Azam ngoma bado mbichi, mechi saba mfululizo bila ushindi: Ubaoni Azam 1-1 Mtibwa Sugar

Baada ya kutoka sare na Yanga, gonjwa la sare laendelea kuitafuna klabu ya Azam Fc ikicheza kwenye uwanja wa Azam Complex,Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam imetoshana nguvu sawa na Mtibwa Sugar kwa kufungana bao 1-1.

Dakika ya 2 Mshambuliaji mwenye mwili uliojengeka Rashid Mandawa aliwanyanyua mashabiki wa Mtibwa Sugar kwa kufunga bao safi kwa njia ya kichwa akiunganisha krosi ya Issa Rashind hata hivyo Azam walisawazishwa kupitia kwa kiungo wao mkabaji Himid Mau kwa njia ya...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

MillardAyo

VIDEO: Azam FC walikipiga na Mtibwa Sugar, tazama goli la ushindi

World Cup 2014 Brazil. Brazuca football
Copyright: ververidis / 123RF Stock Photo

April 13 2016 Azam FC walicheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu Turiani kufanikiwaekichkuwafunga wenyeji wao  goli 1-0. Goli la Azam FC lilifungwa na nahodha John Bocco kwa mkwaju wa penati. Jikumbushe kwa kutazama goli lao hapa. Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika […]

The post VIDEO: Azam FC walikipiga na Mtibwa Sugar, tazama goli la ushindi appeared first on...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Bocco aibebea Azam Kaitaba: Ubaoni Azam 3-2 Kagera Sugar

BAO lililofungwa na nahodha John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 86, limeiwezesha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kuibuka na pointi zote tatu baada ya kuinyuka Kagera Sugar mabao 3-2 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kaitaba. Bukoba, mkoani Kagera jioni ya Jana.

Bao hilo linamfanya Bocco kufikisha mabao matano kwenye msimu huu wa ligi akizidiwa mabao mawili na Shiza Kichuya wa Simba, anayeongoza kileleni kwa mabao saba.

Mabao mengine ya Azam yalifungwa na Mudathir Yahya na...

 

3 years ago

MillardAyo

Ushindi wa Azam FC waishusha Yanga kileleni, cheki pichaz walivyoiadhibu Mtibwa Sugar Dec 30

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 30 kwa mchezo mmoja wa kiporo kumaliziwa katika dimba la Azam Complex Mbande Chamazi. Huu ni mchezo ambao ulikuwa unakutanisha timu ambazo zinatafuta nafasi ya kusogelea kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi. Mchezo wa December 30 ulikuwa unazikutanisha timu ya Azam FC dhidi ya klabu ya […]

The post Ushindi wa Azam FC waishusha Yanga kileleni, cheki pichaz walivyoiadhibu Mtibwa Sugar Dec 30 appeared first on TZA_MillardAyo.

 

2 years ago

Zanzibar 24

Shaaban Iddi aipa Azam ushindi wa kwanza Kirumba; Ubaoni Azam 1-0 Toto African

Azam jana jioni ilitoa nuksi kufuatia ushindi mwembamba ulioupata dhidi ya Toto African. Shukran kwa Shaban iddi aliyefunga goli hilo dakika za usiku dakika 81.

Mbali na rekodi hiyo, ushindi huo pia umeifanya Azam FC kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikifikisha jumla ya pointi 22 sawa na Stand United iliyoishusha kutokana na kuwa na tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa.

The post Shaaban Iddi aipa Azam ushindi wa kwanza Kirumba; Ubaoni Azam 1-0 Toto African appeared...

 

3 years ago

MillardAyo

Cheki Video ya magoli ya Mtibwa Sugar dhidi ya Azam FC, Mtibwa wakimbadilikia refa baada ya goli lao kulikataa

Mchezo wa pili wa Kundi B wa michuano ya Mapinduzi 2016 ulichezwa usiku wa January 3 kwa kuzikutanisha klabu za Mtibwa Sugar dhidi ya Azam FC. Huu ni mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, baada ya Azam FC kusawazisha goli, lakini pia kuna goli lilifungwa na Mtibwa Sugar lilikataliwa na muamuzi na kuleta […]

The post Cheki Video ya magoli ya Mtibwa Sugar dhidi ya Azam FC, Mtibwa wakimbadilikia refa baada ya goli lao kulikataa appeared first on TZA_MillardAyo.

 

4 years ago

Mwananchi

Azam yaichakaza Mtibwa Sugar

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Azam wamelizamisha jahazi la Mtibwa Sugar kwa kuichapa mabao 5-2 jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

 

2 years ago

Bongo5

Azam FC kujipima nguvu na Mtibwa Sugar J’mosi

Katika kujiandaa na mzunguko wa raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Klabu ya Azam FC, inatarajia kukipima kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, siku ya Jumamosi ya Desemba 10 saa 1.00 usiku.

img_1827

Azam FC iliyoanza maandalizi ya mzunguko huo wa pili Jumatatu iliyopita, itautumia mchezo huo kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza mikikimikiki ya ligi, ambapo inatarajia kufungua pazia kwa kucheza na African...

 

4 years ago

Michuzi

Azam FC yaiadhibu Mtibwa Sugar leo,yaichapa bao 5-2


Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao lao la tano dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Azama Complex jijini Dar es Salaam. Azam ilishinda 5-2. (Picha na Francis Dande)
 Mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar akimiliki mpira.
 Frank Domayo (shoto) akichuana na beki wa Kagera Sugar, Mussa Nampaka.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo.
Kipre Tchetche akimiliki mpira.
 Frank Domayo akishangilia bao lake.

 

2 years ago

Michuzi

Azam FC kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar


KATIKA kujiandaa vilivyo kuelekea mechi za raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kukipima kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Jumamosi ijayo Desemba 10 saa 1.00 usiku.

Azam FC iliyoanza maandalizi ya mzunguko huo wa pili Jumatatu iliyopita, itautumia mchezo huo kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza mikikimikiki ya ligi, ambapo inatarajia...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani