ALICHOLAZIMISHWA SUGU KUFANYA AKIWA GEREZANIMbunge wa Mbeya kupitia CHADEMA Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, amesema alishangazwa na kitendo cha kusikia imepigwa simu kutoka juu, na kueleza kwamba ni lazima yeye na Masonga wavae sare za jela  Akizungumzia suala hilo Sugu amesema kwamba kitendo hicho kilimshangaza kwani kulikuwa kuna watu wengine wengi walikuwa hawana sare na wamefungwa mule muda...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

11 months ago

Zanzibar 24

Sugu atoboa siri alicholazimishwa kufanya akiwa gerezani

Mbunge wa Mbeya kupitia CHADEMA Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu‘, amesema alishangazwa na kitendo cha kusikia imepigwa simu kutoka juu, na kueleza kwamba ni lazima yeye na Masonga wavae sare za jela.

Akizungumzia suala hilo Sugu amesema kwamba kitendo hicho kilimshangaza kwani kulikuwa kuna watu wengine wengi walikuwa hawana sare na wamefungwa mule muda mrefu lakini walikosa sare, hivyo kitendo cha kulazimishwa yeye ambaye yuko kwa muda mfupi kilikuwa...

 

11 months ago

Zanzibar 24

Sugu ashangazwa kutoka gerezani

Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ambaye ameachiwa huru leo may 10, 2018 kutoka gerezani alikofungwa akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela.

Akizungumza na East Africa Radio, Sugu amesema hakuwa anajua kama anaachiwa mpaka pale alipofuatwa na polisi kuambiwa ajiandae, na hajui imekuwaje mpaka akaachiwa sasa kwani ilijulikana ataachiwa huru mwezi wa 6.

“Watu wote walikuwa wanatarajia...

 

11 months ago

Malunde

MBUNGE SUGU NA MWENZAKE WATOKA GEREZANI

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru leo Alhamis Mei 10,2018 jijini Mbeya

 

11 months ago

Malunde

MBOWE ASHANGAA SUGU KUTOKA GEREZANI

Kufuatia kuachiwa huru kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga kutoka Gereza la Ruanda, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amesema bado hawajafahamu ni taratibu gani zimetumika kuwaachia huru wakati kifungo chao kilikuwa bado.

“Katika mazingira ya kawaida, siku yao ya kifungo walichokuwa wamepewa kilikuwa kinaishia Juni 5, mwaka huu, lakini ghafla wakapewa taarifa kwamba wataachiwa leo. Hatuna hakika sana ni taratibu gani...

 

12 months ago

Malunde

MBUNGE SUGU ASHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE GEREZANI

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa gerezani huku familia yake ikiisherehekea kwa kula chakula pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Nuru, Uyole jijini Mbeya.

Sugu ambaye anafikisha umri wa miaka 46, alisherehekea siku hiyo akiwa gerezani ambako anatumikia kifungo cha miezi mitano.

Keki ya mbunge huyo ilipambwa kwa kuchorwa pingu, mnyororo na taswira ya chumba cha Magereza.

Sugu alihukumiwa kifungo...

 

11 months ago

Zanzibar 24

Magereza waeleza sababu ya Sugu kutoka gerezani mapema

Jeshi la Magereza limeeleza kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiliwa huru kwa msamaha wa Rais uliotolewa katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Afisa Habari wa Jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo, Rais alitoa msamaha kwa wafungwa ambapo baadhi walitoka siku hiyo hiyo na wengine walibaki kumalizia muda wao, kutokana na...

 

11 months ago

Malunde

KAULI YA NAPE NNAUYE BAADA YA SUGU KUTOKA GEREZANI

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemkaribisha uraini Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kutoka gereza la Ruanda alipokuwa akitumikia kifungo chake.

Nape amesema kuwa anakumbuka Mbunge huyo ambaye pia ni msanii aliwahi kuimba juu yake wakat alipoanza siasa.

“Karibu tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo nilipoanza siasa},” ameandika Nape kupitia ukurasa wake Twitter.

Sugu na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walitiwa hatiani...

 

1 year ago

Malunde

MAGEREZA WATAJA SABABU ZA KUMZUI PROFESA JAY KUMUONA SUGU GEREZANI

Mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ jana alizuiwa kumuona mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi pamoja na katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga baada ya kuzuiwa na maofisa wa magereza.

Profesa Jay aliyeambatana na mke wake, Grace Haule walifika jana jijini Mbeya na kwenda gerezani kuwaona Sugu na Masonga ambao wapo mahabusu wakikabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Mkuu wa magereza Mkoa wa Mbeya,...

 

3 years ago

Mwananchi

Kada Chadema ashinda udiwani akiwa gerezani

Kada mwingine wa Chadema ameukwaa uongozi kwa staili ya aina yake baada ya wananchi kumchagua kuwa diwani wa Kata ya Lusaka akiwa gerezani ambako anatumikia kifungo cha miezi sita kwa kosa la kupigana hadharani.

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani