166 watiwa mbaroni kwa kutumia ovyo mitandao

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu zaidi ya 166, ambao wanatuhumiwa kutumia mitandao ya kijamii kutangaza matokeo yasiyo rasmi. Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova alisema jana kuwa watu hao walikamatwa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Malunde

ASKARI POLISI WANNE WALEVI WATIWA MBARONI KWA KUFYATUA OVYO RISASI NA KUJERUHI MTU MWANZA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ahmed Msangi ametoa amri kukamatwa kwa askari polisi wanne wa Kituo Kikuu cha Polisi Nyamagana kutokana na asakri hao kumjeruhi kwa risasi mke wa Mwenyekiti mtaa.
Kamanda Msangi amesema polisi hao tayari wametiwa mbaroni kwa kumjeruhi kwa risasi mguuni Bi. Editha Ntobi ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Majengo Mapya uliopo katika Kata ya Mabatini jijini Mwanza.
Msangi amesema polisi hao wanatuhumiwa...

 

5 years ago

Mwananchi

Wawili watiwa mbaroni kwa ‘unga’

Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), kimewakamata mkazi wa Ilala na raia wa Nigeria, kwa tuhuma za kukutwa na begi lenye kilo 4.8 za dawa zinazodhaniwa kuwa ni za kulevya.

 

1 year ago

Zanzibar 24

14 watiwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Watu 14 washikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa tuhuma za mauaji, wizi pamoja na kukutwa na noti bandia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa watuhumiwa 10 kati ya hao wanaoshikiliwa wanatuhumiwa kwa kosa la mauaji, watatu kwa tuhuma za wizi na mmoja kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia.

Kwa mujibu wa Kamanda Mtafungwa amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako ulifanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa huo na kubaini watuhumiwa hao wakiwemo...

 

4 years ago

Habarileo

Watano watiwa mbaroni kwa upigaji ramli

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi MwombejiWATU watano wa kijiji cha Mheza kilichopo Kata ya Mhinduro wilayani Mkinga wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa wakipiga ramli za uchonganishi zilizolenga kufichua wachawi.

 

3 years ago

Mwananchi

100 watiwa mbaroni kwa kuchoma ofisi ya Serikali

Kundi la wananchi leo lilivamia ofisi ya Serikali ya kata ya Njoro,Manispaa ya Moshi, na kuichoma moto wakipinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea udiwani wa Chadema, Jomba Koyi.

 

5 years ago

Michuzi

23 WATIWA MBARONI KWA KUKUTWA NA BANGI MKOANI PWANI

JESHI LA POLISI MKOANI PWANI,LINAWASHIKILIA VIJANA 23 WALIOKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA KETE 354 ZA BANGI,PUNI 4,MISOKOTO 8 PAMOJA NA PANGA 1,VISU VINNE NA SIME 3,IKIWA NI KATIKA SEHEMU YA UPEKUZI WA  MAGARI YATOKAYO DAR ES SALAAM AMBAPO KATIKA UPEKUZI HUO WATUHUMIWA HAO WALIPATIKANA.
KATI YA WATUHUMIWA HAO 7 WAMESHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUPATIKANA NA MAKOSA WALIYOKUTWA NAYO NA WENGINE WALIACHIWA BAADA YA KUPATIKANA NA MAKOSAJI HALISI.
KIASI HICHO CHA BANGI KINGEINGIA MWALONI KINGELETA...

 

3 years ago

Mwananchi

Mstaafu wa JWTZ, mwanae watiwa mbaroni kwa ujangili

Polisi Kanda Maalumu ya Tarime, inawashikilia watuhumiwa watano akiwamo mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na mwanae kwa tuhuma za kukutwa na nyara za Serikali.

 

3 years ago

Dewji Blog

Watu wanne watiwa mbaroni kwa tuhuma za ujambazi

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupitia kikosi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha limekamata watu wanne kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Hezron Gymbi amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana maeneo ya Chamanzi muda mfupi baada ya kukutana na kupanga kufanya uhalifu wa kutumia silaha.

Watuhumiwa hao wanaofahamika kwa majina ya Uswege Seleman (23), Hassan...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani