BASATA yaonya wasanii dhidi ya lugha chafu, maadili wakati huu wa kampeni za kisiasa

_DSC3283

Katibu Mtendaji, Basata, Godfrey L. Mngereza.

Katika siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la wasanii kuvunja maadili, kukaidi adhabu na kutumia lugha chafu kwa makusudi katika kazi za Sanaa hususan muziki hali ambayo imezua malalamiko, masikitiko na hofu kwa jamii ambayo ni walaji wa kazi za Sanaa.

Lugha hiyo chafu ambayo inajidhihirisha kwa matusi ya wazi, maneno ya uchochezi, kashfa, kejeli, dharau na udhalilishaji wa kada mbalimbali za kijamii wakiwemo viongozi wa kitaifa inaonesha wazi kulenga katika kuigawa jamii na kufifisha amani, upendo, uzalendo na ustaarabu tuliokuwa nao watanzania.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa misingi ya Sanaa Duniani kote kazi zote za Sanaa zinapaswa ziwe ni zenye kuonya, kuelimisha, kuadabisha, kukosoa, kuburudisha, kuhamasisha na kuchochea maendeleo chanya katika jamii na siyo kuigawa au kuivuruga jamii.

Ndiyo maana msanii anayefanya kazi zake kwa kuzingatia misingi ya Sanaa anatambuliwa kuwa ni kioo cha jamii, kiongozi na pia ni mwalimu wa yale yote yaliyo mema katika jamii inayomzunguka.

Kinyume na misingi hiyo ya Sanaa, baadhi ya Wasanii, studio za kurekodia na kutengenezea muziki, vyombo vya habari vya kielektroniki na mitandao ya kijamii ama kwa kutumiwa au kwa utashi wao binafsi wamekuwa wakijihusisha na Sanaa zenye viashiria vya uchochezi na kuvunja misingi ya weledi katika Sanaa hususan katika kipindi hiki cha kampeni na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Aidha, baadhi ya Wasanii wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya vyama vya Siasa au wagombea na kujikuta wakitumiwa vibaya na kuvunja misingi ya Sanaa kwa faida za kisiasa. BASATA linapenda kutoa maagizo yafuatayo:

1.Wasanii wana haki zote za kikatiba na kidemokrasia kushiriki shughuli za Siasa lakini wanawajibika kwa kiwango cha hali ya juu kulinda misingi ya weledi, maadili, miiko na hadhi yao kama inavyofanyika katika tasnia zingine.

2.Wasanii wanapaswa kutambua kwamba kuna maisha na Taifa baada ya uchaguzi mkuu. Umoja wa kitaifa na umoja baina ya wasanii wa kada zote za Sanaa ndiyo utakuwa msingi mkuu wa kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla pasipo kugawanyika katika misingi ya itikadi za kisiasa

3.Wasanii wasitumie nafasi na umaarufu wao kuligawa taifa, kukashifu viongozi wa kitaifa, kudharau mamlaka, vyama na makundi mbalimbali katika jamii kwa kile kinachoitwa ushabiki wa kisiasa. Ieleweke kuwa Serikali haitafumbia macho wale wote watakovunja sheria, kanuni na taratibu. Tukumbuke kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

4.Ijulikane kuwa wasanii kama kundi muhimu katika kipindi cha kampeni za kisiasa ni sawa na watu wengine wanaopewa kazi ili kutimiza lengo lililokusudiwa. Wasanii wasitumiwe kama vyombo tofauti na watu wengine.

BASATA linatoa onyo kali kwa msanii yeyote atakayeendelea kukaidi, kuvunja maadili na kusambaza kwa njia yoyote ile kazi ya Sanaa yenye ukengeufu wa maadili.

BASATA linawatakia wasanii wote utekelezaji mwema wa maagizo haya lakini kubwa kuliko yote kutambua kwamba tunatakiwa kujenga mshikamano, umoja wa kitaifa na kustawisha amani tuliyonayo ambapo ikitoweka itaathiri ufanisi wa Wasanii na kuirejesha itatugharimu sana.

Sanaa itumike kulinda amani, kujenga upendo, umoja wa kitaifa na mshikamano baina ya makundi mbalimbali ya kijamii.

SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

GPL

BASATA YAONYA LUGHA CHAFU NA MAADILI KWENYE KAMPENI

Katibu Mkuu Mtendaji Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), Geofrey Ngereza. BASATA YAONYA LUGHA CHAFU, MAADILI HUSUSAN KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU Katika siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la wasanii kuvunja maadili, kukaidi adhabu na kutumia lugha chafu kwa makusudi katika kazi za Sanaa hususan muziki hali ambayo imezua malalamiko, masikitiko na hofu kwa jamii ambayo ni walaji wa kazi za Sanaa. Lugha hiyo...

 

2 years ago

Michuzi

BASATA YAONYA LUGHA CHAFU, MAADILI HUSUSAN KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

KATIKA siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la wasanii kuvunja maadili, kukaidi adhabu na kutumia lugha chafu kwa makusudi katika kazi za Sanaa hususan muziki hali ambayo imezua malalamiko, masikitiko na hofu kwa jamii ambayo ni walaji wa kazi za Sanaa.
Lugha hiyo chafu ambayo inajidhihirisha kwa matusi ya wazi, maneno ya uchochezi, kashfa, kejeli, dharau na udhalilishaji wa kada mbalimbali za kijamii wakiwemo viongozi wa kitaifa inaonesha wazi kulenga katika kuigawa jamii na kufifisha...

 

2 years ago

Michuzi

BASATA YAONYA WASANII DHIDI YA MATAPELIBaraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawataka wasanii wote kuwa makini na wakuzaji Sanaa (Mapromota) au baadhi ya wanaojiita wadau wa Sanaa ambao wamekuwa wakitumia njia za kiulaghai na utapeli katika kujipatia faida na manufaa kupitia mgongo wa Wasanii.Baraza linatoa angalizo hili kufuatia kuwepo kwa ongezeko la matukio ya baadhi ya watu wanaojiita wadau wa Sanaa ambao wamekuwa wakiwadanganya wasanii na kuwalaghai kwa kuwaahidi fursa mbalimbali kama za maonesho ya ndani na nje ya nchi ambazo...

 

3 years ago

Vijimambo

BASATA YALAANI TABIA CHAFU NA ISIYO NA MAADILI ILIYOONESHWA NA MSANII SHILOLE

Tarehe: 14/05/2015TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba kwa hisia nchini Ubelgiji.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubeligiji hivi karibuni.

Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole...

 

2 years ago

Michuzi

BASATA YAAGIZA WASANII WOTE KUSAJILIWA NA YAONYA MAPROMOTA

BASATA LAAGIZA WASANII WOTE KUSAJILIWA, LAONYA MAPROMOTA WATAKAOTUMIA WASANII WASIOSAJILIWA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawataka wasanii wote nchini kuhakikisha wamesajiliwa na kuwa na vibali vya Baraza kwani kufanya vinginevyo ni kuvunja sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha BASATA ambayo inamtaka mtu yeyote anayejihusisha na shughuli za Sanaa kuwa amesajiliwa na kupewa kibali na BASATA.
Aidha, BASATA linawaagiza Wakuzaji Sanaa wote (Mapromota) wanaoendesha matukio ya...

 

3 years ago

GPL

BASATA YALAANI TABIA CHAFU NA ISIYO NA MAADILI ILIYOONESHWA NA MSANII SHILOLE KWENYE ONESHO LAKE NCHINI UBELIGIJI

Tarehe: 14/05/2015 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba kwa hisia nchini Ubelgiji. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubeligiji hivi karibuni. Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na… ...

 

3 years ago

Michuzi

BASATA YALAANI TABIA CHAFU NA ISIYO NA MAADILI ILIYOONESHWA NA MSANII SHILOLE KWENYE ONESHO LAKE NCHINI UBELGIJI

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubelgiji hivi karibuni.
Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa...

 

3 years ago

Michuzi

Mh. Pindi Chana azindua kampeni ya Mpe riziki si matusi yenye lengo la kuondoa lugha chafu na matusi kwa wanawake wa sokoni

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb) akizundua kampeni ya Mpe riziki si matusi yenye lengo la kuondoa lugha chafu na matusi kwa wanawake wa sokoni na wanaofanya shughuli zao katika sekta zisizo rasmi. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Belinda Jijini Dar es salaam tarehe 27 Februari 2015. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya Mpe riziki si matusi yenye lengo la...

 

1 year ago

Bongo5

Waziri Nape adai BASATA wanaonana na wasanii wakati wa kufungia nyimbo zao

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye amekiri kuwepo kwa udhaifu katika sheria ambazo zinaliongoza Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) lililopewa dhamana ya kusimamia na stawisha shughuli za sanaa nchini.

Waziri Nape

Waziri Nape amedai kwa sasa baraza hilo linakutana na wasanii wakati wa kuzifungia kazi zao pale wanapokiuka maadili ya kazi za sanaa.

“BASATA ambalo ndio baraza lipo chini yangu sio rafiki kwa msanii,” Waziri Nape alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM....

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani