BASATA hawajaufungia wimbo wangu – Nay wa Mitego

12534376_937830476307673_1527161113_n

Rapper Nay wa Mitego amekanusha taarifa zilizoenea kuwa, baraza la sanaa la taifa, BASATA limeufungia wimbo wake wenye utata, Shika Adabu Yako.

12534376_937830476307673_1527161113_n

Nay ametoa ufafanuzi huo kwenye Instagram kwa kuandika:

Pale unaposikia eti kuna wasiopenda kuambiwa Ukweli wamezusha Eti Wimbo wa #ShikaAdabuYako Basata wamefungia. Guys Wimbo haujafungiwa na Basata awajafungia Wimbo ila wale wenye Team zao kwenye mitandao wamechanwa kwenye #ShikaAdabuYako ndio wameufungia kwenye Masikio Yao sababu ya hawataki...

Bongo5

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Mwananchi

Basata laufungia wimbo wa Nay Mitego

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeufungia rasmi wimbo "Wapo" wa msanii Elibariki Emmanuel maarufu kama Nay wa Mitego.

 

2 years ago

Dewji Blog

BASATA yaufungia wimbo wa Nay wa Mitego “WAPO”

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo Wapo ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitego kutumika kwa namna yoyoye ile.

Hali kadhalika limeonya watu wote wanaotumia kazi za wasanii zilizopigwa marufuku na baraza hilo kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria za nchi na kwamba watakaobainika kuzitumia watachukuliwa hatua kali.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza amewataka wasanii na wadau wa kazi za sanaa nchini kuzingatia...

 

2 years ago

Zanzibar 24

BASATA yaufungia rasimi wimbo wa Nay wa Mitego ‘WAPO’

Baraza la Sanaa ka Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo ‘WAPO’ uliombwa na msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kutumika kwa namna yoyote ile.

Kwa mujibu wa BASATA kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kusimami kazi za Sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yafanyikayo katika tasnia ya Sanaa hayaachi taifa na wasanii katika hali sizizo salama.

Katika kutekeleza majukumu haya, Baraza linahakikisha linalinda maadili miongoni mwa...

 

2 years ago

Bongo5

Rasmi: BASATA yaufungia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego (Video)

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeufungia wimbo ‘Wapo’ wa rapa Nay wa Mitego kwa madai wimbo huyo hauna maadili.

Rapa huyo ana siku ya pili anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na wimbo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu hii Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa, Godfrey Mngereza amesema ni marufuku wimbo huo kupigwa sehemu yoyote kutokana na maudhui mabaya ya wimbo huo.

“Tunatangaza rasmi kuufungia wimbo mpya wa Nay wa Mitego, huu wimbo hauna maadili, marufuku hii siyo kwa...

 

3 years ago

MillardAyo

AUDIO: Basata kuhusu kuufungia wimbo wa Nay wa Mitego ‘Pale Kati’

WED344

Ni July 16, 2016 ambapo Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limetoa rasmi tamko la kuufungia wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego uitwao PALE KATI. Akizungumza na millardayo.com Katibu mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza alisema..’Ni kweli tumeufungia wimbo wa msanii Nay wa Mitego  kwasababu haupo kimaadili katika jamii ya kitanzania ukizungumzia maneno yenye […]

The post AUDIO: Basata kuhusu kuufungia wimbo wa Nay wa Mitego ‘Pale Kati’ appeared first on...

 

3 years ago

Bongo5

Nay wa Mitego aitwa BASATA, ni issue ya wimbo wake ‘Pale Kati’

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limemwita msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego ikiwa ni siku chache toka watangaze kuufungia wimbo wake ‘Pale Kati’ kutokana na wimbo huo kudaiwa kukiuka maadili.
Nay true boy

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay wa Mitego amesema kwa sasa hawezi kulizungumzia swala la kufungiwa kwa wimbo wake mpaka pale atakapofanya kikao na BASATA.

“Kesho nimeitwa BASATA, nadhani itakuwa ni vizuri nikizungumzanao, alafu ndo nije kuzungumza issue ya kufungiwa,” alisema Nay.
Nay wa Mitego
Picha ya...

 

2 years ago

Bongo5

Wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego ulisitishwa kupisha taratibu za kipolisi – BASATA

Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Baraza hilo limedai kuwa msanii kama ilivyo kwa raia yeyote anaweza kukamatwa na kushtakiwa...

 

3 years ago

Bongo5

It’s official: BASATA yaufungia wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’

nay new2

BASATA limetoa makucha yake. Hii ni taarifa yake rasmi iliyotoka Ijumaa hii:

nay new2

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.

Sambamba na kuufungia wimbo huo, BASATA litampa karipio kali Msanii huyo na kumwagiza kuacha mara moja kujihusisha kwa namna yoyote na tabia ya...

 

3 years ago

Michuzi

BASATA YAUPIGA MARUFUKU WIMBO WA SHIKA ADABU YAKO WA MSANII NAY WA MITEGO


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.
Sambamba na kuufungia wimbo huo, BASATA litampa karipio kali Msanii huyo na kumwagiza kuacha mara moja kujihusisha kwa namna yoyote na tabia ya kuutangaza wimbo au kuusemea katika vyombo vya habari vinginevyo hatua kali zaidi na...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani