CCM Mkoa wa Magharibi Unguja wafanya tathmini ya uchaguzi wa chama na jumuiya

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Unguja kimesema kina matarajio ya kufanyika kwa ufanisi uchaguzi wa Chama na jumuiya ndani mkoa huo baada ya kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza katika mchakato huo hivi karibuni.

Akizungumza Katibu wa Mkoa huo, Bi. Aziza Ramadhan Mapuri mara baada ya kufanya ziara fupi katika  Wilaya za Dimani na Mfenesini na kuzungumza na wajumbe wa Kamati za Sekreterieti za wilaya 6hiyo kwa lengo la kufanya tathimini ndogo juu ya maendeleo na kasoro zilizopo katika  uchaguzi huo.

Amesema ziara hiyo imekuja baada ya wanachama kutojitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi kwa  ngazi za mashina na matawi ya jumuiya kutokana na kuwa na hofu iliyotokana na kutoelewa marekebisho ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, juu ya kipengele cha kinachosema kazi za muda wote kwa baadhi ya nafasi zinazogombewa.

Alisema wanachama wengi waliokuwa na nia ya kuchukua fomu walitawaliwa na hofu ya kuwa endapo watajitokeza kuwania nafasi za ngazi hizo watakuwa hawana fursa za kugombea nafasi zingine katika ngazi za juu.

Aidha Katibu huyo alifafanua kwamba nafasi zilizotajwa kuwa ni za muda wote ni zile za kiutendaji zikiwemo za Katibu na Mwenyekiti lakini zingine zilizobaki zinaruhusiwa kushika nafasi zaidi ya moja na kwa ngazi tofauti.

Pia alieleza kwamba chanzo cha kuwepo kwa ziara hiyo ni baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadalla kubaini mapungufu katika mchato huo na kuagiza ngazi husika za chama na jumuiya kutoa elimu na maelekezo ya kina juu ya changamoto hizo kwa viongozi wa ngazi zote ili nao wawaelimishe wanachama katika maeneo husika.

” Tunatarajia kuwa baada ya kuongezwa muda wa uchaguzi wanachama wetu wengi watajitokeza zaidi kuchukua fomu ili kupata viongozi wengi.”, alisema Bi. Aziza.

Hata hivyo alipongeza maamuzi ya busara na hekima ya kujenga chama yaliyofikiwa na Naibu Katibu Mkuu huyo kwa kuongeza muda wa uchukuaji wa fomu ambapo kwa mujibu wa taarifa ya awali uchaguzi wa ngazi za chama ulikuwa ufanyike April 17 hadi 31 mwaka huu lakini kwa sasa utafanyika April 25 hadi 31 mwaka huu.

Kwa upande wa uchaguzi huo kwa ngazi ya Jumuiya za chama utafanyika Juni 18 hadi 22 mwaka, na matarajio ya mkoa huo ni kuona muda uliobaki unatumiwa vizuri na Wanachama wa chama hicho kwa kuchukua fomu kwa wingi ili kupata viongozi na watendaji wenye sifa na vigezo vya kukiimarisha chama na jumuiya.

The post CCM Mkoa wa Magharibi Unguja wafanya tathmini ya uchaguzi wa chama na jumuiya appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

CCM Blog

WABUNGE WA VITI MAALUMU CCM MKOA WA DAR, WAFANYA ZIARA KUHAMASISHA WANACHAMA NA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA KUELEKEA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA UMOJA WA WANAWAKE WA CCM UWT

Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, akizungumza na Viongozi na Wanachama wa UWT, wakati wa ziara ya wabunge hao katika Wilaya ya Kinondoni, kuhamasisha wanachama juu ya uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama. Mkutano huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Ndugumbi, Magomeni Barafu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum CCM, Ikupa Alex.

 Baadhi ya Wanachama wa...

 

5 months ago

Michuzi

MASAUNI AFUNGUA MKUTANO WA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA UMOJA WA WAZAZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA DAR ES SALAAM

 Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam, mkutano huo umefanyika leo, katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu Mwenyekiti anayemaliza muda wake   wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Angela...

 

3 years ago

Michuzi

JUMUIYA YA WAZAZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA WAKE

  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed (kushoto) na Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje wakionesha daftari hilo baada ya kuzinduliwa. Viongozi wa meza kuu wakipiga makofi wakati wakiimba wimbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kabla ya kuzindua daftari hilo. Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mavela, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu,Katibu wa Jumuia...

 

5 months ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS APIGA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA CCM MKOA WA KUSINI UNGUJA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kusini Unguja akipiga kura kuchagua viongozi wa CCM mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika kwenye Hoteli ya Coconut Tree, Marumbi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja. Makamu wa...

 

8 months ago

Zanzibar 24

Operesheni za Polisi mkoa wa mjini magharibi Unguja

Kete 240 za dawa za kulevya na chupa 24 za pombe ya kienyeji zimekamatwa wakati wa operasheni za polisi katika mkoa wa mjini magharibi Unguja.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Unguja Haji Abdalla Haji wakati akizungumza na Zanzibar24 huko ofisini kwake Polisi Madema.

Kamanda Haji amesema kufuatia operasheni walizo zifanya kwa wiki hii mnamo tarehe 15, wamefanikiwa kukamata jumla ya kete 240 za dawa za kulevya na chupa 24 za pombe ya kienyeji zenye ujazo wa lita...

 

3 years ago

Michuzi

DK SHEIN AHUDHURIA MKUTANO WA MABALOZI MKOA WA MAGHARIBI UNGUJA

  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa Amani alipohudhuria katika mkutano wa Mabalozi wa Mkoa wa Magharibi Unguja akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mikoa ya Unguja Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono Mabalozi waliofika...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Ofisi ya chama cha soka wilaya ya Magharibi “B” Unguja yaanza kung’ara

Chama cha Soka Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kinaendelea na ujezi wake wa kuijenga upya ofisi yao iliopo Mwanakwerekwe Ijitimai ili kufikia vigezo vya vyama vya soka vya vilivypo zanzibar.

Ofisi hiyo kwasasa inafanyiwa ukarabati baada ya chama hicho kupata uhalali wa eneo hilo na kuamua kuijenga ofisi  hiyo mjengo wa kisasa kutokana na kuondolewa wasi wasi na kupewa warka halali wa eneo hilo ambapo ujenzi huo unatarajiwa kumalizika February 2017.

Ofisi hiyo inajengwa na Ukumbi wa kisasa...

 

3 years ago

Vijimambo

Dk Shein Afutarisha Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wengine katika futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,Wananchi na Waislamu wa Mkoa Mjini Magharibi wakiwa katika futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika viwanja vya Ikulu Mjini UngujaWananchi na Waislamu wa Mitaa mbali mbali katika Mkoa...

 

4 months ago

Michuzi

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA SINGIDA CHAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO

Na,Jumbe Ismailly SINGIDA 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimezindua kampeni zake za uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Kaskazini na kusisitiza juu ya kudumisha amani,utulivu na mshikamano uliopo hapa nchini.
Akizindua kampeni hizo zilizofanyika katika Kijiji cha Mtinko,Singida Vijijini,kwa niaba ya Katibu mkuu wa CCM taifa,Naibu katibu mkuu wa CCM,Tanzania bara,Rodrick Mpogolo alisema idadi kubwa ya wananchi wameendelea kukichagua chama cha mapinduzi kutokana na kuwa na mipango...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani