CHETI CHA KIFO CHAKWAMISHA KESI YA DK. MVUNGI

Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk. Sengondo Mvungi

Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk. Sengondo Mvungi

NA CHRISTINA GAULUHANGA-KISUTU

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeshindwa kuendelea na kesi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk. Sengondo Mvungi hadi hapo upande wa mashtaka utakapoleta cheti cha kifo cha mshtakiwa wa kwanza, Chibago Chiugati (33), anayedaiwa kufa akiwa gerezani.

Uamuzi huo umetolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas  Simba ambaye aliuagiza  upande wa mashtaka kuhakikisha unapeleka cheti cha kifo ili mahakama hiyo iweze kukiangalia na kujiridhisha ili kuondoa jina la mshtakiwa katika orodha ya washtakiwa.

“Hakuna namna nyingine ya kuliondoa jina la mshtakiwa Chiugati… nawaomba upande wa mashtaka mhakikishe cheti hicho kinapatikana mapema kwa sababu wenzetu wa magereza walileta taarifa mapema, hatuwezi kukubali kirahisi hadi cheti kitakapoonekana ndipo tutaliondoa jina lake,” alisema Hakimu Simba.

Katika kesi hiyo, kulikuwa na washtakiwa kumi ambapo wanne kati yao, waliachiwa huru baada ya kuonekana hawana hatia ambao ni Ahmad Kitabu (30), Zacharia Msese (33), Masunga Makenza (40) na John Mayunga (56).

Wakili wa Serikali, Pamela Shinyambala, alidai hivi karibuni kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), alisema hana nia ya kuendelea na kesi kwa washtakiwa hao kwa mujibu wa kifungu 91 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Wakili Shinyambala, alidai DPP ataendelea na mashtaka kwa washtakiwa sita waliobaki ambao ni Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Msungwa Matonya (30) na Longishu Losingo aliyewahi kuwa mlinzi wa marehemu Dk. Mvungi.

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

GPL

KESI KIFO CHA KANUMBA, SURA MPYA!

Stori: Shakoor Jongo Jipya! Baada ya kimya cha muda mrefu, imefichuka kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ imechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa kimyakimya, Ijumaa Wikienda limenasa kinachoendelea. Staa wa sinema za Kibongo, Lulu Elizabeth Michael, 'Lulu".
WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA
Uchunguzi wa gazeti hili… ...

 

4 years ago

GPL

KESI YA KIFO CHA KANUMBA, LULU AKESHA AKIOMBA

Stori: imelda Mtema na Mayasa Mariwata
STAA wa Filamu ya Foolish Age, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema hivi sasa anakesha akiomba ili mambo yaende vizuri katika kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, Ijumaa lina maelezo yake ya kutosha. Lulu amemwambia paparazi wetu kuwa alishaanza kuyasahau matatizo hayo lakini hataweza kupingana na amri ya mahakama iliyopanga kuanza kusikiliza kesi hiyo...

 

4 years ago

GPL

KESI YA KIFO CHA KANUMBA... LULU AANIKA UKWELI

Stori: Waandishi Wetu
MWANGA umeanza kuonekana juu ya kesi inayomkabili staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kumuua bila kukusudia staa mwenzake wa muvi, Steven Charles Meshack Kusekwa Kanumba ambapo safari hii aliamua kukiri vipengele kibao, Risasi Mchanganyiko lina habari yote. Akikiri mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania juzi (Jumatatu) wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, nyota huyo aliweka wazi...

 

7 months ago

BBCSwahili

Kesi ya muhubiri aliyetabiri kifo cha rais Mugabe kuendelea

Muhubiri wa Zimbabwe Phillip Mugadza ameshindwa katika harakati zake za kutaka mahakama ya juu nchini humo kufutilia mbali mashtaka dhidi yake kwa kutabiri kwamba rais Mugabe atafariki baadaye mwezi huu

 

6 months ago

Malunde

MAHAKAMA YASEMA LULU ANA KESI YA KUJIBU KIFO CHA KANUMBA

Mahakama Kuu imesema msanii wa kike katika fani ya uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu anayekabiliwa na kesi ya kuua bila ya kukusudia ana kesi ya kujibu.
Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa fani hiyo, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika amesema baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa...

 

4 years ago

Mwananchi

Upelelezi kesi ya Dk Mvungi kitendawili

Upelelezi wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi bado ni kitendawili.

 

1 year ago

Habarileo

Washitakiwa 4 kesi ya Mvungi waachiwa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya 10 waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya bila ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi.

 

1 year ago

Mtanzania

WANNE WAACHIWA KESI YA DK. MVUNGI

new-law

Na PATRICIA KIMELEMETA – DAR ES SALAAM

WASHTAKIWA wanne kati ya kumi wanaodaiwa kumuua aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi, wameachiwa huru.

Waliachiwa jana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwaona hawana hatia.

Washtakiwa hao ni Ahmad Kitabu (30), Zacharia Msese (33), Masunga Makenza (40) na John Mayunga (56).

Akisoma uamuzi huo mahakamani hapo jana, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas  Simba, Wakili wa Serikali, Pamela Shinyambala,...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani