Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM kizuizini kwa kuhujumu uchumi wa Nchi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano jana Jumatano wapandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi ikiwamo kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ‘ ARV’s ‘ na kusababisha hasara ya Sh 148 milioni. Kabla ya kusomewa mashtaka ya kesi hiyo mpya ya uhujumu uchumi namba 80 ya 2017, mahakama ilimfutia kesi iliyokuwa na mashtaka matano yanayofanana na hiyo iliyofunguliwa mwaka 2014. Kesi hiyo ilifutwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuomba iondolewe kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao. Kesi hiyo ilikuwa katika hatua ya usikilizwaji wa  mashahidi wa upande wa mashtaka na mashadi tisa walikuwa wamekwishatoa ushahidi wao na washtakiwa walikuwa nje kwa dhamana. Baada ya kesi hiyo kufutwa, Madabida ambaye ni ofisa mtendaji mkuu wa kiwanda hicho na wenzake Seif Shamte ambaye ni mkurugenzi wa uendeshaji, Simon Msoffe (meneja masoko) na Fatma Shango (mhasibu msaidizi) wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd. Pamoja na Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa  walikamatwa tena na kufunguliwa kesi hiyo mpya ya uhujumu uchumi. Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa hao hawakurusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Wakili wa Serikali, Pius Hilla alisema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika lakini DPP bado hajafanya maamuzi kama isikilizwe Kisutu ama Mahakama Kuu. Washtakiwa wote wanatetewa na Mawakili Denis Msafiri, Makaki Masatu na Nehemiah Nkoko. Wakili Msafiri alisema Mahakama ya Kisutu inayo mamlaka ya kuisikiliza hiyo kwa sababu kiwango chake cha fedha kipo chini ya Sh 1 bilioni ambayo ndiyo inapaswa kusikilizwa Mahakama Kuu. Kutokana na hoja hiyo Wakili Hilla aliomba wapewe muda hadi leo Alhamisi ndiyo wajibu hoja ya upande wa utetezi. Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi leo Alhamisi kutokana na ombi hilo na kuamuru washtakiwa wapelekwe polisi hadi leo Alhamisi itakaposikilizwa hoja kama mahakama hiyo ina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo ama la.

The post Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM kizuizini kwa kuhujumu uchumi wa Nchi appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

MwanaHALISI

Mbunge CCM atuhumiwa kuhujumu uchumi

MBUNGE wa Kwimba, Mwanza, Shannif Mansour (CCM), anatuhumiwa kugoma kulipa kodi ya eneo lake la ardhi lenye ukubwa wa hekta 39,000, kiasi cha zaidi ya Sh.  500 milioni tangu mwaka 2010, anaandika Moses Mseti. Mansour kupitia kampuni yake ya Sineji Tanzania Limited, anatuhumiwa kuigomea serikali kulipa kiasi hicho cha fedha kwa madai yeye hawezi kulipa ...

 

2 months ago

Malunde

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DAR AACHIWA KWA DHAMANA

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefanikiwa kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Ni baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasilisha cheti kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo kimeipa mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, washtakiwa hao walisomewa mashtaka mapya matano mahakamani hapo leo Ijumaa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Katika mashtaka hayo mawili ni...

 

3 months ago

Malunde

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUSAMBAZA ARV's FEKI

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano jana Jumatano walipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi ikiwamo kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ' ARV’s ' na kusababisha hasara ya Sh 148 milioni.

Kabla ya kusomewa mashtaka ya kesi hiyo mpya ya uhujumu uchumi namba 80 ya 2017, mahakama ilimfutia kesi iliyokuwa na mashtaka matano yanayofanana na hiyo iliyofunguliwa mwaka...

 

4 years ago

Tanzania Daima

Mlebanoni kizimbani kwa kuhujumu uchumi

RAIA wa Lebanon, Mohamed Attwi (27), amepandiswa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana, akikabiliwa na mashitaka sita likiwemo la kuisababishia hasara ya zaidi ya...

 

3 years ago

BBCSwahili

Nigeria:PDP lawamani kwa kuhujumu uchumi

Uongozi wa Muhamadu Buhari ambao utachukua madaraka siku ya ijumaa wiki hii unailaumu utawala wa Goodluck Jonathan kwa kuhujumu uchumi

 

3 years ago

StarTV

PDP chalaumiwa kwa kuhujumu uchumi Nigeria.


Uongozi wa Muhamadu Buhari ambao utachukua madaraka siku ya ijumaa wiki hii unailaumu utawala wa Goodluck Jonathan kwa kuhujumu uchumi

Uongozi wa serikali mpya ya rais Muhamadu Buhari ambayo itaingia madarakani siku ya ijumaa wiki hii inaulaumu utawala unaondoka wa Goodluck Jonathan kwa kuhujumu taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Uongozi wa All Progressives Congress (APC) unailaumu utawala uliopoa sasa kwa ukosefu mkubwa wa mafuta ukosefu wa umeme na upungufu wa uzalishaji...

 

3 months ago

Zanzibar 24

Vigogo wanne wa TANESCO wafikishwa Mahakamani kwa kuhujumu Uchumi

Maofisa wanne wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco )na watu wengine wawili wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 202 ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 2.7. Hati ya Mashtaka imesomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliyekuwa akisaidiana na wakili wa Serikali Gloria Mwende ambapo watuhumiwa wote wanakabiliwa nashtaka moja la kula njama, kutoa taarifa za uongo, kuisababishia...

 

2 years ago

StarTV

Raia wawili wa China wapatiwa dhamana kwa Kesi Ya kuhujumu Uchumi

Mahakama kuu kanda ya Bukoba imetoa dhamana kwa watuhumiwa wawili raia wa China waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya CHICCO wanaokabiliwa na tuhuma za kuliingizia hasara ya zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni sabini na tatu shirika la umeme nchini TANESCO.

Dhamana hiyo imetolewa na Kaimu Msajili wa mahakama kuu kanda ya Bukoba Dennis Mpelembwa baada ya watuhumiwa hao kutimiza masharti manne waliyopewa na mahakama hiyo.

 Washtakiwa hao wawili raia wa CHINA Whang Lee na Zhang...

 

9 months ago

Malunde

MKURUGENZI WA HALOTEL AHUKUMIWA KULIPA MIL 700 KWA KUHUJUMU UCHUMI


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya Halotel, Do Hong


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewatia hatiani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania ya Viettel inayofanya biashara kama Halotel, Do Hong na wenzake wanane, kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuwataka kulipa faini ya zaidi ya Sh. milioni 700.
Hata hivyo, Hong ameachiwa huru baada ya kulipa Sh milioni 479 ambazo kati yake, sh milioni 20 ni faini na sh milioni 459 ni fidia ya hasara...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani