ARDHI YASABABISHA MGOGORO KATI YA FAMILIA NA SERIKALI MJINI GEITA


Na Joel Maduka ,Geita.
Familia ya Bw Mlelemi Mashirungu inayoishi mtaa wa Mkolani Kata ya Nyankumbu wilayani Geita imeilalamikia serikali kwa kuanzisha ujenzi wa shule ya msingi Shinde kwenye shamba la ukoo huo lenye ukubwa wa ekari 20 bila makubaliano na serikali ya Halmashauri ya mji wa Geita .
Msimamizi wa eneo hilo Bw Sizya Mashirungu amesema eneo la ujenzi wa shule hiyo lilitengwa na serikali ya kijiji kabla ya kubadilishwa na kuwa mitaa lakini ameshangazwa na kitendo cha serikali...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

StarTV

Serikali yaombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi

Serikali imeombwa kuingilia kati na kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na uongozi wa Kiwanda cha karatasi cha Mgololo kilichopo wilayani Mufindi na ule wa waliokuwa watumishi wa Kiwanda hicho kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa ombi hilo kwa Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina alipotoa taarifa ya kushindwa kutatulika kwa mgogoro huo licha ya jitihada za kutafuta suluhu.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa...

 

3 years ago

StarTV

Wakazi Vicheji waiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi:

Wakazi wa kata ya Vicheji Wilaya ya Mkuranga wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa Shamba lililotelekezwa kwa zaidi ya miaka 30 huku mmiliki wa shamba hilo akiwa hafahamiki.

Licha ya sintofahamu hiyo ya umiliki, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vicheji, Ramadhani Lugome amedaiwa kutotoa ushirikiano kwa wananchi ili kutafuta suluhu ya kupunguza hali ya uhalifu kwenye msitu huo.

Mmoja wa wazee wa kata hiyo ya  Vicheji, Maulidi Abdalla Mtulia amesema wananchi wa kata hiyo hawana imani...

 

3 years ago

StarTV

Wakazi Mekomariro Bunda waiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi.

Wakazi wa kijiji cha Mekomariro kata ya Mihingo wilayani Bunda mkoani Mara wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu kati yao na kijiji cha Sirorisimba wilayani Butiama ili kuepusha mapigano yanayoweza kutokea katika eneo hilo.

Mgogoro huo unadaiwa kuwa ni wa muda mrefu na umekuwa ukipigwa danadana na uongozi wa juu bila sababu za msingi kukiwepo baadhi ya viongozi kutokujali matatizo ya wakazi wa maeneo hayo.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mikomarilo kata ya...

 

5 years ago

Michuzi

KINANA AINGILIA KATI MGOGORO SUGU WA ARDHI KATI YA WANANCHI NA MWENKEZAJI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ameingilia kati Mgogoro wa ardhi uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu katika kijiji cha Mawenzusi,wilaya ya Sumbawanga mjini.Mgogoro huo uliohusu Wananchi na anayedaiwa kuwa Mwekezaji inaelezwa kuwa maamuzi yalikwishatolewa na Mh.Rais Jakaya Kikwete,kuwa Wananchi wapewe kipao mbele na Mwekezaji apewe kiasi,lakini mpaka sasa hakuna lililotekelezwa kufuatia Watendaji waliokuwa wamepewa dhamana ya kulisimamia jambo hilo kusua sua na hatimaye kutopatiwa...

 

11 months ago

CCM Blog

WAZIRI MPINA AAHIDI SERIKALI KUTATUA KISTAARAB MGOGORO WA ARDHI KATI YA MNADA WA PUGU NA WAKIJIJI CHA BANGULO, ASIMAMISHA WANANCHI KUJENGA NYUMBA MPYA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kuhaga Mpina akizungumza na wananchi katika Mnada wa Pugu, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.

Na Bashir Nkoromo, Pugu
Serikali ameagiza shughuli mpya za ujenzi na nyingine za maendeleo ikiwemo kilimo katika Kijiji cha Bangulo Kata ya Pugu Stesheni kusimama kuanzia leo, kusubiri mgogoro wa eneo kati ya Kijiji hicho na Mnada wa mifugo wa Pugu upatiwe ufumbuzi.

Akizungumza na wananchi leo baada ya kutembelea maeneo ya mpaka wa Mnada huo,...

 

3 years ago

Channelten

Mgogoro wa Ardhi Babati, Naibu Waziri Maliasili aingilia kati

bati haki

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Ramo Makani ameingilia kati mgogoro wa ardhi wa mipaka kati ya vijiji vinne vilivyomo jirani na hifadhi ya taifa ya Tarangire wilayani Babati vijijini mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi.

Naibu waziri huyo aliyekuwepo ziarani mkoani arusha akitembelea maeneo yenye migogoro yaliyopakana na hifadhi za taifa na kuwataka wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi kuacha kuwekeza kwenye migogoro na kuheshimu mipaka.

Waziri Makani pia amewataka...

 

1 year ago

Channelten

Mgogoro wa Ardhi Manyara, Kamati ya ulinzi na Usalama yaingilia kati

jangwa-1024x562

Kamati ya ulinzi na usalama mkoani manyara imeingilia kati na kufanikiwa kuirejeshea eneo lenye ukubwa wa hekari 10 pamoja na kuijengea nyumba ya kudumu familia ya Pascalina Michael iishiyo eneo la ayalagaya wilayani babati ambalo limekuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu baina ya ndugu wa upande wa mwanaume wa familia hiyo pamoja na kutoa vitisho vya kuchomea nyumba na kuuwawa kwa wanafamili hao endapo wataendelea kubaki kwenye eneo hilo.

Familia hii iliyakimbia makazi yake kwa muda kutokana...

 

2 years ago

Channelten

Mgogoro wa Ardhi Ndato Rungwe Wananchi wamuomba Rais aingilie kati

Wananchi wa kata ya Ndato wamemuomba Rais Dk John Pombe Magufuli kuingilia kati Mgogoro wa Ardhi baina yao na chama cha mapinduzi ambao utasababisha Shule ya Msingi Gooye kuvunjwa na hivyo wanafunzi kukosa mahali pa kusomea.

Kauli hii imetolewa na wananchi wa kata ya Ndanto Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe hususani wa kijiji cha Ndaga na Gooye wakati wa Mkutano Mkuu , ambao umeitishwa kwa ajili ya kutoa mrejesho wa hukumu ya kesi kutoka baraza la ardhi la Wilaya , ambayo CCM imeshinda,...

 

2 years ago

Channelten

UGAWAJI wa ardhi kiholela inayofanywa na viongozi wa serikali ya Kijiji yasababisha migogoro

Tanzania_Kigoma_location_map.svg

UGAWAJI wa ardhi kiholela inayofanywa na viongozi wa serikali ya Kijiji na mtaa mkoa wa Kigoma imeelezwa kuwa chanzo cha kujenga chuki,vinyongo na hasira kwa wananchi na hivyo kusababisha migogoro isiyo na tija.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa semina elekezi kwa wenyeviti wa Mtaa na vijiji ili watambue majukumu yao, pamoja na kutambua changamoto zinazo wakabili na sio kutumia madaraka waliyonayo kwa maslahi yao binafsi.

Baadhi ya viongozi wa serikali ya vijiji na mtaa wamegeuka kuwa miungu...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani