3 weeks ago

VOASwahili

Kenya yapiga marufuku matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya kisiasa

mamlaka ya mawasiliano ya Kenya, imetangaza kupigwa marufuku kwa upeperushaji wa matangazo ya moja kwa moja wa mikutano ya kisiasa, katika kile ilichokiita “kusaidiA kupunguza hali ya taharuki nchini.”

 

4 weeks ago

BBCSwahili

Somaliland yapiga kura katika uchaguzi wa urais

Shughuli ya kupiga kura imeanza katika Jamhuri iliojitangaza ya Somaliland katika uchaguzi wa urais.

 

1 month ago

Zanzibar 24

Uvccm yapiga msasa vijana wake, yahoji utekelezaji wa ilani

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Wilaya ya Mjini, Hudhaima Mbarouk Tahiri amewasihi vijana walioshindwa kuendelea na elimu ya juu kutokata tamaa badala yake watumie fursa ya sekta ya ujasiriamali kujiajiri wenyewe.

Wito huo ameutoa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka miwili ndani ya Jimbo la Kikwajuni Unguja.

Amesema vijana wanatakiwa kuwa wabunifu katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kujiunga...

 

1 month ago

VOASwahili

Marekani yapiga hatua katika shambulizi la ISIS Somalia

Marekani imefanya shambulizi la anga kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya wapiganaji wa Kikundi cha Islamic State nchini Somalia Ijumaa na kusema imepiga hatua ya kipekee katika vita hii.

 

1 month ago

Zanzibar 24

Burundi yapiga marufuku wanawake kupiga ngoma

Serikali ya Burundi imepiga marufuku upigaji wa ngoma katika mikutano isiokuwa rasmi ikiwemo sherehe za kitamaduni na harusi katika jaribio la kuhifadhi mila hiyo ya zamani ambayo inajuliakana kimataifa.

Makundi yote yanayotaka kufanya tamasha za kitamaduni sasa yatalalizimika kujisajili na wizara ya Utamaduni na hayataruhusiwa kupiga ngoma kando na mikutano rasmin ya serikali bila ruhusa , agizo ambalo limetiwa saini na rais Pierre Nkurunziza.

Hatahivyo wanaweza kushiriki katika kucheza...

 

2 months ago

Channelten

Biashara ya Mahindi kutoka nchi jirani ya Rukwa, Serikali yapiga marufuku wafanyabiashara kuyaingiza kwa magendo

 

SERIKALI mkoani Rukwa imepiga marufuku utaratibu wa wafanyabiashara kuingiza mahindi mkoani humo kutoka nchi jirani ya Zambia kwa kutumia njia za panya na kuyauza kwa bei ya chini inayosababisha mahindi yaliyolimwa nchini kukosa soko na kuikosesha serikali mapato.

Ziara ya ghafla ya mkuu wa mkoa wa Rukwa katika mpaka usio rasmi wa Safu umebaini kushamiri kwa biashara haramu ya kusafirisha mahindi kutoka nchi jirani ya Zambia kwa kutumia njia za panya bila kulipia tozo halali za serikali...

 

2 months ago

Channelten

Hali ya Kisiasa Nchini Kenya, Serikali yapiga marufuku maandamano baadhi ya maeneo

bomet_university_title_deed_legal_says_cs_matiangi_29089_L

Serikali ya Kenya imetangaza kupiga marufuku maandamano ya wafuasi wa upinzani NASA katikati ya miji nchini humo.

Waziri wa Usalama na Mambo ya ndani Fred Matiang’i, amesema maandamano hayo hayataruhusiwa katikati ya jiji la Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Matiang’i ameongeza kuwa hatua hii imechukuliwa baada ya baadhi ya waandamanaji wa upinzani kupora mali ya watu katika miji hiyo siku ya Jumatano.

Aidha, Waziri huyo amefafanua kuwa serikali haiwezi kuzuia maandamano kwa sababu ni haki ya...

 

2 months ago

VOASwahili

Serikali Kenya yapiga marufuku maandamano

Wakati vyama vya upinzani nchini Kenya vikiahidi kufanya maandamano wakidai kuwepo mabadiliko kabla ya marejeo ya uchaguzi wa urais kufanyika, serikali imepiga marufuku maadamano katika miji mikuu mitatu.

 

2 months ago

RFI

Serikali ya Kenya yapiga marufuku maandamano ya upinzani katikati ya miji

Serikali ya Kenya imetangaza kupiga marufuku maandamano ya wafuasi wa upinzani NASA  katikati ya miji  nchini humo.

 

2 months ago

BBCSwahili

Serikali Kenya yapiga marufuku maandamano miji mikuu

Serikali nchini Kenya imepiga marufuku maandamano katika maeneo ya katikati mwa miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

 

2 months ago

BBCSwahili

UN yapiga marufuku meli nne juu ya Korea Kaskazini

Umoja wa Mataifa umepiga marufuku meli nne dhidi ya kufika kwenye bandari za kimataifa baada ya kubainika kwamba zilikiuka vikwazo vilivyowekewa Korea Kaskazini na umoja huo.

 

2 months ago

Channelten

Cameroon yapiga marufuku Mikutano maeneo yanayozungumza Kiingereza

516757DF-6DDF-45D9-BEB9-A8EA4DD31A70_mw1024_mh1024_r1_s

Maafisa nchini Cameroon hapo wamepiga marufuku kwa siku tatu mfululizo, mikutano yoyote ya kuanzia watu wanne na zaidi, katika mkoa wake unaozungumza lugha ya Kiingereza.

Aidha wameamuru kufungwa kwa vituo vya mabasi, migahawa na maduka na kupiga marufuku mizunguko ya watu katika maeneo ya mkoa huo.

Hatua hiyo inalenga kuzuia maandamano ambayo yamepangwa na Wacameroon wanaozungumza Kiingereza kesho-Jumapili, kwa kile wanachosema ni maovu dhidi yao na kutengwa na serikali ya rais Paul Biya,...

 

3 months ago

Malunde

WAZALENDO YAPIGA JEKI UJENZI WA BWENI SHULE YA NAPS KAGERA


Mwalimu wa taaluma wa shule ya Ngara Anglican Primary School (NAPS) God Marco Gwabunga God Gwabunga (kushoto) akipokea saruji kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Wazalendo Media Productions Limited,Hilali Ruhundwa. Mifuko ya saruji iliyotolewa na Kampuni ya Wazalendo Media Productions LimitedBweni la shule hiyo

Kampuni ya Wazalendo Media Productions Limited ya Dar es Salaam imechangia mifuko saba ya saruji kwa shule ya Ngara Anglican Primary School (NAPS) iliyopo wilayani Ngara...

 

3 months ago

BBCSwahili

Kurdistan yapiga kura ya uhuru Iraq

Licha ya upinzani kutoka Iraq na mataifa mengine, Wakurdi wanapiga kura ya maoni kuhusu uhuru wake.

 

3 months ago

Zanzibar 24

SMZ yapiga vita tabia ya uvutaji Sigara hadharani

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib amesema Wizara ya Afya Zanzibar tayari imeweka kanuni ya kukataza kuvuta sigara kwenye mikusanyiko ya watu katika kuwanusuru waathirika wa moshi wa sigara bila ya kuwa wavutaji.

Dkt. Jamala ameeleza hayo alipokuwa akifungua warsha ya siku tatu ya kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Malindi iliyowashirikisha wadau kutoka taasisi mbali mbali za Serikali.

Mkurugenzi Mkuu alisema...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani