CCM Wete Pemba wachaguana

MKUTANO mkuu wa uchaguzi wa CCM wilaya ya Wete kisiwani Pemba, umemrejesha tena madarakani Kombo Hamad Yussuf, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo, baada ya kupata kura 134, dhidi ya mpinzani wake Ali Bakari Ali, aliejikuta na kura 128, ambazo hazikukumuwezesha kushika nafasi hiyo.

Mkutano huo pia, uliwachagua Rashid Hadid Rashid aliepata kura 185, Zulfa Abdalla Said kura 129 na Asaa Ali Salim aliejinyakulia kura 123 kuwa wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM taifa, baada ya kuwashinda wenzao kwenye kinyang’anyiro hicho.

Aidha mkutano huo mkuu wa uchaguzi uliofunguliwa na Makamu wa pili wa rais Zanzibar Mhe: Balozi Seif Ali Idd, uliwachagua Raya Mkoko Hassan aliepata kura 143 na Khamis Issa Khamis kwa kura 115, kuwa wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Mkoa wa kaskazini Pemba.

Wajumbe wengine 10 waliochaguliwa kwa ajili ya kuingia kwenye Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Wete ni pamoja na Hamad Ahmed Baucha, Omar Ali Omar, Khamis Dadi Khamis, Khamis Juma Silima.

Wengine ni Haji Hamad Bakar, Ali Hamad Khamis, Halima Shaame Hamad, Ali Juma Kombo, Ali Mgau Kombo na Salum Said Khamis.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Mwenyekiti mpya wa wilaya ya Wete Kombo Hamad Yussuf, aliwataka wajumbe wa mkutano huo na wanaccm wengine kuhakikisha wanashirikiana katika kukijenga chama chao.

“Uchaguzi umeshamalizika, sasa tuwe pamoja kukijenga chama chetu, ili wengine wavutike kujiunga na waliopo wasitamani kutoka”,alieleza.

Mapema akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, Mjumbe wa Halmashauri Kuuu wa CCM taifa Asia Sharif Omar, alisema sasa makundi basi baada ya kumalizika kwa uchaguzi.

Alisema makundi hayana msingi ndani ya CCM maana yakiendelezwa hadi yakikutana na uchaguzi mkuu ujao wa vyama vingi mwaka 2020, ni hasara kwao na chama chao.

Alieleza kuwa uchaguzi huo ulikuwa baina ya wanaccm wenyewe kwa wenyewe, hivyo hakuna sababu wala haki ya kuendeleza makundi, maana haukushirikisha vyama vyama vyengine.

“Mimi ninanchoamini uchaguzi umekamilika na sote sisi CCM ni washindi, illa viongozi wetu tumeshawapa sasa tushirikiane kuhakikisha tunakirejesha tena Ikulu chama chetu kwa shangwe kwa kila uchaguzi unapofanyika ”,alifafanua.

Katika hatua nyengine Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM, aliwataka viongozi waliochaguliwa kujipanga upya ili kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama.

Alisema dhamira ya CCM ni kuhakikisha kinaendelea kushika hatamu za uongozi na kuwaongoza wananchi wote kwa lengo la kuwaletea maendeleo bila ya ubaguzi.

Awali Mkutano huo mkuu wa CCM wa uchaguzi wilaya ya Wete ulifunguliwa na Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Mhe: Balozi Seif Ali Idd, ambae aliwataka wanaccm kuchagua viongozi imara, wenye nia ya kukijenga chama na wanachama wake.

NA HAJI NASSOR, PEMBA

The post CCM Wete Pemba wachaguana appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

GPL

KATIBU MKUU WA CCM, NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE WILAYA YA WETE MKOA WA KASKAZINI PEMBA

Pichani kati ni Meneja Utawala wa shirika la Ununuzi wa Karafuu (ZSTC), Bw.Issa Hassani akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kulia alipokwenda kutembelea Ghala la Karafuu na kuona zoezi la ununuzi wa Karafuu katika Bandari ya Wete,Kaskazini Pemba. Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako Kisiwani Pemba kwa ziara ya Kuhimiza na Kukagua utekelezaji wa ilani ya...

 

3 years ago

Michuzi

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO WILAYA YA WETE MKOA WA KASKAZINI PEMBA.

Pichani kati ni Meneja Utawala wa shirika la Ununuzi wa Karafu (ZSTC),Bwa.Issa Hassani akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kulia alipokwenda kutembelea Ghala la Karafuu na kuona zoezi la ununuzi wa Karafuu katika Bandari ya Wete,Kaskazini Pemba. Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako Kisiwani Pemba kwa ziara ya Kuhimiza na Kukagua utekeleza wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010. Ghala la Karafuu kama lionekanavyo...

 

3 years ago

Michuzi

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE WETE-KASKAZINI PEMBA,AWATAKA VIONGOZI WA CUF KUTENDA HAKI KWA WANANCHI.

Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukikatiza mapema jioni ya leo katikati ya msitu ukielekea katika kijiji cha Mnarani -Makangale kuzungumza na wanachama wa chama hicho,micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Vijana wapatao 105 waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM,katika kijiji cha Mnarani Makangale,ambapo alikwenda kushiriki ujenzi wa tawi lao liitwalo Maskani tuheshimiane.  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na...

 

3 years ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS WA TIMU YA JAMHURI YA PEMBA BW.SULEIMAN SALEH AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIIONI 8 MJINI WETE PEMBA

Timu kongwe visiwani Zanzibar Jamhuri ya Wete Pemba iliyoanzishwa mwaka 1954 imepokea vifaa mbali mbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 8 kutoka kwa Bw.Suleiman Saleh ambaye alimkabidhi mdaada huo. Mjini Wete Pemba jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba.

Bw..Saleh ambaye ni Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC alikabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo...

 

3 years ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS WA TIMU YA JAMHURI YA PEMBA BW.SULEIMAN SALEH AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA SHILINGI MILIONI 8 MJINI WETE PEMBA

Timu kongwe visiwani Zanzibar Jamhuri ya Wete Pemba iliyoanzishwa mwaka 1954 imepokea vifaa mbali mbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 8 kutoka kwa Bw.Suleiman Saleh ambaye alimkabidhi mdaada huo mjini Wete Pemba jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba.
Bw.Saleh ambaye ni Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC alikabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo viatu,...

 

3 years ago

Vijimambo

MAKAMU WA RAIS WA TIMU YA JAMHURI YA PEMBA BW. SULEIMAN SULEIMAN SALEH AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIIONI 8 MJINI WETE PEMBA

Timu kongwe visiwani Zanzibar Jamhuri ya Wete Pemba iliyoanzishwa mwaka 1954 imepokea vifaa mbali mbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 8 kutoka kwa Bw.Suleiman Saleh ambaye alimkabidhi mdaada huo. Mjini Wete Pemba jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba.Bw..Saleh ambaye ni Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC alikabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo...

 

2 years ago

Michuzi

UZINDUZI WA KIWANJA CHA BASKETBALL WETE PEMBA

 Baadhi ya Wanamichezo wa Michezo mbalimbali katika Wilaya ya Wete   wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Kiwanja cha Baskatball na ugawaji wa Vifaa mbali mbali vya Michezo katika Nyumba za  Polisi Mess Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana. Baadhi ya Wanamichezo wa Michezo mbalimbali katika Wilaya ya Wete   wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Kiwanja cha Baskatball na ugawaji wa Vifaa mbali mbali vya Michezo katika Nyumba za  Polisi Mess Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana. Rais wa Zanzibar na...

 

2 years ago

Michuzi

UZINDUZI WA KIWANJA CHA BASKETBALL WETE, PEMBA

 Baadhi ya Wanamichezo wa Michezo mbalimbali katika Wilaya ya Wete   wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Kiwanja cha Baskatball na ugawaji wa Vifaa mbali mbali vya Michezo katika Nyumba za  Polisi Mess Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Baadhi ya Wanamichezo wa Michezo mbalimbali katika Wilaya ya Wete   wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Kiwanja cha Baskatball na ugawaji wa Vifaa mbali mbali vya Michezo katika Nyumba za  Polisi Mess Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa...

 

3 years ago

Michuzi

WANANCHI WA WETE, PEMBA WAPEWA ELIMU YA KATIBA

SHEHA wa shehia ya Kipangani Ali Said Hamad akifungua mkutano wa kuelimisha katiba inayopendekezwa, ulioandaliwa na Kituo cha Hudma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba, kulia ni Hakimu wa Mahakama ya Ardhi mkoa kusini Pemba Salim Hassan Bakar na kushoto ni Mratibu wa ZLSC Fatma Khamis Hemed.MWANASHERIA wa serikali Albaghir Yakout Juma, akitoa ufafanuzi wa Katiba inayopendekezwa mbele ya wananchi wa wilaya ya wete Pemba, mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria ...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani