BENKI YA DUNIA YAONESHA NIA KUSHIRIKI UJENZI RELI YA ISAKA - KIGALI

Ujumbe wa Tanzania (kulia) na ujumbe wa Benki ya Dunia (kushoto) wakiwa katika majadiliano ya miradi ya maendelea inayotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka ujao wa fedha. Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop akitoa ufafanuzi wa miradi ambayo itatekelezwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bi. Mamta Murthi . Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akielezea miradi ambayo itatekelezwa kwa mwaka ujao wa fedha. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, Prof. Florens Luoga.
Na. WFM- Washington DC
Benki ya Dunia imeonesha dhamira ya kuisaidia Tanzania katika ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka kwenda Rusumo na baadae Kigali pamoja na miundombinu mingine ya usafirishaji  kama barabara ili kusaidia kuendeleza biashara na ustawi wa jamii kwa ujumla.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati wa majadiliano na wataalamu wa Benki ya Dunia yaliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, kwenye mikutano ya mwaka ya kipupwe inayoendelea mjini Washington DC Marekani.
Dkt. Mpango amesema kuwa miradi ya Kikanda ambayo Benki hiyo imeonesha nia ya kuitekeleza ni ile ya uboreshaji wa mazingira na bandari katika ziwa Victoria zikiwemo za mikoa ya Mwanza, Musoma na Kigoma na Bandari zilizoko katika Ziwa Tanganyika ambazo zitarahisisha usafiri wa kwenda Burundi na Congo.
‘Miradi hii ya Kikanda na Kitaifa ambayo Benki ya Dunia imepanga kuitekeleza kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa mwaka ujao wa fedha itahakikisha kunakuwa na mazingira endelevu na tija kwa kuwa inagusa nchi zote zinazozunguka maziwa hayo mawili’, alieleza Dkt. Mpango.
Amesema kuwa ni lazima kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kadri iwezekanavyo ili kuendelea kufaidi rasilimali za maziwa hayo makubwa  kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na nchi jirani zinazozunguka maziwa hayo.
Aidha amebainisha kuwa mwakani, Benki ya Dunia imeonesha nia ya kutoa fedha kwa ajili ya tekeleza mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji eneo la Ruhuji ambapo utakapokamilika unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 300.
‘Eneo hili la sekta ya umeme ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya viwanda kwa kuwa uchumi wa viwanda hauwezi kukua bila kuwepo umeme wa uhakika’ alifafanua Waziri Mpango.
Vilevile Benki ya Dunia (WB) imekubali kuisaidia Tanzania kutoa mafunzo katika uchambuzi wa miradi mbalimbali ili kusaidia Serikali ya Tanzania kutokuingia kwenye madeni makubwa zaidi ambayo hayawezi kulipika.
Waziri Mpango alieleza kuwa kutokuwa na ufanisi wa kutosha katika kuchambua miradi ambayo inagharamiwa na fedha za mikopo inasababisha nchi kubeba mzigo mkubwa wa madeni hivyo ni vyema Tanzania ikahakikisha kuwa miradi hasa ile inayogharamiwa kwa fedha za mikopo inachambuliwa vizuri ili mradi husika unapokamilika uweze kulipa deni.
Amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali itakua na miradi mingi ya kutekeleza, miongoni mwa miradi hiyo ni kupambana na tatizo la utapiamlo hivyo ni vema kama nchi ikaangalia namna bora ambayo Benki ya Dunia inaweza kusaidia katika utekelezaji wake.
“Kitaalamu mpaka mwanadamu anapofikisha siku 1000 ni kipindi muhimu sana kinachoamua maisha ya mwanadamu atakapokuwa mtu mzima atakuwa na uwezo gani wa kufikiri, kutokana na hali hiyo mtu ambaye atakua na utapiamlo uwezo wake utakua ni mdogo zaidi kulinganisha na mtoto aliyepata lishe bora’” alifafanua Dkt. Mpango.
Katika kutekeleza mradi huo Serikali itafanya kazi na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Taasisi ya Chakula na Lishe ili kuhakikisha kwamba Taifa linapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la utapiamlo.
Mikutano hiyo ya mwaka ya kipupwe kati ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na Wataalamu wa Benki ya Dunia imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa Tanzania itanufaika kutokana programu mbalimbali ambazo zitagharamiwa na Benki ya Dunia kwa mikopo nafuu.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 months ago

Michuzi

MAWAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WA TANZANIA NA RWANDA WAKUTANA KUJADILI MRADI WA UJENZI WA RELI YA ISAKA- KIGALI


Benny Mwaipaja, WFM

Mawaziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania na Rwanda wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.

Katika Mkutano huo wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana...

 

10 months ago

Michuzi

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA -AfDB KUSHIRIKI UJENZI WA RELI YA KATI YA KISASA TANZANIABenny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kushirikiana na Tanzania kujenga mradi mkubwa wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kuipatia mkopo wenye masharti nafuu.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.

Dkt. Weggoro amesema kuwa Benki yake...

 

1 year ago

Michuzi

BENKI YA UBL YAONESHA NIA YA KUWEKEZA KATIKA KILIMO NCHINI TANZANIA


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Benki ya UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni na pia kufanya kazi na Watanzania pamoja na Serikali yake. 
Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal Jamall wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Bw. Jamall alisema kuwa kwa sasa...

 

4 years ago

Mwananchi

Benki ya Dunia yainusuru reli ya kati

Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati ya Afrika Mashariki umeongezewa nguvu ya kifedha baada ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) kupitisha kiasi cha Dola300 milioni za Marekani (Sh490 bilioni) kugharimia sehemu ya reli hiyo.

 

4 months ago

AllAfrica.Com

Tanzania: Construction of Isaka-Kigali Standard Gauge Railway to Start This Year - Magufuli


AllAfrica.com
Tanzania: Construction of Isaka-Kigali Standard Gauge Railway to Start This Year - Magufuli
AllAfrica.com
Dar es Salaam — President John Magufuli and his Rwandan counterpart, Paul Kagame, have agreed to start the construction of the standard gauge railways (SGR) from Isaka to Kigali this year as part of efforts to connect Rwanda to the Dar es Salaam port ...
Rwanda, Tanzania agree on SGR from Isaka to KigaliIndependent
Magufuli dismisses proposal to extend presidential term in...

 

1 year ago

Michuzi

IRAN YAONESHA NIA KUWEKEZA NCHINI


Na Veronica Simba – Dodoma

Balozi mpya wa Iran hapa nchini, Mousa Farhang amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumzia uwezekano wa nchi za Tanzania na Iran kushirikiana katika sekta za nishati na madini.

Balozi Farhang alimtembelea Profesa Muhongo jana, Aprili 28, 2017 ofisini kwake mjini Dodoma.

Akizungumzia nia ya nchi yake kushirikiana na Tanzania katika sekta ya nishati, Balozi Farhang alimwambia Waziri Muhongo kuwa...

 

11 months ago

Zanzibar 24

UN yaonesha nia ya kuisaidia kifedha Zanzibar

Shirika la  Umoja wa Mataifa UN limesema itaisaidia  Zanzibar katika Nyanja mbalimbali za maendeleo  kwa  kuwawezesha kuwapatia Fedha watakazo weza kubuni miradi   ya maendeleo ili kuwakomboa wananchi katika hali gumu ya maisha.

Akizungumza katika ziara ya siku mbili iliyoandaliwa na UN  katika Mkoa wa kusini Unguja na Mkoa wa kaskazini Unguja  na Mkoa wa mjini Magharibu Mwakilishi Mkaazi Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez  amesema UN imejipanga kuwasaidia wananchi wa Zanzibar...

 

1 year ago

Michuzi

KOREA KUSINI YAONESHA NIA YA KUWEKEZA TANZANIA

                           Watanzania waliosoma Nchi Korea Kusini wameunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuleta wawekezaji ambao wanataka kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya nguo, vifaa tiba, uzalishaji wa nishati ya umeme wa jua, kilimo na katika sekta ya Sanaa,utamaduni na michezo.
Mwenyekiti wa Baraza la Uwekezaji kutoka Korea Kusini hapa nchini Kakono David ametoa kauli hiyo wakati anaongoza Ujumbe wa Baraza la Uwekezaji la Korea Kusini...

 

4 years ago

Habarileo

Paras India yaonesha nia kuwekeza afya nchini

UJUMBE wa uongozi wa juu wa Shirika la Afya la Paras la nchini India linalomiliki hospitali za ngazi ya kimataifa, umewasili jijini Dar es Salaam jana ambapo pamoja na mambo mengine umeanza mchakato kuwekeza katika sekta ya afya. Ujumbe huo ukiongozwa na Naibu Meneja wa Hospitali hizo anayehusika na Uhusiano wa Kimataifa, Anuradha Sharma, ulipokelewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart ambaye ni Mbunge wa zamani wa Njombe Magharibi, Yono Kevela.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani