Agnes Masogange kukamatwa kwa amri ya Mahakama

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa hati ya kukamatwa Msanii Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange (28), baada ya kushindwa kufika mahakamani mara kwa mara ya pili kesi yake ilipopangwa kutajwa.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Wilbroad Mashauri ametoa amri hiyo baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa lakini mshtakiwa, wadhamini na wakili wa utetezi wote hawakuwepo mahakamani.

Wakili wa Serikali Adolf Nkini alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa lakini kwa sababu mshtakiwa na wadhamini wake hawakuwepo mahakamani kwa mara ya pili, aliomba hati ya kukamatwa mshtakiwa.

Hakimu alisema kwa sababu mara mbili mfululizo mshtakiwa ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake bila taarifa mahakama yake inatoa hati ya kukamatwa kwake.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!Share on Whatsapp

Bongo5

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Malunde

MAHAKAMA YATOA AMRI YA MSANII AGNES MASOGANGE AKAMATWE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili.

Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya...

 

1 year ago

Michuzi

KAMANDA SIRRO ATHIBITISHA KUKAMATWA KWA AGNES MASOGANGE, KUHOJIWA ZAIDI KUFUTIA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Video Queen Agnes Masogange anayeshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya Dawa za Kulevya.

 

1 year ago

Bongo5

Mahakama yatoa amri kukamatwa kwa Tundu Lissu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kukamatwa kwa mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu na kuamuru wadhamini wake kufika mahakamani hapo.

lissu

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Thomas Simba baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi yake ilipangwa kusikilizwa Alhamisi hii lakini Lissu hakuwepo mahakamani hapo.

Alijitokeza mdhamini wake mmoja kati ya wawili, Robert Katula na kudai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi wa mahakama kuu Tanzania kanda ya ziwa.

Hakimu alimhoji...

 

9 months ago

Michuzi

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YASHINDWA KUSIKILIZA KESI YA AGNES MASOGANGE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu imekwama kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili video Queen, Agnes Gerald 'Masogange' kwa sababu ana tatizo la kiafya.

Hayo yameelezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya wakili wa serikali, Costantine Kakula kueleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Hata hivyo, wakili wa Masogane, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi...

 

1 year ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZ...: MAHAKAMA YATOA AMRI YA KUKAMATWA MBUNGE TUNDU LISSU KWA KUSHINDWA KUSIKILIZA KESI YAKE

Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imetoa amri ya  kukamatwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kuamuru wadhamini wake kufika mahakamani hapo kujieleza kwanini wasilipe fungu la dhamana kutokana na mshtakiwa huyo kushindwa kufika kusikiliza kesi yake bila ruhusa.
Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio.
Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa...

 

1 year ago

Bongo5

Agnes Masogange apandishwa kizimbani, aachiwa kwa dhamana

Video queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepandishwa kizimbani Jumatano hii katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya.

Mrembo huyo ambaye ni maarufu kwa kupamba video za muziki wa wasanii wa bongo fleva, amekana tuhuma hizo na kesi yake kuahirishwa hadi Machi 21 mwaka huu.

Katika mashtaka yake mawili yaliyosomwa na mwendesha mashtaka Mashauri Wilboard chini ya wakili wa serikali Constatine Kokulwa, Agnes anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina...

 

2 years ago

Bongo5

Exclusive: Babutale aeleza yake kuhusiana na amri ya mahakama ya kukamatwa na kumlipa sheikh milioni 250

Meneja wa Tip Top Connection na wa Diamond Platnumz, Babutale anakabiliwa na mtihani mzito baada ya mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kutoa hati ya kukamatwa kutokana na kudaiwa kutotii amri iliyomtaka amlipe Shekh Hamis Mbonde, shilingi milioni 250.

13525399_932827003529799_1639302313_n

Kwa mujibu wa habari iliyoandiwa na gazeti la Mwanahalisi Jumanne hii, Tale anatakiwa alipe kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kudaiwa kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya...

 

2 years ago

Bongo5

Agnes Masogange ana ujauzito wa Davido?

masogange4

Kama ni ‘kiki’ basi imefanikiwa, kwa sababu hadi mitandao ya Nigeria imeripoti kuwa kuna uwezekano Agnes Masogange akawa na ujauzito wa staa wa Naija, Davido.

masogange4

Agnes na Davido wameonekana kuwa karibu siku za hivi karibuni, baada ya kuwa wanapost picha tofauti tofauti wakiwa wanakula bata pamoja kama couple.

maso david

Mtandao wa Pulse wa Nigeria umeandika kuwa kuna uwezekano malkia huyo wa ‘shepu’ Bongo, Agnes akawa na ujauzito wa Davido baada ya kupost picha ya kipimo cha mimba kinachoonesha...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani