CHANETA YAANZISHA PROGRAMU YA KUHAMASISHA MCHEZO WA NETBALI NCHI NZIMA

Na. Jumbe Ismailly CHAMA cha Netbal Tanzania (CHANETA)  kimeanzisha Program maalumu ya kuhamasisha mchezo wa Netball kuanzia ngazi ya wilaya, Mkoa hadi Taifa  ili kuhakikisha kiwango cha mchezo huo kinakua kwenye maeneo yote nchini badala ya sasa ambapo baadhi ya mikoa mchezo huo umeanza kutoweka kabisa.Mjumbe wa Chaneta Taifa, Yasinta Silivester aliyasema hayo kwenye mafunzo ya walimu wa mchezo wa Netball yaliyohudhuriwa na walimu 19 wa shule za msingi na sekondari wa Mkoa wa Singida na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Mwenge mjini Singida.
“Mheshimiwa mgeni rasmi chama cha netball kimekuwa na Program sasa hivi ya kuhamasisha mchezo wa netball kuanzia ngazi ya wilaya,Mkoa hadi Taifa”alisisitiza Yasinta.
Kwa mujibu wa Yasinta mwezi wa nane,mwaka huu kutakuwa na semina ngazi ya taifa,hivyo walimu waliohudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika shule ya sekondari Mwenge,angependa wasinyimwe ruhusa ya kuhudhuria mafunzo hayo yatakayofanyika Mkoani Manyara.Hata hivyo kiongozi huyo wa kitaifa alisisitiza kwamba ni muhimu kwa walimu hao wakahudhuria kwenye mafunzo hayo ya kitaifa kutokana na Mkoa wa Singida kuwa bado upo nyuma sana katika mchezo wa netbali.
“Meshimiwa mgeni rasmi mimi kama mjumbe wa taifa wa chaneta nasimamia kanda za Kaskazini na kanda ya kati  yenye mikoa ya Manyara,Singida,Arusha,Kilimanjaro na Dodoma,kwa hiyo mwezi huu kulikuwa na semina ngazi ya basic ya Mkoa Kilimanjaro ,Manyara walifanya mwaka jana na mwaka huu Singida mwezi wa nane kutakuwa na semina ngazi ya taifa”aliweka bayana mjumbe huyo wa chaneta taifa.
Akizungumza na walimu wa michezo waliohudhuria mafunzo hayo ya siku tano,Afisa michezo wa Mkoa wa Singida,Martin Kapera pamoja na mambo mengine alitumia fursa kuvipongeza vituo  vya Televisheni vya Channel Ten Azamu kwa mchango wake wa kutangaza michezo katika Mkoa huo. Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo.Grace Irumba alisisitiza kwamba mchezo huo wa Netbali kidogo ulikuwa kama vile unataka kulala lala,lakini kwa uwezo wake Mungu uongozi wa Taifa na viongozi uliopo mikoani kila mmoja anataka kuuamsha mchezo huo katika Mkoa wake.
Katika risala ya wanasemina hao iliyosomwa na Luiza Mujah iliyataja malengo ya mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kupata ujuzi wa uamuzi wa mpira wa Netbali unaoendena na sheria mpya za mpira wa Netbali ili waweze kuutumia ujuzi huo kwenye maeneo yao                                                    Mjumbe wa kamati ya utendaji Taifa CHANETA,Yasinta Silivester akizungumza na walimu 19 waliohudhuria mafunzo ya siku tano ya mchezo wa Netiball yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Mwenye, mjini Singida. Afisa michezo wa Mkoa wa Singida,Henry Kapera akisaini vyeti vya kuhitimu mafunzo kwa walimu wa michezo wa Netibali Mkoani Singida. Mwalimu Luiza Mujah (mwenye fulana ya njano) akikabidhiwa na Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida, Henry Kapera cheti cha kuhitimu mafunzo ya mchezo wa Netibali.Washiriki wa mafunzo ya mchezo wa Netibali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi,ambaye pia ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida, Henry Kapera(aliyevaa fulana nyekundu), viongozi wa Chaneta Mkoa na Taifa. (Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Tanzania Daima

Wizara yaanzisha programu ‘Panda Miti Kibiashara’

WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, imeanzisha programu ya Panda Miti Kibishara (Private Forestry Programme). Mradi huo una lengo la kuwahamasisha...

 

1 year ago

Michuzi

TEMESA YAANZISHA PROGRAMU YA KUBAINI VIPURI BANDIA


Na Theresia Mwami TEMESA iringa
Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) imeanzisha program ya kubaini vipuri bandia kwa ajili ya kuboresha huduma za matengenezo ya magari na mashine mbalimbali.
Agizo hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt.Mussa Mgwatu alipotembelea karakana ya TEMESA mkoani Iringa kujionea jinsi karakana hiyo inayotumia kutumia mfumo huo wa kubaini vipuri bandia.
Dkt Mgwatu ameongeza kuwa mfumo huu umekuja wakati sahihi kwani kwa sasa kumekuwa na uingizwaji wa vipuri bandia...

 

2 years ago

Michuzi

NEC YAANZISHA PROGRAMU ENDELEVU ZA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA.

Na. Aron Msigwa – NEC, Musoma

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutekeleza programu endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura ili kuwaelimisha wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura kutekeleza wajibu na haki waliyonayo kikatiba ya kupiga kura katika chaguzi zijazo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Musoma kuhusu mkakati wa NEC wa kuwafikia wananchi moja kwa moja kuwapatia elimu ya mpiga...

 

4 years ago

Mwananchi

Chadema kutikisa nchi; Helikopta tatu kurushwa nchi nzima

>Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuanzia leo, kinarusha helkopta tatu kwa siku 14 mfululizo, katika  kutekeleza kampeni iliyopewa jina la Operesheni Pamoja Daima (ODB) itakayoendeshwa katika mikoa yote nchini.

 

3 years ago

Vijimambo

TBL YAANZISHA PROGRAMU YA MAFUNZO YA KUENDELEZA WAUZAJI WADOGO WADOGO WA VINYWAJI VYAO NCHINI

 Meneja Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Emma Oriyo  (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam , kuhusu maandalizi ya uzinduzi Programu ya mafunzo ya kuendeleza wauzaji wadogo wadogo wa vinywaji vya TBL nchini. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Dar es Salaam, Abel Swai Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Dar es Salaam, Abel Swai (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa...

 

3 months ago

BBCSwahili

Mtoto mwenye umri wa miaka 6, amebuni programu ya mchezo wa komputa

Mtoto mwenye umri wa miaka 6, amebuni programu ya mchezo wa komputa ambayo imebeba uhusika wake mwenyewe kama mtoto shujaa

 

1 year ago

Michuzi

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA ISTANBUL KWA NCHI ZILIZO KWENYE KUNDI LA NCHI MASIKINI DUNIANI KWA UPANDE WA AFRIKA

Tanzania imeshiriki katika Mkutano ulioitishwa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani kushiriki katika Mkutano wa kujadili utekelezaji wa Programu ya Istanbul (Istanbul Programme of Action - IPOA) kwa nchi zilizo kwenye kundi la nchi masikini barani Afrika. Mkutano huo umefanyika kwenye Hoteli ya Radisson Blu, Dakar, Senegal kuanzia tarehe 28 Februari hadi 1 Machi 2017.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Mhe. Bi. Maria...

 

1 year ago

Michuzi

MKUTANO WA KUJADILI UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA ISTANBUL KWA NCHI ZILIZO KWENYE KUNDI LA NCHI MASIKINI DUNIANI KWA UPANDE WA AFRIKA, DAKAR, SENEGAL, TAREHE 28 FEBRUARI NA 1 MACHI 2017

 Tanzania imeshiriki katika Mkutano ulioitishwa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani kushiriki katika Mkutano wa kujadili utekelezaji wa Programu ya Istanbul (Istanbul Programme of Action - IPOA) kwa nchi zilizo kwenye kundi la nchi masikini barani Afrika.

Mkutano huo umefanyika kwenye Hoteli ya Radisson Blu, Dakar, Senegal kuanzia tarehe 28 Februari hadi 1 Machi 2017. 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Mhe. Bi. Maria...

 

2 years ago

Habarileo

Bomoabomoa nchi nzima

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesimamisha kazi ya bomoabomoa kwa siku 15 kwa wavamizi waliojenga katika Bonde la Mto Msimbazi, Dar es Salaam na kuwataka wavamizi hao kubomoa wenyewe na kuondoka maeneo hayo, kabla ya kazi hiyo kuanza tena Januari 5, mwakani.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani