Azam yamtambulisha kocha mpya raia wa Romania

Klabu ya Azam FC imemshusha kocha mpya anaejulikana kwa jina la Aristica Cioaba kutoka Romania.

Kocha huyo amepewa mkataba wa miezi sita kwa ajili ya matazamio kama atafanya vizuri huenda akapewa mkataba wa muda mrefu lakini kinyume na hapo atafata nyayo za akina Zeben Hernandez.

Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd amesema Aristica Cioaba atasaidiwa na makocha wazalendo ambao wanaiongoza Azam kwa sasa wakiongozwa na Idd Cheche.

“Tumeshapata kocha mpya kutoka Romania ambaye tumempa mkataba wa miezi sita ili tuweze kuangalia uwezo wake. Kama atafanya vizuri basi tunaweza kumuongezea muda,” anasema Jafar Idd uku akiziua tetesi za makocha wazawa kujiunga na Azam.

“Kwa sasa atakuwa akisaidiwa na makocha wetu wazalendo ambao wapo na timu wakiongozwa na Idd Cheche.”

Baada ya Zeben na wasaidizi wake kutimuliwa, ziliibuka tetesi kuwa huenda Karl Ongala ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo akiwa mchezaji na kocha msaidizi akarejeshwa kwenye benchi la ufundi la Azam FC.

Mkwasa pia ni miongoni mwa makocha waliotajwa kupewa jukumu la kuinoa Azam baada ya kuachana na timu ya taifa ya Tanzania lakini ujio wa Aristica Cioaba unamaliza tetesi hizo.

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!Share on Whatsapp

Bongo5

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Bongo5

Klabu ya Simba yamtambulisha rasmi kocha Joseph Omog

Uongozi wa klabu ya Simba, umemtangaza rasmi kocha Joseph Omog, kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

img_0078

Evans Elieza Aveva ambaye ni Rais wa klabu ya Simba, amemtangaza kocha huyo kutoka nchini Cameroon pamoja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili ambao unamuwezesha kukinoa kikosi cha Wekundu Wa MSimbazi hadi mwaka 2018.

Omog amesaini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari.

Kocha huyo amerudi kwa mara ya pili kwenye ardhi ya Bongo na VPL baada ya awali kuifundisha klabu ya...

 

9 months ago

Michuzi

KOCHA MPYA AZAM AJA NA MBINU MPYA YA KLUIVAA SIMBA J'MOSI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Baada ya kutoka na ushindi dhidi ya Cosmo Politan wa magoli  3-1 na kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la FA, Klabu ya Azam , Jumamosi itakuwa kibaruani kuvaana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
Tayari kikosi cha Azam  kimeanza rasmi mazoezi juzi jioni kwa ajili ya kujiandaa na mtanange huo unaotarajiwa kuwa ni wa kisasi kwa pande zote mbili kutokana na aina ya matokeo yaliyotokea...

 

8 months ago

BBCSwahili

Raia waitaka serikali ijiuzulu Romania

Maelfu ya waandamanaji kwa mara nyingine wameingia barabarani nchini Romania, huku wakitaka serikali ijiuzulu.

 

3 years ago

Michuzi

RAIA WAWILI WA ROMANIA KOTINI KWA KUIHUJUMU TCRA


Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Mahakamani

WATU wawili raia wa Romania wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi ikiwemo udanganyifu,kutumia kadi zisizosajiliwa, kuingiza nchini na kutumia mitambo ya simu bila kibali, kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisababishia hasara ya Sh. Bilioni 2.1 Mamlaya ya Mawasiano Tanzania (TCRA).
Washtakiwa hao ni, Meneja...

 

2 years ago

Dewji Blog

Emirates yamtambulisha Meneja wake mpya wa Tanzania

Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (kushoto), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana.  

Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi...

 

9 months ago

MillardAyo

PICHA: Azam FC imemtangaza kocha mpya leo January 10 2017

img_2226

Siku 13 baada ya uongozi wa Azam FC kutangaza kumfuta kazi kocha wake mkuu na benchi lake la ufundi kutokea Hispania Zeben Hernandez, leo January 10 2017 wamemtangaza kocha mpya anayekuja kurithi nafasi ya Zeben. Azam FC imetangaza kuingia mkataba wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezewa mkataba zaidi na kocha Aristica Cioaba raia wa Romania […]

The post PICHA: Azam FC imemtangaza kocha mpya leo January 10 2017 appeared first on millardayo.com.

 

2 years ago

Bongo5

Studio ya Nahreel ‘The Industry’ yamtambulisha rasmi msanii mpya wa label yao, Rosa Ree

ROSA REE 1

Studio ya The Industry inayomilikiwa na producer Nahreel, imemtambulisha rasmi msanii mpya aitwaye Rosa Ree atakayekuwa chini ya label yao kuanzia January 14, 2016.

ROSA REE 1

Rose Ree mwenye miaka 20 ni rapper wa kike ambaye kazi zake zitaanza kusikika/Kuonekana siku si nyingi kuanzia sasa katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni za Tanzania na nje ya nchi.

Hii ni hatua nyingine kwa founder na mtayarishaji wa studio hiyo Nahreel ambaye pia ni msanii wa kundi la Navy Kenzo, katika kutimiza...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani