Bei ya vifaranga vya kuku wa nyama yapaa, Serikali yaombwa kuingilia kati

800px-Cornish_Rock_broiler_chicks

Wauzaji wa vifanga vya kuku wa nyama wameiomba serikali kuingilia kati kunusuru kufa kwa biashara ya kuku wa nyama kutokana na walichodai ni kuzuiwa kuingizwa kwa vifaranga hivyo na mayai kutoka nje ya nchi huku wazalishaji wa ndani wakishindwa kumudu soko jambo ambalo limewakatisha tamaa wafugaji.

Wakizungumza na channel ten wauzaji wa vifaranga katika eneo la Tazara jijini dar es salaam wamesema kwa sasa bei ya vifaranga imepaa kutoka 1300-1500 hadi kufikia 1850 – 2200 kwa kifaranga kimoja huku bei hizo pia zikiongezeka kutegemeana na muda ambao mteja atahitaji kupata.

Hali hiyo imesababisha pia kupanda kwa bei ya kuku sokoni ambapo kwa sasa huuzwa kati ya 6500- 7500 ukilinganisha na awali ambapo walikuwa wakinunuliwa kutoka kwa mfugaji kati ya 5000 – 5700 huku wauza chipsi nao wakilalamikia udogo wa kuku wanaouziwa sokoni ikilinganisha na bei.

Channel ten inaendelea kuzitafuta mamlaka husika ili kupata ufafanuzi wa suala hili.

Share on: WhatsApp

The post Bei ya vifaranga vya kuku wa nyama yapaa, Serikali yaombwa kuingilia kati appeared first on Channel Ten.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

StarTV

Serikali yaombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi

Serikali imeombwa kuingilia kati na kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na uongozi wa Kiwanda cha karatasi cha Mgololo kilichopo wilayani Mufindi na ule wa waliokuwa watumishi wa Kiwanda hicho kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa ombi hilo kwa Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina alipotoa taarifa ya kushindwa kutatulika kwa mgogoro huo licha ya jitihada za kutafuta suluhu.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa...

 

8 months ago

Mwananchi

Mradi wa vifaranga vya kuku wawapandisha chati

Wanafunzi wawili wa kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara, wametawazwa kuwa wanasayansi wanaochipukia nchini, baada ya kubuni mradi wa kutotolesha vifaranga vya kuku kwa gharama nafuu.

 

3 years ago

Michuzi

NAFASI ZA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MASHINE ZA KUTOTORESHA VIFARANGA VYA KUKU.

Taasisi  ya  RafikiElimu  FOUNDATION  kupitia  MRADI  WA ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI  NA  VIJIJINJI inatangaza  nafasi  za   MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI WA  MASHINE  ZA  KUTOTOLEA  VIFARANGA  WA KUKU. Mashine   zitakazo fundishwa  kutengeneza  ni  INCUBATOR  ( MANUAL & AUTOMATIC) ZENYE  UWEZO  WA KUTUNZA  JOTO  KWA  SAA  48 PAMOJA  NA KUTOTORESHA  MAYAI   KUANZIA  240  HADI  5000.Vile  vile  yatatolewa  mafunzo  ya   UTENGENEZAJI  WA MAJIKO  SANIFU...

 

3 years ago

Dewji Blog

Nafasi za mafunzo ya utengenezaji wa mashine za kutotolesha Vifaranga vya Kuku.

OMARIBARAKA

Taasisi  ya  RafikiElimu  FOUNDATION  kupitia  MRADI  WA  ELIMU  YA  UJASIRIAMALI MIJINI  NA  VIJIJINJI  inatangaza  nafasi  za   MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI  WA MASHINE  ZA  KUTOTOLEA  VIFARANGA  WA  KUKU.

Mashine   zitakazo fundishwa  kutengeneza  ni  INCUBATOR   ( MANUAL & AUTOMATIC) ZENYE  UWEZO  WA  KUTUNZA  JOTO  KWA  SAA  48...

 

2 years ago

Dewji Blog

Silverlands Tanzania yapania kuinua uchumi kwa wananchi kupitia ufugaji wa vifaranga bora vya kuku

Kampuni ya Silverland Tanzania  inayojishughulisha na masuala ya uuzaji na usambazaji wa Chakula bora na Vifaranga bora vya kuku imeelezea kuwa,  tokea kuanzishwa kwake hapa Tanzania imekuwa ni mkombozi katika ukuaji wa uchumi baada ya jamii kuipokea vyema biashara yao hiyo.

Wakizungumza mapema leo Machi 20.2016 wakati wa kilele cha maonyesho ya bidhaa mbalimbali ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, wamebainisha kwa sasa suala la ufugaji limekuwa pana hivyo limeweza kuongzeza ajira na uchumi...

 

1 year ago

Dewji Blog

Mahindi, nyama ya kuku , ndizi na mihogo vyatajwa kuchangia kupanda kwa mfumuko wa bei ya taifa

Mfumuko wa Bei ya Taifa kwa mwezi Mei, 2016 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.1 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2016.

Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2016 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2016.

Kwa mujibu wa wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam, kuongezeka kwa mfumuko wa Bei...

 

9 months ago

Global Publishers

Serikali yapiga marufuku kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje

kuku-waliochinjwa

Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.

Katazo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na Kituo kimoja cha runinga ilipotaka kupata ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.

Ole Nasha amesema...

 

4 months ago

Michuzi

MAUAJI YA KIBITI, WANANCHI WAVITAKA VYAMA VYA SIASA KUINGILIA KATI

Na Mwandishi Wetu, Pwani
BAADHI ya wananchi wilayani Kibiti, mkoani Pwani, wamewataka viongozi wa vyama vya siasa vikubwa wilayani humo kukaa meza moja kuangalia namna ya kukemea vitendo vya mauaji vinavyoendelea kwenye ukanda huo.
Aidha wamesema kwa umoja wao kutawezesha kushirikiana na serikali kumaliza janga hilo. Pia wameiomba serikali kupeleka askari wa JWTZ kutanda katika wilaya za Rufiji na Kibiti hadi maeneo ya vijijini ili kudhibiti vitendo hivyo vinavyomaliza watu wasio na hatia.
Hata...

 

4 weeks ago

Channelten

Mvutano kuhusu viwango vya mishahara, Dk Shein aombwa kuingilia kati

5bf0Ali-Mohamed-Shein

Jumuiya ya Uwekezaji katika Sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI), imemuomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kuingilia kati mvutano uliojitokeza kuhusiana na viwango vipya vya mishahara ya kima cha chini vilivyopandishwa kutoka shilingi 145,000 hadi shilingi 300,000 bila ya kushirikishwa kwa wawekezaji katika sekta hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa na wawekezaji wa sekta hiyo, Mlezi wa ZATI Bwana Simai Mohamed Said...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani