Azam imeweka historia katika Mashindano ya Mapinduzi Cup

Timu ya Azam FC imeweka rikodi kuwa timu pekee kufika fainali katika Mashindano ya Kombe la Mapinduzi bila ya kuruhusu kufungwa hata bao moja.

Azam wametinga fainali baada ya kuitoa Taifa ya Jang’ombe kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ambapo katika makundi pia michezo yake yote mitatu hawajaruhusu bao hata moja.

Walianza mchezo wao wa kwanza kwa kuifunga Zimamoto ya Visiwani Zanzibar bao 1-0, wakatoka sare tasa (0-0) na Jamhuri ya Pemba kisha kuifuga Yanga kipigo takatifu cha mabao 4-0, hivyo imecheza michezo yote hiyo bila ya lango lao linaloongozwa na Aishi Manula kuguswa.

Azam FC kesho kutwa Ijumaa January 13, 2017 watacheza Fainali na timu ya Simba mchezo utakaopigwa majira ya Saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan.

Hii ni fainali ya tatu kucheza timu ya Azam katika mashindano hayo ambapo aliwahi kucheza mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013 na zote kufanikiwa kutwaa Ubingwa baada ya kuzifunga timu ya Jamhuri na timu ya Tusker ya Kenya, hivyo ana historia nzuri ya kutopoteza michezo ya fainali katika Kombe hilo.

 

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

The post Azam imeweka historia katika Mashindano ya Mapinduzi Cup appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

BBCSwahili

Azam,Yanga sare Mapinduzi Cup.

Timu ya Yanga imetoshana nguvu na Azam FC, kufuatia sare ya bao 1-1 katika Mechi ya Kundi B la michuano ya Mapinduzi Cup 2016

 

11 months ago

Zanzibar 24

Yanga ya kunutwa 4-0 na Azam FC Mapinduzi Cup 2017

Michezo ya mwisho ya hatua ya Makundi ya Kombe la Mapinduzi kwa Kundi B imechezwa leo January 7 2017 katika uwanja wa Amaan Zanzibar, mchezo kati ya Yanga dhidi ya Azam FC ndio mchezo uliyokuwa unasubiriwa kwa hamu zaidi  licha ya kuwa timu zote zilikuwa zimefuzu.

Katika mchezo huo Azam FC ambao wanaonekana walikuwa wanasuasua katika michuano hiyo, imewashangaza wengi kwa kuwafunga Yanga kwa goli 4-0.

Magoli ya Azam FC yalifungwa na:-

John Bocco  dakika ya 2,

Yahaya Mohamed dakika ya...

 

11 months ago

Zanzibar 24

Ni Simba, kuvaana na Azam fainali Mapinduzi CUP

Dakika 90 zimemaliza kwa vigogo wa soka nchini Simba na Yanga kwenda bila kufungana katika mchezo wa kombe la Mapinduzi iliyopigwa katika uwanja wa Amaan.

Ndipo hatua ya matuta imeweza kuipeleka timu ya Simba Fainali  baada ya kupata jumla ya Penati 4-2 ambapo itakutana na Azam FC waliokuwa wa kwanza kutinga Fainali hiyo baada ya kuifunga Taifa ya Jang’ombe goli 1-0.

The post Ni Simba, kuvaana na Azam fainali Mapinduzi CUP appeared first on Zanzibar24.

 

11 months ago

Bongo5

Mapinduzi Cup Fainali leo ni Simba au Azam FC?

Fainali za 11 za michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup zinatarajiwa kupigwa leo kwenye dimba la Amaan Visiwani Zanzibar kwa kuzikutanisha timu za Simba na Azam zote za Dar es Salaam.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:15 usiku wa leo, utakuwa ni wa pili kuzikutanisha timu hizo katika fainali ya michuano hiyo.

Awali zilikutana katika fainali ya mwaka 2012 na Azam FC ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa taji lake la kwanza kati ya mawili ya Kombe la Mapinduzi, linguine likija mwaka 2013...

 

1 year ago

Michuzi

MASAUNI AZINDUA MASHINDANO NAGE MAPINDUZI CUP ZANZIBAR, ACHANGIA VICOBA JIMBONI KWAKE

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi kabla ya kuzindua Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani. Naibu Waziri wa...

 

2 years ago

MillardAyo

VIDEO: Magoli ya Azam FC vs Mafunzo FC 1-2 Mapinduzi CUP 2015

Hii ni January 7 2016 kutoka kombe la Mapinduzi 2016 linaloendelea Zanzibar ambapo Azam FC inayofundishwa na kocha Stewart Hall ilivunja rekodi yake yenyewe kwa kutolewa katika michuano ya kombe hili kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi toka waanze kushiriki michuano, Azam FC walikubali kipigo cha goli 2-1 kutoka Mafunzo FC ya Zanzibar, tazama ilivyokua kwenye […]

The post VIDEO: Magoli ya Azam FC vs Mafunzo FC 1-2 Mapinduzi CUP 2015 appeared first on TZA_MillardAyo.

 

1 year ago

TheCitizen

Young Africans, Simba, Azam to face off in Mapinduzi Cup

Archrivals Young Africans and Simba SC are among the nine teams that have been lined up for the Mapinduzi Cup scheduled to start in January next year.

 

11 months ago

Zanzibar 24

Azam kucheza fainali mara ya tatu Mapinduzi Cup

Timu ya Azam FC imefanikiwa kutinga hatua ya fainali kwa mara ya tatu katika Mashindano ya Mapinduzi CUP baada ya jioni ya leo kuwafunga Taifa ya Jang’ombe bao 1-0 mchezo ulosukumwa katika Uwanja wa Amaan.

 

Bao pekee la Azam amefunga Frank Domayo katika ya dakika 33 na pia katangazwa kuwa nyota wa mchezo huo  yani Man of the Match.

 

Hii ni fainali ya tatu kucheza timu ya Azam katika mashindano hayo ambapo aliwahi kucheza mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013 na zote kufanikiwa kutwaa...

 

11 months ago

Michuzi

MAKOCHA SIMBA, AZAM WATAMBIANA FAINALI ZA MAPINDUZI CUP


Kocha  msaidizi wa Simba Jackson Mayanja

Kueleka mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi baina ya Azam na Simba makocha wa pande zote mbili wameanza kutambiana kila mmoja akijinadi kuwa ana uwezo wa kumfunga mwenzake ndani ya dakiika 90.Fainali hiyo inayofanyika kesho kwenye uwan ja wa Amani inawakutanisha timu hizo zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo Azam wakiwatoa Jang'ombe Taifa kwa goli 1-0, Simba wakiwatoa Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2.Kocha  msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amejigamba...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani