AJALI KIVUKO CHA FERI: Gari Latumbukia Baharini Likiwa Na Watu Wawili, Maiti Zaopolewa Baadaye

Watu wawili wamefariki dunia usiku wa kuamkia Aprili 20 baada ya gari aina ya Hiace walilokuwa wamepanda kuserereka na kutumbukia katika Bahari ya HINDI.

HIACE hiyo ambayo namba zake hazikufahamika mara moja , ilipata kadhia hiyo wakati ikiwa tayari imeegesha ndani ya Kivuko cha Mv. Kigamboni  kwa lengo la kuvuka kwenda Kigamboni.

AJALI KIVUKO CHA FERI

Ni siku moja tu  baada ya Rais Dakta John Magufuli kuzindua daraja linalounganisha maeneo ya Kigamboni, Feri na Kurasini ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu kutatua kero ya usafiri utokanao na Vivuko.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Brown Mwakalago, ndugu hao walitoka nyumbani kwao Mkoani Mbeya kwenye msiba wa kaka yao kuja kumalizia matanga kwake Vijibweni Kigamboni.

AJALI KIVUKO CHA FERI

AJALI KIVUKO CHA FERI

Mpaka Star Tv inaondoka katika eneo la Feri Kigamboni, waokoaji hao walikuwa wamefanikiwa kuiopoa miili yote miwili huku juhudi za kulitoa gari hilo ikionekana kuwa na ugumu kutokana na umbali wa kina cha bahari ambapo gari hilo limezama.

StarTV

Read more


Habari Zinazoendana

9 months ago

Malunde

GARI LATUMBUKIA MTO WAMI NA KUUA WATU WAWILI


Picha hii ya mtandao inaonyesha moja ya ajali zilizowahi kutokea katika mto huo.

MADEREVA wawili wa kampuni ya Usangu Logistics wamekufa baada ya gari la mizigo walilokuwa wakisafi ri nalo kutumbukia katika Mto Wami uliopo Chalinze, wilayani Bagamoyo.
Akizungumza jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jonathan Shana alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa saa 7:00 kuamkia jana. Gari aina ya Scania lenye namba za usajili T857 ARP lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Arusha lilikatika...

 

4 years ago

GPL

GARI LAKAMATWA LIKIWA LIMEBEBA MAITI YENYE DAWA ZA KULEVYA MKOANI MOROGORO

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Hizi ndio baadhi ya Pipi zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala. …

 

1 month ago

Malunde

MKURUGENZI WA TBC APATA AJALI YA GARI KIGOMA, WATU WAWILI WAFARIKINa Rhoda Ezekiel- Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji TBC Dr. Ayoub Rioba amepata ajali ya gari katika kijiji cha Mgombe kata ya Nyakitonto wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wakitokea wilayani Kibondo kuelekea mjini Kigoma.


Akizungumza leo Jumanne Machi 20,2018  mara baada ya tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi  mkoa wa Kigoma Martine Otieno amesema ajali hiyo pia imesababisha vifo vya watu wawili.
  Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili...

 

2 years ago

Channelten

Gari latumbukia Kivukoni Watu 2 wapoteza maisha, 4 wanusurika

Screen Shot 2016-04-20 at 3.46.54 PM

Watu wawili wamefariki Dunia kwa kuzama wakiwa katika gari eneo la Feri jijini dsm baada ya gari waliyokuwa wamepanda kutumbukia ghafla baharini mapema leo alfajiri.

Watu hao waliopatwa na mauti inadaiwa walikuwa wakisubiri Kivuko eneo la Fery kwa ajili ya kwenda Upande wa Pili wa Kivuko Kigamboni ambapo wakiwa watu sita kwenye gari, wanne waliteremka na kubakia mwanamke mmoja ambaye inasemakana alikuwa mgonjwa na dereva wa gari hilo.

Vikosi mbali mbali vya jeshi la wananchi JWTZ, Zimamoto,...

 

2 years ago

Global Publishers

Wawili wafariki baada ya gari kuzama baharini

1

Kikosi cha Uokoaji kikiopoa mwili wa mmoja wa watu waliokuwa kwenye gari hilo.

WATU wawili wanasadikiwa kufariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace walilokuwemo kuserereka wakati likiingia katika kivuko na kutumbukia baharini leo eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa mkuu wa kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto, tayari mwili wa mtu mmoja mwanaume umepatikana na jitihada za kusaka mwili wa mtu mwingine anayesadikika kuwa ni mwanamke zinaendelea.

2

4 years ago

Michuzi

ajali yaua watu wawili na kujeruhi wawili mkoani lindi

Na Abdulaziz Ahmed, LindiWatu wawili wamekufa na wawili kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Michenga, wilaya ya Ruangwa Ruangwa mkoani Lindi.Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alisema gari hiyo aina ya Toyota Rava4 yenye namba za usaji T574CWC.Iliyokuwa inaendeshwa na Mohamed Mchalaganya(27) iliacha njia na kupinduka katika barabara ya Ruangwa-Nanganga, ilitokea jana saa 11.30 jioni.
Kamanda Mzinga aliwataja waliokufa...

 

4 years ago

Michuzi

BASI LA SUMRY LAUA WATU 1( WAKATI WAKISITIRI MAITI ILIYOGONGWA NA GARI SINGIDA.


WATU 19 wakiwemo askari Polisi wanne wamepota maisha katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipopamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika. Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Utaho, kilometa 20 nje ya Mji wa Singida katika Barabara Kuu ya Singida Dodoma. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Geofrey Kamwela, alisema jana kuwa...

 

2 years ago

Habarileo

Gari latumbukia Kigamboni, laua 2

WATU wawili wamepoteza maisha baada ya gari waliyokuwa wamepanda iliyokuwa ndani ya Kivuko cha Mv Kigamboni cha jijini Dar es Salaam, kusererekea baharini. Watu hao waliokufa jana alfajiri ni dereva wa gari hiyo aina ya Toyota Hiace, yenye namba za usajili T 271 CRG, aliyefahamika kwa jina moja la Dani na abiria, Nice Mwakalago.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani