DCEA waeleza walivyomnasa Shamim Mwasha na mumewe akiwa darini kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema mfanyabiashara Abdul Nsembo maarufu kama Abdukandida ni papa (kinara) katika mtandao wa biashara ya dawa hizo na anajulikana katika nchi mbalimbali zikiwamo Brazil na Marekani.
Nsembo alikamatwa na DCEA Mei Mosi mwaka huu, usiku wa manane akiwa amejificha juu ya dari nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam, mpaka sasa anaendelea kushikiliwa na mke wake Shamim Mwasha kwa kudaiwa kukutwa na gramu kati ya 560 hadi 700 za heroin...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 week ago

Malunde

Shamim Mwasha na mumewe wafikishwa mahakamani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewapandisha kizimbani Shamim Mwasha na mume wake, Abdul Nsembo kwa tuhuma za kusafrisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Costantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, alidai  kuwa Mei Mosi mwaka huu kwa pamoja washtakiwa hao wakiwa meneo ya Mbezi Beach walisafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 232.70 huku wakijua kufanya hivyo...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Mbowe mikononi mwa polisi kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kufuatia kukaidi wito wa jeshi hilo alipotakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati kwa ajili ya mahojiano kufuatia tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amethibitisha taarifa hizo kuwa wanamshikilia kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa CHADEMA Boniface Makene, amesema...

 

2 years ago

Bongo5

Jeshi la polisi ladaiwa kumshikilia Vanessa Mdee kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia muimbaji Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita.

Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi...

 

2 years ago

Ippmedia

Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam yawashikilia watu 84 kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Watu 84 wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya wanashikiliwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam pamoja na kete 18 za dawa za kulevya aina ya Kokeini,Heroine na bangi.

Day n Time: Jumatano Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

2 years ago

Ippmedia

Zaidi ya watu 349 wamekamtwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya jijini Dar es Salaam

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salam kamishna Simon Sirro amesema zaidi ya watu 349 wamekamtwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya toka kuanza kwa kampeni ya kupambana na dawa za kulevya wakiwemo askari wa jeshi la polisi tisa kati ya kumi na mbili wanaotuumiwa kushirikiana na mtandao huo ambao watafikishwa katika tume ya maadili.

Day n Time: Alhamisi Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

2 years ago

Zanzibar 24

Shamsa Ford anena mazito kwa mumewe ambaye anapanda Mahakamani leo kwa tuhuma za dawa za kulevya

nilipoolewa nilijua ipo siku nitapitia hivi vitu huzuni,furaha, maudhi, kudharauliwa, kuchekwa na nk.ila pamoja na yote hayo haitabadilisha mapenzi yangu kwa mume wangu kipenzi. Nina amini kuwa wewe ni mume aliyenipa Mungu na wala Mungu hakutukutanisha kwa bahati mbaya.Dunia nzima ikuzomee na kuamini kile wanachoamini lakini jua una mke anayekupenda kwa dhati .Ninakujua, ninakuamini na kukupenda sana ndomaana niliolewa na wewe kwasababu nilijua utakuwa baba bora kwa mwanangu kama ambavyo...

 

2 years ago

Michuzi

NEWZ ALERT:WATUMISHI WAWILI WA TRA WANASHIKILIWA NA VYOMBO VYA DOLA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA

Watumishi Wawili Wa TRA wanashikiliwa na vyombo vya dola wakituhumiwa kujihusisha na upitishaji Wa kemikali ambazo hutumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya Heroin.
Kukamatwa kwa watumishi hao wa umma kumetangazwa  leo na Kamishina Wa Operasheni ya Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya Mihayo Msekela.Kamishina wa Oparesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela akifafanua japo alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali...

 

1 week ago

Michuzi

TUHUMA ZA KUKUTWA NA GRAMU 232.70 ZA HEROINE ZAWAFIKISHA KORTNI SHAMIM NA MUMEWE

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MMILIKI wa Blog ya 8020 Fashion, Shamim Omary Mwasha (41) na mume wake, Abdul Nsembo(45) wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa wakikabiliwa na tuhuma za kusafrisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.
Akisoma hati ya mashtaka leo Mei 13, 2019  Wakili wa Serikali, Costastine Kakula amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi, Steven Mhina kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo Mei 1,2019 wakiwa huko Mbezi...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani