Breaking nyuzzzz.......: Askari Polisi auawa kwa kapigwa risasi jijini Dar usiku huu

Taarifa iliyotufikia usiku huu, inaeleza kuwa Askari mmoja wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyetambulika kwa jina la Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay Kinondoni Jijini Dar es salaam, ameuawa usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati akiwa kazini katika eneo la Sayansi Kijitonyama.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZ.....: MSHAMBULIAJI DANNY MRWANDA AMWAGA WINO YANGA USIKU HUU

Mshambuliaji Danny Mrwanda amemwaga wino wa kuitumikia klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam kwa mkataba wa mwaka mmoja usiku huu.
Yanga imewafanyia umafia watani zao wa jadi Simba,ambayo ilionyesha nia kubwa ya kumuhitaji Mrwanda ikiwa ni kwa hudi na uvumba na tayariilishatangaza nia yake hiyo ya kutaka kumsajili.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga imeamua kumsajili Mrwanda kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro...

 

12 months ago

Malunde

Breaking : MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA USANDA - SHINYANGA USIKU HUU


Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nshoma Shija anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 mkazi wa Kitongoji cha Mabu,kijiji Shabuluba kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga (Vijijini) mkoa wa Shinyanga Nshoma Shija (70) ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

Malunde1 blog imeambiwa kuwa mwanamke huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake wakati anapika viazi nje ya nyumba yake majira ya saa moja usiku huu Jumamosi Aprili 21,2018. 
Taarifa zaidi tutawaletea

 

3 years ago

Michuzi

Breaking nyuzzzz....: Bodaboda wafunga Barabara ya Mandela usiku huu baada ya mwenzao kugongwa

 Waendesha pikipiki zipakiazo abiria jijini Dar (Bodaboda) usiku huu wamefunga Barabara ya Mandela eneo la Riverside, Ubungo kwa kupanga mawe na kuegesha pikipiki zao, baada ya mwenzao mmoja kugongwa na gari ambayo ilitoweka eneo la tukio. Wamedai kuwa wameamua kuchukua uamuzi huo wa kafunga Barabara hiyo, kwa kuwa wamekuwa wakidharauliwa na watu wenye magari, hivyo wamechukua uamuzi huo kushinikiza na wao kuheshimiwa kama vyombo zingine vya usafiri.

 

1 year ago

Malunde

Breaking News : DIWANI WA CHADEMA KATA YA NAMAWALA AUAWA KWA KUKATWA KATWA MAPANGA USIKU HUU

Godfrey Luena enzi za uhai wake
Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Taarifa zilizothibitishwa na mbunge wa jimbo la Mrimba kupitia chama cha Demokrasia ma Maendeleo(CHADEMA) Mhe.Suzan Kiwanga zinaeleza kuwa diwani wa kata ya Namwawala kupitia Chadema ndugu.Godfrey Luena ameuwawa kwa kukatwakatwa na watu wasiojulikana usiku huu mara baada ya kuvamiwa akiwa nyumbani...

 

5 years ago

Michuzi

Breaking Newssss: moto wateketeza soko la mitumba la karume jijini Dar usiku huu

Pichani ni mwanga wa moto unaotoka ndani ya soko la mitumba la Karume lililopo maeneo ya Ilala jirani na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam  ambalo linateketea na moto usiku huu.  Taarifa zilizotufikia katika meza ya usiku zinasema kuwa moto huo ulianza kidogo kidogo katika baadhi ya vibanda ambavyo wenye navyo walikuwa hawapo, kabla ya kushika  kasi na kuteketeza kila kitu kilichopo kwenye eneo  hilo. Tunafuatilia kujua kama kuna watu walioathirika na moto huo pamoja...

 

2 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZ......: GARI YATEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR JIONI HII

Gari aina ya Nissan x-trial ambalo namba zake za usajiri hazikuonekana kwa haraka likiwa limeanza kushika moto upambe wa mbele na kupelekea kuteketea gari lote. tukio hilo limetokea jioni hii kando ya barabara ya Nyerere na usoni kabisa mwa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii, Jijini Dar es salaam, huku baadhi ya wasamalia wakijaribu kuokoa sehemu ya vitu vilivyokuwemo ndani ya gari hilo. hakuna alepoteza maisha wala kujerugiwa katika ajali hii. Chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika....

 

1 year ago

Malunde

JAMBAZI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKIDAIWA KUTAKA KUPIGA ASKARI POLISI SHINYANGAMtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Joseph Dogani (50) mkazi wa kata ya Ndala Mjini Shinyanga anayedaiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi sehemu mbalimbali za mwili wake akidaiwa kutaka kuwapiga risasi askari polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Januari 2,2018,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema tukio hilo limetokea Januari 1,2018 saa 9:45 alasiri.
Amesema Joseph Dogani alifariki papo hapo baada ya kupigwa risasi na polisi baada ya...

 

4 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZ.....: KITUO CHA POLISI IKWIRIRI,RUFIJI CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI,ASKARI WAWILI WAUWAWA

Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii,inaeleza kuwa majambazi yamevamia kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua Askari wawili na kupora silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar  aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
 Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza...

 

2 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZ....: JESHI LA POLISI LAWASIMAMISHA KAZI ASKARI 12 WALIOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Kufuatia tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa ili uchunguzi ufanyike dhidi yao. 
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita, IGP Mangu alisema ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo,...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani