(Today) 14 minutes ago

Dewji Blog

Zantel yatoa msaada wa vitabu 152 kwa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Zanzibar

Kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL imekabidhi  msaada wa vitabu vyenye thamani ya Tsh. milioni 10 kwa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, kilichopo Unguga, Zanzibar  kwa  lengo la kuboresha elimu Visiwani humo.

Msaada huo umekabidhiwa na Mwenyekiti wa Zantel, Bi. Rachel Samren kwa Mkurugenzi wa chuo hicho cha  Karume cha Sayansi na Ufundi, Bw.  Haji Abdulhamid, tukio lililofanyika chuoni hapo huku likishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali...

 

(Today) 2 hours ago

Zanzibar 24

Msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja na Pemba

Msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja na Pemba. Jumla ya mabao 563 yamefungwa kupitia michezo 261 iliyo chezwa katka viwanja na Pemba na kwa upande wa Unguja jumla mabao 563 yamefungwa kupitia michezo 243 ambayo imesha chezwa.

 

 

The post Msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja na Pemba appeared first on Zanzibar24.

 

(Today) 2 hours ago

Michuzi

ZANTEL YATOA MSAADA WA VITABU 152 KWA CHUO CHA KARUME CHA SAYANSI NA UFUNDI CHA UNGUJA,ZANZIBAR

Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji Abdulhamid (kushoto) akifurahia msaada wa vitabu vyenye thamani ya Tsh. milioni 10 vilivyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa shule yake jana kisiwani Unguja, Zanzibar. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin na kulia ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa.Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren akikabidhi vitabu vyenye thamani ya Tsh. milioni 10 kwa Mkurugenzi wa chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji...

 

(Today) 4 hours ago

Zanzibar 24

Palestina yatiliana saini na wizara ya afya Zanzibar makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya afya

Wizara ya Afya imetiliana saini na Jamhuri ya watu wa Palestina makubaliano mapya ya mashirikiano ya miaka mitano ambapo Palestina itaipatia Wizara msaada wa mafunzo kwa madaktari na wafanyakazi wa kada nyengine.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alitia saini kwa niaba ya Wizara na Palestina iliwakilishwa na Balozi wa Nchi hiyo Tanzania Hazem Shabat.

Akizungumza katika shehere hiyo iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Waziri wa Afya alisema kupitia mashirikiano hayo mapya Palestina...

 

(Yesterday)

Dewji Blog

Nchi ya Palestina na Zanzibar watiliana saini ushirikiano katika sekta ya Afya

Wizara ya Afya imetiliana saini na Jamhuri ya watu wa Palestina makubaliano mapya ya mashirikiano ya miaka mitano ambapo Palestina itaipatia Wizara msaada wa mafunzo kwa madaktari na wafanyakazi wa kada nyengine.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alitia saini kwa niaba ya Wizara na Palestina iliwakilishwa na Balozi wa Nchi hiyo Tanzania Hazem Shabat.

Akizungumza katika shehere hiyo iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Waziri wa Afya alisema kupitia mashirikiano hayo mapya Palestina...

 

(Yesterday)

Mwananchi

Wagonjwa 500 wapasuliwa vichwa Zanzibar

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema visiwa hivyo vimepata mafanikio katika sekta ya afya baada ya kufanikiwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa 500 wa maradhi ya kichwa na uti wa mgongo.

 

(Yesterday)

Zanzibar 24

Maradhi ya Vichwa maji, Uti wa mgongo na kensa ya ubongo sasa yatibika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imesema uwepo wa kitengo cha kutibu magonjwa sugu katika Hospitali ya Mnazi mmoja  itaweza kusaidia wananchi kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa pamoja na matibabu ya  maradhi mbalimbali ikiwemo   Vichwa maji, Uti wa mgongo  na Mishipa ya fahamu na kensa ya ubongo .

Akizungumza na Waandishi wa habari nje ya kongamano la Madaktari kutoka nchi mbalimbali wakiwemo wazanzibar amesema kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakisafirisha wagonjwa wao kwaajili ya...

 

2 days ago

Michuzi

RAIS WA ZANZIBAR AONGEA NA WALIMU WAKUU WA SKULI ZA SEKONDARI UNGUJA LEO

 Baadhi ya Walimu wa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Mkutano na Walimu wa Skuli za Sekondari za Mikoa mitatu ya Unguja,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja Baadhi ya Walimu wa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Mkutano na Walimu wa Skuli za Sekondari za...

 

2 days ago

Zanzibar 24

Zanzibar yawa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya ubongo na uti wa mgongo

Zanzibar itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la maradhi ya vichwa maji na uti wa mgongo na kensa ya ubongo litakalofanyika kwa siku tatu kuanzia kesho katika kituo cha maradhi hayo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha upasuaji wa maradhi hayo NED, Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alisema nchi tisa kutoka Afrika, Ulaya na Marekani zitashiriki Kongamano hilo.

Amesema Zanzibar imepewa nafasi hiyo kutokana na juhudi za Rais Shein katika...

 

3 days ago

Michuzi

Rais wa Zanzibar Dkt Shein akutana na Madaktari Bingwa wa Upasuaji Kichwa na Uti wa Mgongo

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu inayohusiana na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu,Uti wa Mgomgo na Vichwa maji  Dr.Hosea Piquer akiongoza Ujumbe wa Wataalamu   wa Upasuaji wa Kichwa na Uti wa mgongo   walipofika Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo na RaisRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Wataalamu   wa Upasuaji wa Kichwa na Uti wa...

 

3 days ago

Zanzibar 24

Wachezaji waliogoma kujiunga na timu ya taifa ya wanawake Zanzibar Queens wasamehewa na ZFA

Wachezaji watano (5) wa timu ya New Generation Queens ya Kwahani waliogoma kujiunga na timu ya taifa ya Zanzibar Wanawake  “Zanzibar Queens”  wamesamehewa na sasa wapo huru kucheza ligi mbali mbali za vilabu pamoja na timu ya Taifa ya Zanzibar.

Wachezaji hao waligoma kwenda kushiriki Mashindano ya CECAFA Women championship yalofanyika JINJA nchini Uganda kuanzia September 11-20 mwaka jana (2016) ambapo Zanzibar walifungwa michezo yote mitatu na kufikisha idadi ya kufungwa mabao 30-1.

Kamati...

 

4 days ago

Zanzibar 24

Mabadiliko: Ligi kuu ya soka Zanzibar msimu ujao timu 12 tu

Ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2017-2018 yani msimu ujao inatakiwa kuchezwa kwa vilabu 12 tu kwa Zanzibar nzima na mfumo wa kuchezwa kanda mbili tofauti yani kanda ya Pemba na kanda ya Unguja umefikia tamati msimu huu.

 

Kwa mujibu wa Makamu wa Urais wa ZFA Pemba Ali Mohammed amesema baada ya kupatiwa uanachama wa kudumu kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika wametakiwa kupunguza timu na kubakiwa na timu 12 tu kwa msimu ujao.

 

Wadau wengi wa soka Visiwani Zanzibar wanahamu ya...

 

4 days ago

Zanzibar 24

Mambo 2 yaliofanya Zanzibar kuwemo kwenye kumbukumbu za Dunia za Guiness

Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania iliyoundwa baada ya Muungano wa tarehe 26 April, 1964.

Tumetembelea orodha ya rekodi mbalimbali katika rekodi za Guiness na hapa tunakuletea mambo mawili ambayo yameifanya Zanzibar kuwemo katika kumbukumbu za Guiness:

 Jambo la kwanza linaloifanya Zanzibar kuwemo kwenye rekodi za Guiness ni vita iliyopiganwa tarehe 27 August 1896 kati ya Uingereza na Zanzibar. Vita hii ilipiganwa kati ya dakika 38 na 45 na inashikilia rekodi ya kuwa ndiyo...

 

4 days ago

Zanzibar 24

Kampuni ya Garware yaonesha nia ya Kujenga Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Zanzibar

Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa  miundombinu ya Ujenzi ya Garware yenye Makao Makuu yake Mjini Bombay Nchini India imeonyesha nia yake ya kutaka kujenga Ukumbi Mpya wa Kisasa wa Kimataifa wa Mikutano Zanzibar endapo itapata fursa ya kufanya kazi hiyo.
Uwamuzi huo umekuja kufuatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na mpango wa Kutaka kujenga Ukumbi wenye hadhi hiyo katika azma yake ya kuimarisha Sekta ya Utalii inayoonekana kuimarika na kuleta ufanisi mkubwa.
Mkurugenzi Miradi wa...

 

5 days ago

Zanzibar 24

RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amezindua mashindano ya Mpira wa miguu ‘Majimbo Cup’

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amezindua mashindano ya Mpira wa miguu ‘Majimbo Cup’ na kuwataka vijana wanaoshiriki mashindano hayo kucheza kwa maadili na nidhamu kama kilivyo chama chao cha CCM.t

Uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ikiwa ni maadhimisho ya mwaka mmoja tokea kuapishwa kwa Dk. Shein kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kufuatia ushindi wa kishindo alioupata katika uchaguzi mkuu...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani