6 months ago

Michuzi

AZAM KUMPELEKA MBARAKA YUSUPH AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU


MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mbaraka Yusuph, anatarajia kuondoka nchini kesho Jumatano jioni kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa uchunguzi wa goti lake la kushoto baada ya kuumiza ‘meniscus’ (washa).


Yusuph alipata majeraha hayo akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wakati ikicheza na Libya kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Chalenji ulifanyika nchini Kenya Desemba 3 mwaka huu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo,...

 

8 months ago

Malunde

OFISI ZA YUSUPH MANJI ZAFUNGWA KWA DENI LA MILIONI 300

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji ameendelea kuingia matatani baada ya Kampuni ya Udalali ya Yono kuzifunga ofisi zake zilizopo Barabara ya Pugu.

Yono wamezifunga ofisi na maghala ya Manji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga akituhumiwa kudaiwa kodi ya zaidi ya Sh300 milioni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Yono, Scholastika Kevela jana Ijumaa alisema, ‘’ni kweli tumezifunga ofisi za Manji zilizopo eneo la Pugu, anadaiwa fedha nyingi za kodi...

 

9 months ago

Malunde

HUKUMU YA YUSUPH MANJI KESI YA DAWA ZA KULEVYA OCTOBER 6,2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu kesi ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji, October 6, 2017 baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake wa mashahidi saba.

Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Manji, Hajra Mungula kumueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba wamefunga ushahidi wao wa mashahidi saba ambapo baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha amesema kutokana na kufungwa ushahidi huo anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, October 6, 2017.

Awali,...

 

9 months ago

Malunde

YUSUPH MANJI ANYANG'ANYWA SHAMBA NA SERIKALI

Serikali imelifuta shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji, lenye ukubwa wa eka 714.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amesema shamba lingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa.

Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa watashitakiwa.

"Muyaache...

 

9 months ago

Malunde

JENGO LA OFISI ZA MAWAKILI WA YUSUPH MANJI ZAVAMIWA NA WATU WASIOJULIKANA

Watu wanane wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wamevamia jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza na kufanya uharibifu wa mali za wapangaji.
Jengo la Prime House lina ghorofa tano lipo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala jijini Dar es salaam.
Mwandishi ameshuhudia barabara ya kuingia eneo hilo ikifungwa kwa muda na polisi ambao walitumia magari yao kuziba njia na kuweka uzio wa utepe wa rangi ya njano.
Jengo la Prime House lina ofisi za kampuni...

 

10 months ago

Malunde

YUSUPH MANJI AGOMA KUTUMBULIWA UDIWANI CCM

Mfanyabiashara Yusuf Manji ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo September 9, 2017 kuwa yeye bado ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu na kudai kuwa hatambui kuvuliwa udiwani kama ilivyotangazwa na Mstahiki Meya wa Temeke, Abdallah Chaulembo September 6, 2017.

Manji ametoa malalamiko hayo, kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili na wenzake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo katika kesi hiyo ambayo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai upelelezi...

 

10 months ago

Malunde

Breaking News: YUSUPH MANJI ATUMBULIWA UDIWANI WAKE


Mfanyabiashara Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.


Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema hayo leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari.

Kutokana na hilo wamemuondoa Manji kwenye nafasi hiyo kutokana na kukosa sifa

 

10 months ago

Malunde

PROFESA WA JKCI: MOYO WA YUSUPH MANJI UMEWEKWA VYUMA ILI KUMSAIDIA KUPUMUA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohammed Janab ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 30, 2017 kuwa moyo wa Mfanyabiashara Yusuf Manji umewekwa vyuma ili kumsaidia kupumua.

Prof. Janab ambaye ni Daktari wa moyo na Shahidi wa kwanza upande wa utetezi ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Manji ambapo akiongozwa na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula,...

 

10 months ago

Channelten

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemkuta Mfanyabishara Yusuph Manji na kesi ya kujibu

1

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemkuta Mfanyabishara Yusuph Manji na kesi ya kujibu kuhusu tuhuma za kutumia Dawa za kulevya aina ya Heroin. Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi mfawidhi Cyprian Mkeha mapema leo.

Hakimu Mkeha amesema ameridhika na ushahidi wa upande wa Jamhuri na kwamba mshitakiwa ana haki ya kujitetea kutokana na mkojo wake kukutwa dawa aina ya Morphine ambayo zao lake ni Heroin

Baada ya kuelezwa hayo Wakili wa Utetezi Hudson Ndusyepo alidai kuwa...

 

10 months ago

Malunde

MAHAKAMA: YUSUPH MANJI ANA KESI YA KUJIBU KUHUSU KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 25, 2017 imesema Mfanyabiashara Yusuf Manji ana kesi ya kujibu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha, wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Hakimu Mkeha alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na kwamba mshtakiwa ana haki ya kujitetea kutokana na mkojo wake kukutwa na dawa aina ya Morphine ambayo zao lake ni...

 

11 months ago

Malunde

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAOMBI YA DHAMANA YA YUSUPH MANJI


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Leo imeyatupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na   Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji baada ya kukubaliana na mapingamizi yaliyowasilishwa na DPP.

Maombi hayo yametupiliwa mbali na Jaji Isaya Arufani.
Kabla ya kutupiliwa mbali, maombi hayo, Manji alisimama na kuieleza mahakama kukataa kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa sababu za kisiasa.
Amedai, alipopeleka maombi ya dhamana alimpa maelekezo wakili Joseph Tedayo lakini...

 

12 months ago

Malunde

MFANYABIASHARA YUSUPH MANJI ASOMEWA MASHTAKA AKIWA AMELAZWA HOSPITALI

Mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake watatu jana wamesomewa mashtaka saba katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako mahakama ilihamia jana kwa muda.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhamia hospitalini hapo, alikolazwa Manji.

Manji (41) na wenzake, wanadaiwa kukutwa na vitambaa vyenye thamani ya Sh200 milioni, vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Pia, wanadaiwa kukutwa na...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani