Azam kucheza fainali mara ya tatu Mapinduzi Cup

Timu ya Azam FC imefanikiwa kutinga hatua ya fainali kwa mara ya tatu katika Mashindano ya Mapinduzi CUP baada ya jioni ya leo kuwafunga Taifa ya Jang’ombe bao 1-0 mchezo ulosukumwa katika Uwanja wa Amaan.

 

Bao pekee la Azam amefunga Frank Domayo katika ya dakika 33 na pia katangazwa kuwa nyota wa mchezo huo  yani Man of the Match.

 

Hii ni fainali ya tatu kucheza timu ya Azam katika mashindano hayo ambapo aliwahi kucheza mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013 na zote kufanikiwa kutwaa Ubingwa baada ya kuzifunga timu ya Jamhuri na timu ya Tusker ya Kenya, hivyo ana historia nzuri ya kutopoteza mchezo wa fainali.

 

Fainali ya Mashindano hayo yanatarajiwa kupigwa Ijumaa January 13, 2017 saa 2:15 usiku ambapo Azam watacheza na mshindi kati ya Simba au Yanga.

 

Haya ni Mashindano ya 11 tangu kuanzishwa kwake ambapo yalianzishwa tangu mwaka 2007 huku timu moja tu kutoka Visiwani Zanzibar kuchukua kombe hilo ambapo mara mbili likienda Uganda na mara saba likivuka maji kwenda Tanzania bara ambapo mwaka huu utakuwa wa nane kwenda bara kwani timu zote zilizobakia ni za Bara.

 

Miembeni wazee wa Kwalalumpa ndio timu pekee kutoka hapa Visiwani Zanzibar kuchukua kombe hilo ambapo ilichukua mwaka 2009 katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba baada ya kuifunga KMKM.

 

URA na KCCA zote kutoka Uganda ndizo timu mbili kutoka nje ya Tanzania kutwaa taji hilo ambapo URA ilichukua msimu ulopita wa mwaka 2016 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 3-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan huku wenzao KCCA walichukua kombe hilo mbele ya Simba ilikuwa mwaka 2014 katika uwanja wa Amaan.

 

Simba ndio timu inayoongoza kubeba kombe hilo mara nyingi (3) ambapo ilifanikiwa kuchukua mwaka 2008 mbele ya Mtibwa, wakachukua tena mwaka 2011 mbele ya Yanga na mwaka 2015 mbele ya Mtibwa.

 

Mwaka 2011 Simba iliifunga Yanga mabao 2-0 katika Uwanja wa Amaan kwa mabao ya Shija Mkina na Mussa Hassan Mgosi ambae kwasasa ndie Meneja wa Simba.

 

Azam FC ndio timu pekee iloweza kutetea taji lake baada ya kuchukua kombe hilo mara mbili mfululizo mwaka 2012 mbele ya Jamhuri na mwaka 2013 mbele ya Tusker ya Kenya na sasa tena katinga fainali.

 

Timu nyengine kutoka bara zilizowahi kubeba ndoo hiyo ni Yanga ambao wamewahi kuchukua mara moja na ilikuwa ndio mwaka wa kwanza kuchezwa ilikuwa mwaka 2007 walipoifunga Mtibwa huku wenzao hao Mtibwa nawao wamechukua mara moja ilikuwa mwaka 2010 mbele ya timu ya Ocean View.

 

Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

The post Azam kucheza fainali mara ya tatu Mapinduzi Cup appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Huyu ndie mchezaji anaeongoza kucheza mara nyingi mapinduzi Cup

Suleiman Ali “Pishori” ambae kwasasa ni mchezaji wa Kilimani city akitokea Miembeni katika dirisha hili dogo la usajili ndie mchezaji anaeongoza kucheza mara nyingi kuliko mchezaji yoyote kwenye Mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambayo yanahitimishwa usiku wa leo kwenye fainali ya Simba dhidi ya Azam FC.

Pishori amecheza jumla ya mechi 24 katika mashindano hayo akiwa na timu nne tofauti tangu mwaka 2007 yalipoanzishwa mpaka 2014 alipoishia kucheza hivyo amecheza miaka 8 mfululizo pasipo...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Ni Simba, kuvaana na Azam fainali Mapinduzi CUP

Dakika 90 zimemaliza kwa vigogo wa soka nchini Simba na Yanga kwenda bila kufungana katika mchezo wa kombe la Mapinduzi iliyopigwa katika uwanja wa Amaan.

Ndipo hatua ya matuta imeweza kuipeleka timu ya Simba Fainali  baada ya kupata jumla ya Penati 4-2 ambapo itakutana na Azam FC waliokuwa wa kwanza kutinga Fainali hiyo baada ya kuifunga Taifa ya Jang’ombe goli 1-0.

The post Ni Simba, kuvaana na Azam fainali Mapinduzi CUP appeared first on Zanzibar24.

 

1 year ago

Bongo5

Mapinduzi Cup Fainali leo ni Simba au Azam FC?

Fainali za 11 za michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup zinatarajiwa kupigwa leo kwenye dimba la Amaan Visiwani Zanzibar kwa kuzikutanisha timu za Simba na Azam zote za Dar es Salaam.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:15 usiku wa leo, utakuwa ni wa pili kuzikutanisha timu hizo katika fainali ya michuano hiyo.

Awali zilikutana katika fainali ya mwaka 2012 na Azam FC ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa taji lake la kwanza kati ya mawili ya Kombe la Mapinduzi, linguine likija mwaka 2013...

 

1 year ago

Michuzi

MAKOCHA SIMBA, AZAM WATAMBIANA FAINALI ZA MAPINDUZI CUP


Kocha  msaidizi wa Simba Jackson Mayanja

Kueleka mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi baina ya Azam na Simba makocha wa pande zote mbili wameanza kutambiana kila mmoja akijinadi kuwa ana uwezo wa kumfunga mwenzake ndani ya dakiika 90.Fainali hiyo inayofanyika kesho kwenye uwan ja wa Amani inawakutanisha timu hizo zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo Azam wakiwatoa Jang'ombe Taifa kwa goli 1-0, Simba wakiwatoa Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2.Kocha  msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amejigamba...

 

1 year ago

MillardAyo

PICHA: Frank Domayo ameipeleka Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017

whatsapp-image-2017-01-10-at-19-51-57

January 10 2017 Azam FC walishuka dimba kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan, Azam FC ambao wanakumbukumbu ya kupata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Yanga mchezo uliyopita, leo wametinga fainali kwa ushindi wa goli 1-0. Ushindi wa Azam FC uliyowapeleka fainali ya michuano ya Mapinduzi […]

The post PICHA: Frank Domayo ameipeleka Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017 appeared first on millardayo.com.

 

1 year ago

MillardAyo

VIDEO: Goli la Domayo lililoipeleka Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017

whatsapp-image-2017-01-10-at-19-52-33

January 10 2017 Azam FC walishuka dimba kucheza mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan, Azam FC ambao wanakumbukumbu ya kupata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Yanga mchezo uliyopita, leo wametinga fainali kwa ushindi wa goli 1-0. VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

The post VIDEO: Goli la Domayo lililoipeleka Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017 appeared first on millardayo.com.

 

1 year ago

Dewji Blog

Fainali ya ‘kibabe’ Mapinduzi Cup jioni ya leo Zanzibar, Simba Sc dhidi ya Azam FC

Usiku wa leo wa saa  2: 00, Macho yote ya wapenda soka hasa wadau na wanazi wakubwa wa Wekundu wa Msimbazaji Simba  SC na Azam FC  ambapo watashuhudia mtanange mkali katika fainali ya Kombe la Mapinduzi  kwenye dimba  la  Amaan, visiwani Zanzibar.

Mchezo huo unaotarajiwa unatarajiwa kuanza Saa 2:15 usiku wa leo, utakuwa ni wa pili kuzikutanisha timu hizo katika fainali ya michuano hiyo.

Timu hizo zimekuwa na historia nzuri kwenye kombe hilo kwani zimewahi kukutana mara kadhaa huku awali...

 

1 year ago

MillardAyo

Simba vs Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017, bye bye Yanga

screen-shot-2017-01-11-at-12-31-06-am

Usiku wa January 10 2017 visiwani Zanzibar mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Mapinduzi Cup 2017 kati ya Simba dhidi ya Yanga ulichezwa visiwani Zanzibar katika uwanja wa Amaan, baada ya Azam FC kutinga hatua ya fainali kwa kumfunga Taifa Jang’ombe goli 1-0. Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Simba kukutana na […]

The post Simba vs Azam FC fainali Mapinduzi Cup 2017, bye bye Yanga appeared first on millardayo.com.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani