4 months ago

Michuzi

TPA TANGA YAIBUKA MSHINDI KWA TAASISI ZA KISERIKALI ZILIZOSHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI TANGA

Naibu Waziri wa Maliasilia na Utalii Japhet Hasunga kushoto akimkabidhi Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kombe la mshindi wa kwanza wa taasisi za serikali zilizoshiriki maonyesho ya biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakifanyika Jijini Tanga na kumalizika hivi karibuni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akiwa na kombe la mshindi wa kwanza wa taasisi za serikali zilizoshiriki maonyesho ya biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakifanyika Jijini Tanga akiwa na watumishi wa Bandari hiyo

 

4 months ago

VOASwahili

Kashfa mpya ya ufisadi yaibuka Kenya

Sakata nyingine ya ufisadi inayokumba utawala wa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, imejitokeza baada ya tume iliyochunguza jinsi pesa za umma zilivyotumiwa na wizara ya misitu, kutoa ripoti inayoonyesha kwamba takriban shilingi bilioni mbili, zilizotengewa  mradi wa upandajji miti katika shule, kwenye maeneo mbalimbali ya nchi, zimepotea.

 

4 months ago

Michuzi

REMA 1000 FC YAIBUKA KINARA,YAIFUMUA LAMBO FC MABAO 5-3

Kurugenzi CUP ’18 yazidi kutimua vumbi katika dimba la shule ya msingiHaydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, kwa timu ya Rema 1000 FC kwa
kuigaragaza pasipo huruma timu ya Lambo FC kwa mabao 5-3.

Katika mchezo huo uliofanyika leo alasiri timu hizo zilitoana jasho,
upinzani mkali, katika kulisakata kabumbu na kuonyeshana ufundi,
kwenye mashindano hayo  yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga.

Bao la kwanza la timu ya Rema 1000 FC lilitiwa kimiani na...

 

4 months ago

BBCSwahili

Mapya yaibuka dhidi ya Raisi Trump

Rais Trump amekubali rasmi kwamba alimlipia mwanasheria wake binafsi zaidi ya dola laki moja

 

5 months ago

Zanzibar 24

Maradhi ya Ebola yaibuka tena DR Congo

Wizara ya afya DR Congo imetangaza visa vipya vya ugonjwa wa Ebola kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambavyo vilivyothibitishwa na watu 17 waliofariki.

Wataalam wa maradhi ya Ebola kutoka wizara ya afya nchini Congo leo Jumatano wanatarajiwa kuambatana na wale wa shirika la afya duniani WHO kwenda jimboni Equateur baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa visa hivyo.

Kisa kilichotokea katika mji wa Bikoro kinajiri zaidi ya mwaka baada ya mlipuko wa ugonjwa huo kusababisha vifo...

 

5 months ago

Michuzi

Timu ya Ngobanya yaibuka mshindi wa May Day Tornament

Na Chalila Kibuda, Globu Jamii

TIMU ya Ngobanya imeibuka mshindi kati fainali ya May Day Tornament baada ya kuibamiza timu ya Lake Cement kwa bao 2 kwa moja katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kimbiji kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika fainali hiyo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni…. Alisema kuwa mpira wa miguu unaibua fursa kwa vijana katika kuonyesha kipaji na baadaye kujipatia kipato.
Amesema utaratibu unaofanywa na kiwanda cha Saruji cha Lake Cement...

 

6 months ago

Malunde

MAPYA YAIBUKA SAKATA NA MUUGUZI KUPIGWA NGUMI ZA USO SHINYANGA..DIWANI AFUNGUKA KILA KITU (Video)


Diwani wa kata ya Bunambiu Richard Sangisangi (CCM).
Sakata la Muuguzi wa kituo cha afya Bunambiu kilichopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Hilda Simon (35) kudaiwa kupigwa ngumi usoni na kifuani na diwani wa kata hiyo Richard Sangisangi (CCM) limechukua sura mpya baada ya diwani huyo kuibuka na kusema hakumpiga muuguzi huyo. 

Leo Alhamis Machi 15,2018 Sangisangi amefika katika ofisi ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa taarifa zilizotolewa kuwa...

 

7 months ago

Malunde

CCM YAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI UDIWANI ISAMILO...ASILIMIA 2.2 TU NDIYO WALIOPIGA KURA
Mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa kata ya Isamilo jijini Mwanza, Nyamasiriri Marwa ameibuka kidedea kwenye uchaguzi ulioshuhudia asilimia 2.2 pekee ya wapiga kura 18,029 waliandikishwa ndiyo waliojitokeza kupiga kura.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Februari 17, Nyamasiriri ametangazwa mshindi kwa kupata kura 2,220 sawa na asilimia 57 ya kura halali 3,920 zilizopigwa.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Kiomoni Kibamba mgombea kupitia Chadema, John Kisieri amepata kura 1,678...

 

7 months ago

Michuzi

CCM YAIBUKA KIDEDEA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

 Bw. Maulid Mtulia wa Chama cha Mapinduzi(CCM)  akionesha hati yake ya ushindi baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Ubunge, Jimbo la Kinondoni, mkoani Dar es salaam  baada ya kupata kura 30,313 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Salum Mwalim (CHADEMA) aliyepata kura 12,353...Chini ni fomu rasmi ya matokeo hayo.

 

7 months ago

Malunde

CCM YAIBUKA MSHINDI UCHAGUZI SIHA,,,MOLLEL NDIYE MBUNGE Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro baada ya Tume ya Uchaguzi (Nec), kumtangaza Dk Godwin Mollel kuwa mshindi wa kiti hicho.Nec imemtangaza rasmi Dk Mollel kuwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kupata kura 25,611 huku akiwaacha mbali wapinzani wake,  Elvis Mosi wa Chadema, Elvis Mosi aliyepata kura 5,905 na mgombea wa CUF, Tumsifueli Mwanri aliyepata kura 274 huku Mdoe Azaria wa Sau akiambulia kura 170.Kwa upande wa...

 

8 months ago

VOASwahili

Philadelphia Eagles yaibuka mshindi wa Superbowl Marekani

Fainali za mpira wa Football ya Marekani maarufu kama Superbowl ikiwa ni ya 52, uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki kati ya timu ya New England Patriots na Philadelphia Eagles umemalizika. Mchezo huo ulikuwa unafanyika katika jiji la Minneapolis kwenye jimbo la Minnesota na timu ya Philadelphia Eagles imeibuka mshindi kwa point 41 dhidi ya 33 za New England Patriots.  Huu ni ushindi wa kwanza kabisa wa Eagles baada ya kufika finali mara tatu katika kipindi cha miaka 39...

 

8 months ago

BBCSwahili

CHAN 2018: Sudan yaibuka ya tatu baada ya kuishinda Libya kwa penalti

Kipa wa Sudan Akram ameokowa penalti mbili kuchangia ushindi wa timu yake katika nafasi ya tatu ya kombe la ubingwa wa mataifa ya Afrika huko Morocco.

 

8 months ago

Malunde

TANZANIA YAIBUKA KINARA AFRIKA UCHUMI JUMUISHI

Baada ya Tanzania kuibuka kinara wa Uchumi Jumuishi barani Afrika, baadhi ya Wataalamu wa masuala ya uchumi nchini wameelezea kuwa hatua zinazochikuliwa na Serikali kuwawezesha wanachi kuwekeza katika shughuli za kiuchumi na utoaji bora wa huduma za jamii vitaufanya uchumi wa Tanzania kuendelea kukua zaidi.


Wakitoa maoni yao juu ya dhana ya uchumi jumuishi, baadhi ya wataalamu hao wamesema kuwa madiliko ya sera na sheria zinawawezesha wananchi wengi kumiliki uchumi ni sehemu ya vigezo vya...

 

9 months ago

Michuzi

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAIBUKA KIDEDEA TAARIFA BORA YA HESABU KWA MWAKA 2016


Benny Mwaipaja-WFM, Dar es Salaam
Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50)linalohusika na masuala ya utawala, limeibuka kinara kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2016 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James katika...

 

10 months ago

Malunde

MAPYA YAIBUKA MWANAMKE KUMVALISHA PETE YA UCHUMBA MWANAMKE MWENZAKE GEITA
Sakata la mwanamke aliyemvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwatia mbaroni watu wengine watatu akiwemo aliyevishwa pete.
Sura mpya ya kwanza ni mtuhumiwa Milembe Suleiman (36), anayedaiwa kumvalisha pete mwanamke mwenzake Janeth Shonza, aliyekuwa akishikiliwa na polisi mkoani Geita kuhamishiwa mkoani Mwanza.
Pili, jeshi la polisi pia limefanikiwa kumtia mbaroni mwanamke aliyevishwa pete, Janeth Shonza (25), mwanafunzi wa mwaka wa...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani