BREAKING NYUZZZZZ: MAHAKAMA YAMKUTA LULU NA KESI YA KUJIBU KUHUSU KIFO CHA KANUMBA

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo Oktoba 23, 2017 imemkuta Msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael Maarufu kama Lulu, anakesi ya Kujibu.
Ni kuhusu tuhuma zinazomkabili za kumuua msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba ambaye pia alikuwa ni mpenzi wake, April 6 mwaka 2012.Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao kwa kuita mashahidi wanne.
Kesi imeahirishwa hadi saa tano kamili ambapo Lulu ataanza kujitetea.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Malunde

MAHAKAMA YASEMA LULU ANA KESI YA KUJIBU KIFO CHA KANUMBA

Mahakama Kuu imesema msanii wa kike katika fani ya uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu anayekabiliwa na kesi ya kuua bila ya kukusudia ana kesi ya kujibu.
Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa fani hiyo, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika amesema baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa...

 

2 years ago

Michuzi

MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta mshtakiwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ anayekabiliwa na shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ana kesi ya kujibu na anatarajiwa kuanza kujitetea, Novemba 14, mwaka huu.
Uamuzi huo umetolewa leo Oktoba 31/2017 na Hakimu Mkazi Flora Haule wa mahakama hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na zaidi ya mashahidi kumi  walioletwa mahakamani pale na upande wa Mashtaka.
Kabla ya kutolewa...

 

3 years ago

Global Publishers

Mahakama Yamkuta na Kesi ya Kujibu Mtuhumiwa wa Mauaji ya Mwangosi

Mwangosi

Daud Mwangosi enzi za uhai wake.

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa leo imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mjini Iringa, Pasificus Cleophace Simon katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten, Daud Mwangosi.

Daud Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

mwangosi 2

Mwangosi kabla ya kuuawa.

 

2 years ago

Zanzibar 24

Mahakama yakamilisha hukumu ya Lulu kifo cha Kanumba

Mahakama Kuu Dar es Salaam, imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela, muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael, maarufu ‘Lulu’, baada ya kumkuta na hatia ya kuua bila kukusudia.

Hukumu ya kesi hiyo imesomwa mapema leo na Jaji wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ambaye baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa mawakili wa upande wa mshtakiwa aliitoa hukumu hiyo.

Lulu, alishtakiwa kwa kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini, Steven Kanumba ambaye...

 

5 years ago

GPL

KESI YA KIFO CHA KANUMBA, LULU AKESHA AKIOMBA

Stori: imelda Mtema na Mayasa Mariwata
STAA wa Filamu ya Foolish Age, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema hivi sasa anakesha akiomba ili mambo yaende vizuri katika kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, Ijumaa lina maelezo yake ya kutosha. Lulu amemwambia paparazi wetu kuwa alishaanza kuyasahau matatizo hayo lakini hataweza kupingana na amri ya mahakama iliyopanga kuanza kusikiliza kesi hiyo...

 

5 years ago

GPL

KESI YA KIFO CHA KANUMBA... LULU AANIKA UKWELI

Stori: Waandishi Wetu
MWANGA umeanza kuonekana juu ya kesi inayomkabili staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia staa mwenzake wa muvi, Steven Charles Meshack Kusekwa Kanumba ambapo safari hii aliamua kukiri vipengele kibao, Risasi Mchanganyiko lina habari yote. Akikiri mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania juzi (Jumatatu) wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, nyota huyo aliweka wazi...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Mahakama yamtia jambajamba Lulu ajibu kifo cha Kanumba

Mahakama Kuu jijini Dar es salaam, imesema muigizaji  wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) ana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma za kuuawa kwa msanii Steven Kanumba , hivyo anatakiwa kujitetea.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mahakama kuu baada ya kufunga kusikiliza ushahidi upande wa mashtaka na kumtaka muigizaji huyo kuanza kujiandaa kwa ajili ya kutoa utetezi wake.

Wakili wa Elizabeth, Peter Kibatala ambaye ndiye anayemtetea muigizaji huyo, aliomba muda wa dakika 40 ili wajiandae kufanya hivyo,...

 

2 years ago

BBCSwahili

Mahakama yamhukumu 'Lulu' miaka 2 jela kwa kifo cha Kanumba

Mahakama kuu ya Dar es salaam imemhukumu muigizaji maarufu kama 'Lulu', kifungo cha miaka miwili baada ya kumtia hatiani kwa kumuua Steven Kanumba.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani