BANDA RUKSA KUICHEZEA SIMBA MECHI ZILIZOBAKI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Hatimaye kamati  ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekaa leo na kumsikiliza beki wa Simba Abdi Banda aliyesimamishwa na kamati ya saa 72 baada ya klabu ya Kagera Sugar kutuma malalamiko dhidi yake.

Kamati hiyo, imefikia maamuzi ya kumfungia  mechi mbili kwa kosa la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Aprili 2, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Adhabu hiyo inamuweka huru Banda kuweza kuendelea kucheza mechi tatu zilizosalia za timu hiyo baada ya kuwa nje kwa mechi mbili dhidi ya Mbao na Toto Africa zilizochezwa mapema wiki iliyopita.
Katika mchezo huo dhidi ya Kagera Banda alimpiga ngumi Kavila pasi na kuwa na mpira lakini mwamuzi wa mchezo huo hakumpa kadi na kupelekea adhabu yake kuwa nyepesi kulingana na ushahidi alioupeleka katika kamati hiyo.
Kamati iliweza kubaini kuwa Banda  hakupewa adhabu yoyote na refa kwa sababu hakuona tukio hilo, alifanya kitendo cha aina hiyo kwenye mechi namba 169 kati ya Simba na Yanga iliyofanyika Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam akimpiga kiungo Said Juma ‘Makapu’.

Awali, Klabu ya Kagera Sugar iliwasilisha malalamiko dhidi ya kitendo cha beki wa Simba, Abdi Banda kumpiga ngumi kiungo wao George Kavilla wakati akiwa hana mpira, na Mwamuzi wa mechi hiyo kutochukua hatua yoyote.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Mtanzania

Mayanja: Tutashinda mechi zilizobaki

Mayanja-J-1NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

BAADA ya kujiondoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Jackson  Mayanja, amesema jukumu lake sasa ni kuhakikisha kikosi chake kinamaliza michezo yote iliyobaki bila kupoteza.

Timu hiyo tayari imejitoa kwenye mbio za ubingwa kufuatia sare ya bila kufungana na Azam FC, katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi watakamilisha ratiba ya ligi msimu huu kwa kuikabili Mwadui FC,...

 

1 year ago

Bongo5

Dani Alves afikisha mechi 100 kuichezea Brazil

Mchezaji wa timu ya taifa Brazil na klabu ya Juventus, Dani Alves ametimiza mechi yake ya 100 katika timu yake ya taifa baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Peru, mechi iliyochezwa alfajiri ya November 16.

danalves

Wachezaji wengine walioichezea mechi nyumbani nyingi Brazil.

Cafu (142)
Roberto Carlos (125)
Lucio (105)
Claudio Taffarel (101)
Dani Alves (100)
Robinho (99)

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose...

 

2 years ago

MillardAyo

Simba walipofikia na Abdi Banda, lakini usishangae kuona Simba wameigomea TFF (+Video)

sport-news

Huenda unaweza kufikiria ni utani au mkwara tu wa klabu ya Simba kwa shirikisho la soka Tanzania TFF, ila Asubuhi ya March 23, ukweli umethibitika, uongozi wa klabu ya Simba March 23 umefanya mambo mawili makubwa kwa ajili ya klabu yao. Simba kupitia kwa afisa habari wake Haji Manara wameeleza msimamo wao kwa barua “TFF mara […]

The post Simba walipofikia na Abdi Banda, lakini usishangae kuona Simba wameigomea TFF (+Video) appeared first on TZA_MillardAyo.

 

3 years ago

GPL

Mastaa watano Yanga ruksa Simba

Mchezaji wa Yanga, Haruna Niyonzima. Na Wilbert Molandi
WAPO sokoni! Hivi ndivyo utakavyoweza kutamka baada ya wachezaji watano wa Klabu ya Yanga kubakiza miezi sita au chini ya hapo kwenye mikataba yao na timu hiyo. Kila timu hivi sasa inaangalia nafasi ipi yenye upungufu inayohitaji kuboresha kwa kusajili wachezaji wenye uwezo kwenye usajili wa dirisha dogo linalofunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15. Wachezaji hao...

 

4 years ago

GPL

WAMBURA RUKSA KUGOMBEA URAIS SIMBA

Mgombea wa nafasi ya urais klabuni hapo, Michael Wambura. RASMI Kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrejeha Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura kwenye mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya amewaambia Waandishi wa Habari mchana wa leo ofisi za TFF katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba Wambura amerejeshwa baada ya kikao chao...

 

3 years ago

Mwananchi

Ivo, Cholo, Owino ruksa kuondoka Simba

Rais wa Simba, Evance Aveva ametoa ruhusa kwa wachezaji wake, Ivo Mapunda, Nassor Said ‘Cholo’, Joseph Owino, Issa Rashida ‘Baba Ubaya’, Haruna Chanongo kufanya mazungumzo na timu nyingine.

 

4 years ago

Mwananchi

Wambura sasa ruksa kuwania urais Simba

Dar es Salaam. Kama ilivyotarajiwa, Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrejesha Michael Wambura kugombea urais wa Simba baada ya vikao vya siku mbili kujadili rufaa yake dhidi ya kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, uamuzi uliofanywa kwa kupiga kura na hivyo kumpitisha kwa kura 3-2.

 

2 years ago

Zanzibar 24

Simba ,Yanga ruksa kutumia uwanja wa Uhuru.

Bodi ya ligi Tanzania imethibitisha timu za Simba na Yanga zitautumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao za nyumbani baada ya serikali kuzizuia kuutumia uwanja wa taifa kama uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi zao za ligi kuu.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema, mechi ijayo ya Yanga wataanza kucheza kwenye uwanja huo dhidi ya Mtibwa mchezo unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi October 13.

The post Simba ,Yanga ruksa kutumia uwanja wa Uhuru. appeared first on Zanzibar24.

 

1 year ago

Michuzi

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani