Airtel yazindua duka la kisasa Babati Mkoani Manyara

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka la Airtel mkoa wa Manyara. wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa Airtel. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe akiongea mara baada ya kuzindua duka la Airtel Mkoani Manyara akishuhudia Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara Peter Kimaro. Afisa wa kitengo cha huduma kwa wateja wa dula la Airtel Manyara Bi Ramla Rajabu akimuonyesha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe baadhi ya simu zinazopatikana katika duka jipya lililopo Babati mjini mara baada ya kuzinduliwa kwa duka hilo jipya litakalotoa huduma kwa wateja na wakazi wa mkoa wa Manyara. Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imezindua duka mjini Babati kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wanaoishi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara ikiwa ni mwendelezo wa mpango wake wa kufungua maduka ya kutoa huduma kwa wateja wake nchi nzima.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara,Fransic Masawe,ndiye aliyezindua duka hilo ambaye amesema litasadiai kutoa huduma kwa wakati lakini pia lisaidia kutoa ajira kwa vijana na kuwawezesha wakulima wa mazao ya  kupata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi
 “ nawapongeza Airtel kwa kusogeza huduma karibu na wateja  na kuongeza kuwa duka hilo litakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mji wa Babati  pamoja na maeneo jirani. Napenda kuchukua fursa hii kuwa kuwaasa wakazi wa hapa hususani vijana kuchangamkia fursa za ajira zilizopo kupitia duka hilo ajira kwa lengo lakujiongezea kipato”. Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Fransic Masawe
 Kwa Upande wake Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara,Peter Kimaro,amesema duka hilo linalenga kusogeza huduma karibu na jamii kwani kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wanapata tabu kupata huduma za uhakika lakini pia hatua hiyo inatoa mwanya wakuongeza maduka mengine mengi katika maeneo ya mkoa huo ikiwemo wilaya  ya Katesh
Pia amesema huduma ya mawasiliano ni chachu ya maendeleo kwani inasaidia uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kuwawezesha huduma za kifedha kupatikana kirahisi ambapo kwa sasa watu wengi hutumia Airtel Money kufanya miamala pamoja na kupata mikopo kupitia huduma ya Airtel Timiza ambayo imekuwa ni mkombozi kwa wajasiriamali wadogo wadogo kupata mitaji ya kuendesha biashara zao.
Tunatoa wito kwa wateja wetu kutembelea maduka haya ambayo tunayafungua nchi nzima ili kupata huduma hapa manyara tayari tunayo maduka matatu ambayo moja tunalizindua hapa na mengine mawili yapo katika maeno ya Dareda center na Riloda .aliongeza Kimaro

Baadhi ya wananchi wamesema kufunguliwa kwa duka hilo kutaongeza ajira kwa vijana pamoja na kutoa huduma za uhakika za miamala ya fedha na mawasiliano kwa ujumla tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wanalazimika kufuata huduma umbali mrefu kidogo
Kampuni ya Airtel inampango wakuongeza maduka mengine katika mkoa huo wa Manyara ili kuendelea kusogeza huduma zake kwa wateja kwa urahisi hususani katika maeneo ya vijijini.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Mwananchi

Airtel yazindua Duka la kisasa Dar

Kampuni ya Airtel imekarabati duka lake lililopo Mlimani City na tayari imelizindua likiwa na mwonekano wa kisasa.

 

4 years ago

Michuzi

Airtel yazindua duka la kisasa Mlimani City

Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua rasmi duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia, wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania. Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia, wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa...

 

4 years ago

GPL

AIRTEL YAZINDUA DUKA LA KISASA MLIMANI CITY‏

Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa, Christophe Soulet akikata utepe kuzindua duka la Airtel  lililopo Mlimani City  jijini Dar es Saalam. Wakishuhidia, wa pili ni Andre Beyers Afisa Mkuu wa Masoko Airtel Afrika akiwa na Meneja wa Duka, Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania.
Duka la…

 

2 years ago

Global Publishers

Airtel yazindua Duka la kisasa jijini Dar es Saalam‏

pic 1Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(wakwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja Bi. Zakia Omarypic 2

 

3 years ago

Michuzi

AIRTEL YAZINDUA DUKA MKOANI TANGA

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (katikati), akikata utepe kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini Tanga jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba na (kulia kwake) ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Duka hilo, Mwanavita Chiya.  Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula (kushoto), kuhusu bidhaa mbalimbali zinazouzwa...

 

2 years ago

Michuzi

BENKI YA POSTA TANZANIA, TPB, YAZINDUA HUDUMA ZA KIFEDHA TAWI LAKE LA BABATI MKOANI MANYARA

Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akikata tepe kikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za kifedha kwenye tawi la Benki ya Posta Babati mkoani Manyara leo Februari 9, 2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB, Profesa Lettice RutashobyaMsajili wa hazina, Lawrence Mafuru (wapili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta tawi la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi...

 

4 years ago

Michuzi

Airtel yazindua Mnara wa Mawasiliano Mbulu Mkoani Manyara


 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri akikata  utepe wakati wa uzinduzi wa Mnara wa  huduma za Mawasiliano  katika kijiji cha Aicho wilayani Mbulu Mkoani Manyara ambapo sasa wakazi wa kijiji hicho na jijini vya jirani wameunganishwa na huduma za simu za  mkononi za Airtel. Akishuhudia ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala   pamoja na wakazi wa Kijiji  hichoMeneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala  akiwa na Kaimu Mkurugenzi...

 

4 years ago

Michuzi

Airtel yafungua duka la kisasa Mwanza

 Mrakibu mwandamizi wa polisi  mkoa wa Mwanza SSP  Christopher Cyprian Fuime,  akikata utepe kuzindua duka la Airtel Mwanza mara baada ya matengenezo na kulifanya duka hilo kuwa la kisasa, pembeni yake ni Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba akiwa pamoja na wafanyakazi wa Airtel Mwanza. Uzinduzi huu umefanyika mwisho mwa wiki hii
 Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kulia) akimwonyesha mgeni rasmi Mrakibu mwandamizi wa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani