daraja la kilombero mkoani morogoro lakamilika

Hali ya "Sanda Mkobani" ilivyokuwa wakati wa kuvuka mto Kilombero mkoani Morogoro kabla ya ujenzi wa daraja.Ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero uliopangwa kukamilika mwezi Februari 2017, sasa umekamilika kwa 100% na liko tayari kuzinduliwa.  Daraja hilo linalounganisha wilaya mbili za mkoa wa Morogoro (Ulanga na Kilombero) pamoja na Mkoa wa Ruvuma, litaokoa maisha ya wananchi wa wilaya hizo ambao katika kipindi chote cha mwaka walikuwa wakipata shida kuvuka mto huo huku shughuli za usafirishaji wa mazao ya mpunga, ufuta, mahindi, ufugaji na madini zitarahisishwa,  kuongeza pato na kukuza uchumi wa Taifa.Pia kukamilika kwa daraja la Mto Kilombero kutarahisisha usafiri kutoka Dar kwenda Songea – Ruvuma ambapo ni mbali mfupi sana kwa kupitia Mikumi-Ifakara-Mahenge mpaka Songea kuliko kupitia Iringa-Njombe mpaka Songea.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 months ago

Michuzi

Ajali ya gari aina ya Toyota Noah Kilombero- Mikumi mkoani Morogoro

 Wasamaria wema akiwemo Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Kituo cha ITV , Mkoa wa Morogoro, Hussein Nuha wakitoa msaada wa kusaidia mmoja wa majeruhi ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ambaye ni dereva wa gari Toyota Noah namba ya usajili T 782 DKV  inayofanya safari zake mji wa Ruaha   Kilosa - Mikumi baada ya gari hiyo kupinduka  eneo la Kijiji cha Lumango, katika  kona kali ya barabara ya Kilombero- Mikumi  katika ajali hiyo hapakutokea kifo chochote na majeruhi wote...

 

2 years ago

Michuzi

Programu ya LTSP kuvipatia Hatimiliki ya Ardhi Vijiji 37 vya MALINYI, KILOMBERO na ULANGA mkoani Morogoro

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume ya taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi Dkt Stephen Nindi ( Kulia ), akikabidhi Mpango wa miaka 20 wa Matumizi Bora ya Ardhi wa Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mpango huo umelenga kutunza mazingira na Bio anuai Zilizopo nchini pamoja na kumnufaish Mwananchi wa Kipato cha kawaida. Kiongozi wa Urasimishaji kupitia Programu ya LTSP, iliyo Chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi SAGWILE MSANANGA akitoa maelezo kuhusu Mradi wa kuwezesha...

 

8 months ago

Michuzi

DARAJA LA MTO KALAMBO LAKAMILIKA

Serikali kupitia Wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Rukwa imekamilisha ahadi yake kwa wananchi ya kuwapunguzia changamoto ya usafirishaji wa abiria na mzigio kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la mto Kalambo pamoja na barabara ya Sumbawanga Matai hadi Kasanga port (112km) ambapo Kilomita 71.4 zimeshawekwa lami.
Akizungumza mara baada ya kukagua daraja na barabara hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa...

 

8 months ago

Michuzi

DARAJA LA FURAHISHA MWANZA LAKAMILIKA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha na barabara ya kutoka Furahisha hadi Pasiansi yenye urefu wa KM 2.7, imekamilka kwa asilimia 99 Mkoani Mwanza.

Prof. Mbarawa amesema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujezi wa daraja hilo katika ziara yake ya kikazi mkoani humo na kuridhishwa na ukamilishwaji wa ujenzi wake. “Daraja hili litaondoa changamoto kwa wananchi wanaotembea kwa miguu...

 

2 years ago

Michuzi

BALOZI SIMBA AWAPONGEZA WAOKOAJI AJALI YA MV KILOMBERO, AMALIZA ZIARA YAKE YA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO YA JESHI LA MAGEREZA MKOANI MOROGORO.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani...

 

2 years ago

Michuzi

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MAAFISA WATEULE DARAJA LA KWANZA , MKOANI MOROGORO

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani). Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.  Kamishna Jenerali...

 

4 years ago

Mwananchi

JK azindua ujenzi Daraja la Kilombero

Rais Jakaya Kikwete amezindua miradi miwili mikubwa ya kiuchumi na kijamii katika Wilaya za Ulanga na Kilombero, ukiwamo ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero.

 

9 months ago

Mwananchi

Daraja la mto Kilombero lafungwa kupisha ujenzi

Wakazi wa wilayani Kilombero wanatarajia kurejea katika matumizi ya kivuko katika kuvuka mto Kilombero kufuatia daraja la mto Kilombero linalounganisha wilaya za Ulanga na Malinyi kufungwa kwa muda.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani