja na ubunifu wenye tija unaofanywa na Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Paul...

 

3 weeks ago

Michuzi

CRDB BANK YACHANGIA MIL. 100 ZA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU JIJINI DAR

Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kusaidia Ujenzi wa ofisini za walimu wa Shule za msingi na Sekondari za jijini Dar es salaam, leo Septemba 25, 2017. Makabidhoano hayo yamefanyika kwenye ofisi ya ya Mkuu wa Mkoa. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa ofisi hizo za waalimu, Kanali Charles Mbuge na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na...

 

4 weeks ago

Channelten

Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za walimu Dar es salaam yapokea Matofali 1000

Kamati ya Kuratibu na kusimamia ujenzi wa ofisi za walimu Katika shule za msingi na sekonda katika mkoa wa Dar es salaam, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Col. Charles Mbuge Imepokea Matofali 1000. Kutoka kwa Thobias Hima na Kampuni yake ya A&Bal impex (T) Ltd
Makabidhiano hayo yalifanyika katika eneo la Kigamboni kata ya Sumangira.

Screen Shot 2017-09-23 at 9.01.56 PM
Vilevile kampuni hiyo ya A&Bal impex (T) LTD imetoa ruhusa kwa kamati kutumia eneo lake na Mashine yake ya kufyatulia ili itumike na kamati wakati wa usiku...

 

4 weeks ago

Channelten

Kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu katika shule za msingi na sekondari imepokea matofali 1000 kutoka kampuni A&bal impex (T) ltd

4

Kamati ya kuratibu na kusimamia ujenzi wa ofisi za walimu katika shule za msingi na sekondari jijini Dar es salaam ikiongozwa na mwenyekiti Col. Charles MbugeLeo imepokea matofali 1000 kutoka kwa Thobias Hima na kampuni yake ya A&bal impex (T) ltd. Makabidhiano hayo yalifanyikao ktk eneo LA sumangira kigamboni.
Wengine waluohuria ni Makamu mwenyekiti, katibu na wajumbe was kamati.

 

321

Share on: WhatsApp

The post Kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu katika shule za msingi na sekondari imepokea...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani