Breaking : MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA USANDA - SHINYANGA USIKU HUU


Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nshoma Shija anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 mkazi wa Kitongoji cha Mabu,kijiji Shabuluba kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga (Vijijini) mkoa wa Shinyanga Nshoma Shija (70) ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

Malunde1 blog imeambiwa kuwa mwanamke huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake wakati anapika viazi nje ya nyumba yake majira ya saa moja usiku huu Jumamosi Aprili 21,2018. 
Taarifa zaidi tutawaletea

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Malunde

Breaking News : DIWANI WA CHADEMA KATA YA NAMAWALA AUAWA KWA KUKATWA KATWA MAPANGA USIKU HUU

Godfrey Luena enzi za uhai wake
Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Taarifa zilizothibitishwa na mbunge wa jimbo la Mrimba kupitia chama cha Demokrasia ma Maendeleo(CHADEMA) Mhe.Suzan Kiwanga zinaeleza kuwa diwani wa kata ya Namwawala kupitia Chadema ndugu.Godfrey Luena ameuwawa kwa kukatwakatwa na watu wasiojulikana usiku huu mara baada ya kuvamiwa akiwa nyumbani...

 

2 years ago

Malunde

MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SHINYANGA


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
***Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nyanzobe Maganga (50) mkazi wa Kitongoji cha Nzanza kijiji cha Puni kata ya Puni wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga amefariki dunia kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea jana Aprili 11,2017 majira ya saa tatu na dakika 50 usiku.
Wanasema mwanamke huyo akiwa na mjukuu wake nyumbani...

 

3 years ago

Mtanzania

Diwani CUF auawa kwa kukatwa mapanga

Na Renatha Kapaka, Bukoba

DIWANI wa Kata ya Kimwani Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Silvester Miga (55) wa Chama cha Wananchi (CUF), amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini, baada ya kuvamiwa na kukatwakatwa  mapanga nyumbani kwake.

Tukio la kuuawa kwa diwani huyo lilitokea usiku wa kuamkia jana, akiwa nyumbani kwake akiangalia taarifa ya habari katika runinga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, alisema Miga alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika...

 

1 year ago

Malunde

MWALIMU MKUU AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA


Na Jonathan Musa
Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumkata mapanga mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibumba B,Harun Musiba, iliyopo kata ya Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea usiku wa saa tano wa Januari 13,2018 wakati mwalimu huyo alipotoka kuangalia mpira kati ya Azam na URA ya inchini Uganda uliochezwa jana Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hawezi kuzungumzia sana kwa kuwa yuko njiani kwenda...

 

3 years ago

Michuzi

Breaking nyuzzzz.......: Askari Polisi auawa kwa kapigwa risasi jijini Dar usiku huu

Taarifa iliyotufikia usiku huu, inaeleza kuwa Askari mmoja wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyetambulika kwa jina la Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay Kinondoni Jijini Dar es salaam, ameuawa usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati akiwa kazini katika eneo la Sayansi Kijitonyama.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili...

 

1 year ago

Michuzi

MLINZI SUMA JKT AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA

Na Ripota Wetu, MbeyaJESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema watu wasiojulikana wamemvamia mlinzi wa SUMA JKT Chewe Wilson(34) na kumsababisha kifo baada ya kumkata mapanga sehemu za kichwani na mguu na kisha kupora silaha yake akiwa lindoni.


Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mohamed Mpinga amesema kuwa jeshi hilo limeendelea na jitihada zake za kukabiliana na matukio ya uhalifu ambapo kwa siku kadhaa sasa limekuwa likiendelea kufanya msako kwenye maeneo mbalimbali.

Kamanda...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Wanandoa wauawa kwa kukatwa mapanga usiku wakiwa wamelala

Mtu na mkewe wameuawa kwa mapanga wakiwa wamelala nyumbani kwao kwa kinachodaiwa walikuwa na kesi mbili za kugombea ardhi Baraza la Ardhi la kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho, Bunda, Mara. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 22, mwaka huu, katika kijiji cha Mariwanda, Hunyari. Ofisa tarafa ya Chamriho, Boniphace Maiga jana alithibitisha na kuwataja waliouawa kuwa ni Magina Masengwa (61) na mkewe, Sumaye Sebojimu (58) wa kitongoji cha Kiborogota kijiji cha Mariwanda. Maiga...

 

12 months ago

Malunde

ALIYEKUWA KATIBU MWENEZI WA CCM AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KISHA KUKATWA MAPANGA


Mtendaji wa Kata ya Mwandui iliyopo mwambao wa bonde la ziwa Rukwa, wilayani Sumbawanga mkoani hapa, Benedict Chapewa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, Mei 2,2018.
Kamanda Kyando amesema Chapewa ambaye amewahi kuwa Katibu Mwenezi, CCM Wilaya ya Sumbawanga, alivamiwa na kundi la watu wasiojulikana wakati akiwa anakunywa pombe katika moja ya baa anayomiliki...

 

3 years ago

MillardAyo

Taarifa ya Polisi Tanga kuhusu Watu 8 kuuwawa kwa kukatwa mapanga saa saba usiku

Local news

Kamanda wa Polisi Tanga Leonard Paul amesema ilikua saa saba usiku wa kuamkia May 31 2016 kwenye kitongoji cha Kibatini kata ya Mzizima wilaya ya Tanga umbali wa kilomita 40 – 45 kutoka Tanga mjini sehemu ambako kuna msitu kabla ya kukuta nyumba zipatazo 20 Majambazi walivamia wakiwa na visu na mapanga. Walivamia nyumba tatu na kuua watu […]

The post Taarifa ya Polisi Tanga kuhusu Watu 8 kuuwawa kwa kukatwa mapanga saa saba usiku appeared first on MillardAyo.Com.

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani