AZAM WAMSHUSHA MROMANIA KUKINOA KIKOSI HICHO

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, mchana huu imemtangaza, Aristica Cioaba, kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.
Cioaba, 45, anakuja Azam FC kurithi mikoba ya Mhispania Zeben Hernandez, aliyesitishiwa mkataba pamoja na benchi lake zima la ufundi.
Kocha huyo atasaidiana na makocha wazawa, Idd Nassor Cheche na Kocha wa Makipa Idd Abubakar, walioiongoza timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo saa 10.15 jioni ya leo itasaka fainali kwa kukipiga na Taifa ya Jang’ombe.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu Azam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba, tayari amefanikiwa kumpata kocha huyo na wameingia naye mkataba wa muda wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezwa.Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba kutoka nchini Romania, akimwaga wino wa kukinoa kikosi hicho, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba, huko visiwani Zanzibar leo.
Alisema Cioaba ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ataiongoza Azam FC kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwa msimu, ambapo baada ya kuisha watakaa tena mezani kufanya tathimini ya mafanikio yake na wapi wanaweza kuendelea kutokana na kazi iliyofanyika.
“Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC inapenda wadau wote wa mpira na wapenzi na mashabiki wa Azam kwamba klabu imempata mwalimu, ambaye ndiye ataiongoza klabu kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa msimu.
“Kwa hiyo kwa mashabiki wetu maana yake ni kwamba tukiingia kwenye mechi inayofuata ya ligi, kocha atakuwa ameanza kazi na Cheche (Idd Nassor) atakuwa msaidizi wake na benchi lake zima alilokuwa nalo hivi sasa litaendelea,” alisema.
Kawemba aliongeza kuwa hivi sasa kocha huyo atakuwa na kikosi visiwani Zanzibar kufuatilia mwenendo wa timu ulivyo na ataendelea kutoa ushauri panapohitajika na ataanza rasmi kukaa kwenye benchi mpaka pale vibali vyake vya kufanya kazi nchini vitakapokamilika.
“Taratibu hizo zitakwenda kwa mujibu wa sheria za nchi, ambapo tutaziheshimu na kuona ya kwamba tutazifanya kwa haraka zaidi ili mwalimu aweze kupata kibali cha kufanya kazi hapa nchini, kwa hayo machache tunawaomba mashabiki wetu wawe watulivu wampe sapoti kocha na wadau wote wa mpira waone ya kwamba tumefanya jambo la kheri,” alisema.Kauli ya kwanza ya Cioaba
Kwa upande wake Cioaba, alisema kuwa anafuraha kubwa leo hii kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo huku akiahidi kazi nzuri na kuifanya timu hiyo kuwa bora.
“Najua Azam FC hapa Tanzania ni moja ya timu kubwa yenye historia huko nyuma, napenda kuushukuru uongozi kwa kuniamini na kunipa nafasi kuja kufundisha soka kwenye nchi hii, kwa mashabiki napenda kuwaambia kuwa nalijua soka la Afrika, nimewahi kufundisha Ghana na kupata matokeo mazuri.
“Kuhusu wakati ujao, nina furaha sana kuhusu uongozi walipoongea na mimi wakati tunaweka mipango ya timu ya hapo baadaye na hili ni jambo zuri kwa kocha, kitaaluma nawaahidi mashabiki na watu wote wanaoipenda Azam FC, niko hapa kuwapa mambo mazuri katika kazi yangu kwenye klabu,” alisema.
Msimu uliopita, Cioaba aliiongoza Aduana Stars ya Ghana kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Ghana, ambapo anafahamiana kwa ukaribu na nyota wawili wa Azam FC, Yakubu Mohammed na Yahaya Mohammed, waliosajiliwa kutoka timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo.
Mbali na kufundisha soka nchini Ghana pia amewahi kufanya kazi kwenye miamba ya Morocco, Raja Casablanca, Al Masry ya Misri na katika nchi za Romania, Kuwait, Oman na Jordan.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

Mwanaspoti

Mromania wa Azam asubiriwa kukamilisha usajili wachezaji wa kujenga kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao

 Klabu ya Azam imesema inamsubiri kocha wake Aristico Cioaba arejee nchini ili iendelee na taratibu za usajili.

 

2 years ago

Mtanzania

Thierry Henry aanza kukinoa kikosi cha Ubelgiji

Training National Soccer Team of Belgium - 29082016

BRUSSELS, UBELGIJI

KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thierry Henry, ameanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Henry ameanza kazi Jumatatu wiki hii akiwa na mastaa wa timu hiyo ambao wanafanya vizuri katika Ligi ya England na sehemu zingine walizoungana kwa ajili ya kuitumikia timu yao.

Kabla ya kuanza kwa mazoezi, kocha huyo alikutana na wachezaji wake katika hoteli jijini Brussels na kuanza kujitambulisha mbele yao.

“Hallo...

 

1 year ago

Mwanaspoti

Mromania Azam kimeeleweka

KOCHA mpya wa Azam, Mromania Aristica Cioaba anatarajia kuanza rasmi kuinoa timu hiyo kuanzia kesho Jumatano baada ya vibali vyake vya kazi kutoka.

 

1 year ago

Habarileo

Azam yaajiri kocha Mromania

KLABU ya soka ya Azam imemtangaza Mromania Aristica Cioaba (45) kuwa kocha mkuu akichukua nafasi ya Mhispania Zeben Hernandez ambaye mkataba wake ulisitishwa.

 

11 months ago

Mwanaspoti

Azam kumpa mkataba Mromania

Dar es Salaam. Klabu ya Azam FC imesema imeridhishwa na uwezo wa kocha Aristico Cioaba na unatarajia kuanza naye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.

 

11 months ago

Mwanaspoti

Azam wampa Mromania mwaka mmoja

KLABU ya Azam FC imefikia uamuzi wa kumpa mkataba wa mwaka mmoja kocha Mromania Aristica Cioba na sasa kazi imebaki kwake

 

1 year ago

Bongo5

Hicho ndio kikosi cha Yanga kitachoenda kupambana na Alger

Klabu ya soka ya Yanga SC inapenda kutoa taarifa juu ya safari yake leo Alhamisi kwenda Algeria katika mechi ya marudiano dhidi ya Mc Alger.

Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka Alhamisi jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.

Wachezaji watakaondoka ni Makipa: Deogratius Munishi na Beno Kakolanya.

Nafasi ya ulinzi: Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua, Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin...

 

2 years ago

Bongo5

Brazil wametangaza kumfuta kazi kocha mkuu wa kikosi hicho Carlos Dunga

Brazil imemtimua kocha wao Carlos Dunga baada ya kikosi hicho kushindwa hata kuingia hatua ya mtoano ya michuano ya Copa America kufuatia nchi hiyo kutupwa nje na Peru..

dunga

Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, limetoa taarifa ya kumtimua Dunga ambaye pia alitarajiwa kuiongoza Nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ambayo itachezwa nchini Brazil mwezi Agosti.

Pamoja na Dunga, pia Wasaidizi wake wote wa Benchi la Ufundi wameondolewa, na CBF imesema itateua Watu wengine kuingoza Timu hiyo.

Brazil...

 

2 years ago

Habarileo

Kocha Azam afagilia kikosi chake

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amefurahishwa na kiwango cha wachezaji wake na ari kubwa ya kupambana waliyoionesha walipokuwa wakichuana na Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga juzi.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani