AJALI MBAYA YA NOAH MOROGORO

Hili ni gari la Noah lililopata ajali jana usiku wa saa 8 huko Morogoro Mtaa wa Mazimbu reli ya pili likiwa na vijana wanne ambapo mmoja wao kaaga dunia. Hii ni nguzo iliyogongwa na gari hilo mara baada ya kuhama njia.…

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Michuzi

Ajali ya gari aina ya Toyota Noah Kilombero- Mikumi mkoani Morogoro

 Wasamaria wema akiwemo Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Kituo cha ITV , Mkoa wa Morogoro, Hussein Nuha wakitoa msaada wa kusaidia mmoja wa majeruhi ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ambaye ni dereva wa gari Toyota Noah namba ya usajili T 782 DKV  inayofanya safari zake mji wa Ruaha   Kilosa - Mikumi baada ya gari hiyo kupinduka  eneo la Kijiji cha Lumango, katika  kona kali ya barabara ya Kilombero- Mikumi  katika ajali hiyo hapakutokea kifo chochote na majeruhi wote...

 

5 years ago

Michuzi

ajali mbaya eneo la Mikese, Morogoro, leo Asubuhi

 Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund
 Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea  Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto...

 

5 years ago

Habarileo

Marehemu ajali Noah wafikia 14

MTOTO wa miezi sita aliyejeruhiwa kwenye ajali ya gari dogo la abiria la Toyota Noah na lori la Scania mkoani hapa juzi, amefariki dunia na kufanya idadi ya waliokufa kufikia 14. Happiness Elisha alifariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya St Gaspar, Itigi alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

 

4 years ago

Vijimambo

Ajali ya Noah iliyoua yazua kasheshe

Watu wawili wamekufa na wanane kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Mwada na kuhusisha gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Magara kuelekea Magugu na Babati.

Aidha, ajali hiyo ilizua mvutano mkubwa baada ya wahudumu na maofisa wa kituo cha afya kugoma kupokea majeruhi wakidai wapewe fedha kwanza.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Deus Nsimeki, alitaja gari hilo kuwa ni T .728 CLV na kuwa dereva wake, Kazumba Musa aliyekimbia baada ya ajali hiyo, anatafutwa.
Alisema...

 

5 years ago

GPL

AJALI YA NOAH YAUA WAWILI MBEYA

Gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM iliyopata ajali jana maeneo ya Igurusi mkoani Mbeya. Gari hiyo ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali. GARI ndogo aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T162 BXM limepata ajali na kuua watu wawili jana eneo la Igurusi mkoani Mbeya.…

 

3 years ago

Habarileo

Ajali ya Noah, Scania yaua watu 18

AJALI za barabarani zimeendelea kukatisha uhai wa Watanzania baada ya watu 18 kufa na wengine watatu kujeruhiwa juzi usiku katika ajali iliyohusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa uso katika Kijiji cha Nsalala mkoani Shinyanga.

 

3 years ago

Habarileo

Vifo ajali ya Noah, Scania Shinyanga vyafikia 19

IDADI ya vifo katika ajali ya gari aina ya Toyota Noah na lori aina Scania iliyotokea usiku wa kuanzia juzi katika kijiji cha Nsalala, Shinyanga sasa imefikia watu 19, baada ya majeruhi Hamisa Matiko mwenye umri wa miaka mitano, naye kuaga dunia juzi usiku.

 

3 years ago

Global Publishers

Pichaz: Noah Yapata Ajali na Kuuwa Watu Rombo

AJALI ROMBO (3)Gari hilo likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali.

WATU wapatao sita wanasadikiwa kuwa wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba T568 BNZ walilokuwa wakisafiria kupata ajali mbaya katika Barabara ya Mwika – Himo eneo la Makerere wilayani Rombo.

AJALI ROMBO (4)

Gari hilo linasemekana kuwa lilikuwa likitokea Tarakea kuelekea Moshi hivyo kupata ajali ambapo mpaka sasa idadi kamili iliyothibitishwa na vyombo vya usalama kuhusu watu waliopoteza maisha kutokana...

 

1 year ago

Malunde

DIWANI WA SONGWA NGOLOMOLE AVUNJIKA BEGA AJALI YA NOAH KISHAPU

Diwani wa kata ya Songwa wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga Abdul Ngolomole (CCM)amevunjika bega la mkono wa kushoto baada ya gari aina ya Noah yenye namba za usajili T.219 CHT aliyokuwa anasafiria kuacha njia na kupinduka. 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Jumatano Aprili 4,2018, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema ajali hiyo imetokea jana saa 9 alasiri katika eneo la Mwangungulwa,kata ya Kolandoto kuelekea Kishapu. 
Amesema gari hilo likiendeshwa na...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani