5 days ago

Malunde

Zitto Aiomba Serikali Kuingilia Kati Dhidi Ya Vijana Wanaojipaka Oil Chafu Na Kubaka Wanawake.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe ameiomba Serikali kuingilia kati dhidi ya baadhi ya vijana  wanaokuwa wakijipaka Oil Chafu na kuvamia wanawake  na kuwabaka   jambo ambalo ni Udhalilishaji wa kijinsia . 
Zitto ametoa ombi hilo leo Mei 21,2019  mbungeni jijini Dodoma wakati  akiwasilisha hoja ya dharura ambapo amesema suala la baadhi ya vijana kujipaka oil chafu na kuvamia wanawake  na kuwabaka limekuwa likijitokeza mara kwa mara jimboni kwake ambapo...

 

1 week ago

MwanaHALISI

Shahidi wa Jamhuri: Nyaraka hizi alisaini Zitto

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeendelea kusikiliza kesi Na. 237/2018 ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).  Leo tarehe 17 Mei, 2019, shahidi wa nne upande wa Jamhari ameelezwa kuwa ni Inspekta Salum Seif Masoud, mpelelezi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa ...

 

1 week ago

MwanaHALISI

Shahidi kesi ya Zitto amtaja Lissu

SHAHIDI wa tatu, Shabani Hamis (40) kwenye kesi  Na. 327/2018 ya uchochezi inayomkabili Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameieleza mahakama kwamba, tukio la kushambuliwa Tundu Lissu limefanya azidi kulichukia Jeshi la Polisi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Lissu ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alishambulia ...

 

1 week ago

Michuzi

USHAHIDI KESI YA ZITTO KABWE WAENDELEA KUTOLEWA


Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
SHAHIDI wa pili katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa analichukia jeshi la polisi kuanzia siku alipoona video  kwenye mtandao wa kijamii wa you tube ikimuonyesha Zitto Kabwe  akielezea polisi wanavyowatendea ukatili raia.

Shahidi huyo Mashaka Juma ambaye ni msanii wa filamu, akiongozwa na Wakili wa serikali Mkuu Tumaini Kweka kutoa ushahidi wake, amedai, Oktoba 29,2018 huko...

 

2 weeks ago

MwanaHALISI

Freeman Mbowe, Zitto Kabwe kuiteka Kisutu wiki nzima

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu itaendelea na usikilizaji wa kesi  za uchochezi zinazowakabili viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo, wiki nzima mfululizo. Anaandika Faki Sosi …(endelea) Mahakama hiyo itaendelea na usikilizaji wa kesi hizo kuanzia Jumatatu ya tarehe 13 hadi Ijumaa tarehe 17 Mei 2019. Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi ...

 

3 weeks ago

MwanaHALISI

Zitto, Nape, Polepole wafika na ujumbe msibani kwa Dk. Mengi

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, wamekutana nyumbani kwa Marehemu Dk. Reginald Abraham Mengi na kutoa salamu za rambirambi za vyama vyao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). Kwenye msiba huo Polepole amesema, CCM na Tanzania kwa ujumla itaukumbuka mchango wa Dk. Mengi kupitia uwekezaji wake mkubwa alioufanya ...

 

4 weeks ago

MwanaHALISI

Mei Mosi Zitto ang’aka

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo amepinga sababu zilizotolewa na Rais John Magufuli za kutopandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa miaka minne mfululizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Akizungumza leo tarehe 1 Mei 2019, jijini Dar es Saalam, Zitto amesema Serikali zote zilizopita zilifanya miradi ya maendeleo sambamba na kupandisha mishahara ya Wafanyakazi. ...

 

1 month ago

Malunde

Spika Ndugai Kasema Zitto Kabwe Ni Muongo

Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini,Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi.
Ndugai alisema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.
Alisema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.
Spika Ndugai aliyasema hayo bungeni leo mchana muda...

 

5 months ago

Malunde

ZITTO KABWE AANIKA ORODHA YA VITABU 49 ALIVYOSOMA MWAKA 2018

Tangu Mwaka 2012 nimekuwa naorodhesha vitabu nilivyosoma katika mwaka. Si vitabu vyote huviweka hapa kwani vingine huwa nasoma na kuviacha njiani ama kutopendezwa navyo au kwa kusahau tu. 


Vitabu vingine huwa vitabu rejea na huvirudia kwa ajili ya mafunzo ili kufanya maamuzi Fulani Fulani au kwa ajili ya ibada (kwa mfano Quran) au kwa sababu nyenginezo. Nafurahi kuwa hivi sasa kwenye mitandao duniani kote watu wamekuwa wakiorodhesha vitabu ili kujengana katika utamaduni wa kusoma. Barack...

 

12 months ago

Zanzibar 24

Humphrey Polepole ashangazwa na Zitto Kabwe na Mbowe

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Ndg. Humphrey Polepole amewasikitikia Viongozi wa vyama vya Upinzani nchini, Mbowe pamoja na Zitto Kabwe baada ya kukubaliana kushirikiana kumpata Mbunge jimbo la Buyungu lililoachwa wazi na Mwl. Kasuku Bilago ambaye amefariki dunia, kwa kuwaambia wembe wa CCM ni ule ule.

Polepole amesema hayo ikiwa zimepita siku kadhaa baada ya mazishi ya Mwl. Kasuku Bilago kuzikwa huko Kakonko mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mfupi na kisha kwenda...

 

12 months ago

Malunde

ZITTO KABWE AUNGANA NA CHADEMA

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ametangaza nia ya kushirikiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Aikael Mbowe katika kupigania jimbo la Buyungu lililoachwa na Marehemu Mwalimu Kasuku Bilago.
Kupitia mtandao wake Zitto ameyaweka wazi hayo ambapo amesema kuwa kwa heshima ya Mwalimu Bilago yeye na Mbowe wamekubaliana kuwa watashawishi kuwepo na a Democratic Front Katika Jimbo la Buyungu. 
"ACT Wazalendo itaunga mkono mgombea wa CHADEMA au CHADEMA itaunga mkono mgombea...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani