Bendera ya Tanzania yameremeta katika sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya madola Glasgow, Scotland

 Jina la Tanzania linameremeta wakati wanamichezo wetu walipopita katika maandamano ya ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye sherehe kabambe za ufunguzi katika Uwanja wa Celtic Park jijini Glasgow, Scotland, uliobeba watazamaji 40,000 huku watu bilioni 1 wakiangalia live sherehe hizo kupitia katika TV zao. Takriban  mashabiki 100,000, na wanamichezo 4,000 kutoka katika nchi 71 zitakazoshindana wapo hapo kwa michezo hiyo ambapo hii ni mara ya 20 kufanyika toka ianzishwe. Sehemu ya...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

5 years ago

Michuzi

TIMU YA TANZANIA KATIKA MICHEZO YA JUMUIYA YA MADOLA YATUA JIJINI GLASGOW, SCOTLAND

 Timu ya Tanzania kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola imewasili katika  uwanja wa ndege wa Kimataifa Glasgow, Scotland jana usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya Shirika la ndege la Falme za Kiarabu (Emirates).

 Jumla ya wanamichezo 42 waliwasili Uwanjani hapo na kupokelewa  na Afisa Ubalozi wa Tanzania London Bw. Amos Msanjila. Pamoja na mapokezi na shamrashamra za wenyeji, baadhi ya Watanzania waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo...

 

5 years ago

Dewji Blog

Rais Kikwete akabidhi bendera timu ya taifa ya riadha itayoshiriki michuano ya jumuiya ya madola huko Glasgow, Scotland

ta6

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye hafla fupi ya kukabidhi bendera iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.(PICHA NA IKULU).

ta1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete...

 

5 years ago

Michuzi

Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya Jumuiya ya Madola huko Glasgow, Scotland.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa. Alisema  kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji wake na wako tayari kwa...

 

5 years ago

Michuzi

Timu ya Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola yakaribishwa rasmi leo katika kijiji maalum cha michezo hiyo Glasgow

Waogeleaji wa Tanzania Mariam Foum, Hilal Hemed na Ammaar Ghadiyali wakiwa tayari kwa michuano jijini Glasgow. Timu ya Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola imekaribishwa rasmi leo katika kijiji maalum cha michezo hiyo Glasgow,  Uskochi.Timu ya Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola imekaribishwa rasmi leo kayika kijiji maalum cha michezo hiyo Glasgow,  Uskochi.

 

5 years ago

Michuzi

RATIBA YA MABONDIA WA TANZANIA WANAOWAKILISHA TAIFA KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA SCOTLAND (NDONDI)

Hatimaye ratiba ya mchezo wa ngumi kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola imetolewa leo tarehe 24/07/14 baada ya zoezi la kupima uzito na afya lililofanyika kuanzia saa 2.00 hadi saa 4.00 Asubuhi kwa saa za Scotland, kwa mabondia na waamuzi wote wanaotegemea kushiriki mashindano hayo`1.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa mashindanoo yataanza  tarehe 25/07/14 na yatamalizika tarehe 02/08/14.katika ukumbi wa Secc (Hall 4A) na inaonyesha kuwa captain wa timu ya Tanzania Selemani kidunda ndiye atayeanza...

 

5 years ago

Michuzi

MH. NKAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA MICHEZO WA JUMUIYA YA MADOLA NCHINI SCOTLAND

Naibu Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Mhe. Juma Nkamia (wa pili kushoto mstari wa mbele) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Jumuiya ya Madola leo jijini Glasgow, Uskochi (Scotland). Mkutano huo unafanyika kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo ya Jumuiya hiyo, utakaofanyika keshokutwa haoa Glasgow. Agenda kuu ya Mkutano huo ni Michhezo kwa Maendeleo na Amani.

 

5 years ago

Mwananchi

Kumekucha mashindano ya Jumuiya ya Madola Glasgow

>Mashindano ya Jumuiya ya Madola yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo mjini Glasgow, Scotland, ikiwa ni michuano ya 20 tangu kuanzishwa kwake.

 

2 years ago

Channelten

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland anatarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini Tanzania

8227

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland anatarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini lengo la ziara hiyo ikiwa ni kueleza Viongozi wa Ngazi za Juu wa Taifa kuhusu mageuzi yanayofanywa na sekretarieti ya jumuiya hiyo ikiwemo kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka 12 hadi 6.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katibu mkuu wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Aziz Mlima amesema jumuiya pia inatarajia kuondoa vyeo vya naibu...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani