(Yesterday)

Michuzi

Udahili wa wanafunzi wanaotaka kujiunga Vyuo Vikuu Kuanza Julai 22, 2017


Na Lilian Lundo - MAELEZO.Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) umeutangazia Umma kuwa kuanzia Julai 22 mwaka huu vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini vitaanza kupokea maombi ya udahili kwa mwaka wa masomo  2017/2018.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Eleuther Mwageni (pichani) ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza rasmi udahili kwa mwaka 2017/2018.Prof. Mwageni amesema kuwa waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao  kwenye vyuo...

 

(Yesterday)

MwanaHALISI

TCU yajivua rasmi udahili wa wanafunzi

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imejivua rasmi jukumu la kusimamia suala la udahili kwa wanafunzi ambao wanatarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu mwaka huu , anaandika Hellen Sisya. Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya tume hiyo mapema leo hii, Eleuther Mwageni , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo amesema ...

 

2 days ago

Malunde

MOTO WATEKETEZA BWENI LA WANAFUNZI SHULE YA BUNAMBIYU, NYUMBA YA MFANYABIASHARA NAYO YATEKETEA

Bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Bunambiyu iliyopo katika kata ya Bunambiyu wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga limeteketea kwa moto na kuteketeza mali za wanafunzi 26 wa kike waliokuwa wanalala katika bweni hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Muliro Jumanne Muliro alisema tukio hilo limetokea Julai 17,2017 majira ya saa mbili asubuhi.
Alisema mwalimu wa shule hiyo Wilfred John (28) alibaini bweni kuungua moto na kuteketeza mali za wanafunzi 26 wa kike waliokuwa wanalala...

 

3 days ago

Michuzi

BALOZI ADADI :AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANSI

MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa nchini. Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa chini. Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika...

 

3 days ago

Channelten

Jukwaa la kuvuna wataalamu, Wanafunzi waliosoma vyuo vya nje watakiwa kuunda umoja wao

WhatsApp Image 2017-06-09 at 15.16.49

WAZIRI wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga, amesema wanafunzi wahitimu kutoka vyuo vya nje ya nchi waunde umoja wa mataifa waliyotoka, ili kuwa na jukwaa la kuvuna wataalamu pamoja na wao kutambuana.

Amesema hayo wakati akizindua Chama cha wanafunzi waliosoma China (CAAT), jijini Dar es salaam, ambapo alibainisha vyama vingi vya aina hiyo vimeanzishwa na kupotea kutokana na kukosa msukumo kutoka serikalini.

Amesema wao watakuwa kiungo kati ya...

 

5 days ago

Mwananchi

Walimu shule zilizoshika mkia kidato cha sita watoa sababu za wanafunzi kufeli

Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yametoka huku kama kawaida kukiwa na shule kumi zilizofanya vizuri, na kumi zilizofanya vibaya.

 

5 days ago

Malunde

WANAFUNZI 10 WAFUTIWA MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA SITA 2017Wakati matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yakitolewa leo, Jumamosi Julai 15, imebainika kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu.


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.

Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.

Watahiniwa hao walishindwa...

 

6 days ago

Mwananchi

Wanafunzi watakiwa kupewa elimu ya kujiwekea fedha

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewashauri walimu kuisaidia Benki ya NMB kutoa elimu ya masuala ya kibenki hasa umuhimu wa kujiwekea akiba  kwa wanafunzi wao ili iweze kuwasaidia hapo baadaye.

 

7 days ago

Michuzi

TAESA IKISHIRIKIANA NA ILO YAANDAA PROGRAMU ENDELEVU YA MIAKA MITATU YA KUWANOA WANAFUNZI WA VYUO KUWAJENGEA UWEZO WA KUSHIRIKI KATIKA KAZI KWA VITENDO


Pichani kati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa huduma za ajira, Saneslaus Chandaruba akizungumza jambo mbele ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali,waliohudhuria programu endelevu ya miaka mitatu nchini,iliyohusu jinsi ya kuwajengea Misingi bora wanavyuo ya ufanisi wa kazi katika ushiriki wa kazi kwa vitendo katika ofisi au kampuni tofauti Nchini (intern/ Field work).Programu hiyo imefanyika jijini na kuandaliwa na Wakala wa Huduma za Ajira Tz (TaESA ) kwa kushirikiana na Shirika la kazi la Kimataifa...

 

1 week ago

Mwananchi

Utafiti: Wanafunzi wengi wana ndoto ya kuwa mameneja, maofisa

Wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu nchini wamesema wanapenda kuwa wakurugenzi, mameneja au ofisa wa juu katika vitengo walivyovisomea.

 

1 week ago

Mwananchi

Shirika laongeza uwezo wa wanafunzi kujifunza kwa kucheza

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali duniani la Right to Play, Kevin Frey amewasili nchini kuona utekelezaji unaofanywa na shirika hilo kuongeza uwezo wa kujifunza kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi kupitia michezo.

 

1 week ago

MwanaHALISI

Wanafunzi wajawazito wamganda Rais Magufuli

WANAFUNZI wa wanaopata ujauzito kutorudi shuleni kimezidi kumng’ang’ania Rais John Magufuli hali iliyosababisha kuendelea kupigilia misumali kila anapopata nafasi ya kulizungumzia hilo, anaandika Irene Emmanuel. Rais Magufuli alishapiga marufuku wanafunzi wanaopata ujauzito kurudi shuleni na kuzuia asasi zisizo za kiserikali kuendelea kutetea hilo, lakini pamoja hayo bado amezidi kupinga kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo. ...

 

2 weeks ago

Michuzi

WAKUU WA SHULE BINAFSI WALIPE BIMA ZA AFYA KWA WANAFUNZI –SPIKA MSTAAFU MAKINDA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, ,Anne Makinda amesema wakuu wa shule binafsi wanachukua fedha za huduma ya matibabu ya afya kwa wanafunzi lakini wanafunzi hao wamekuwa hawapati huduma wanazostahili na kulingana na kiasi walicholipia. 
Wakuu wa Shule binafsi wamekuwa wakilipisha wanafunzi fedha za huduma ya matibabu ikiwa ni njia moja ya maelezo kujiunga (joining instruction) ila inapotokea mtoto anaumwa humrudisha kwa wazazi wake. 
Mwenyekiti huyo...

 

2 weeks ago

Mwananchi

Wanafunzi Lucky Vincent kurejea mwezi ujao

Wanafunzi watatu wa Shule ya Lucky Vincent ambao walijeruhiwa katika ajali iliyotokea Mei 6 na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva, watarejea mwezi ujao.

 

2 weeks ago

Malunde

BODI YA MIKOPO KUTANGAZA SIFA NA VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPANGIA WANAFUNZI MIKOPO 2017/2018Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema hivi karibuni itatangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia wanafunzi mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaotarajia kuanza miezi michache ijayo.


Ufafanuzi huo umetolewa jana (Ijumaa, Julai 7, 2017) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya wateja waliotembelea Banda la HESLB katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani